Wana JF,
Kinachofanywa na Nchimbi ni hadaa na hii inadhihirisha ulehelege wa Serikali iliyopo madarakani na ambayo imekosa mwelekea kwa kutojua inatoka wapi na inaelekea wapi. Kwa kumbukumbu zangu, miaka michache iliyopita, chini ya raisi huyuhuyu, na Wizara hiyohiyo, waziri wa wizara hiyo Mohd Seif Hatib, kama sikosei, alijitokeza pale uwanja wa JNIA katika kumlaki na kumpokea Richard ambaye aliibuka mshindi wakati wa shindano hilo miaka michache iliyopita. Na katika maneno yake, alisema kuwa ushindi alioupata Richard ni matokea ya sera safi ya michezo na utamaduni inayofanyiwa kazi na kutekelezwa na serikali iliyoko madarakani. Leo serikali ileile, Wizara ileile inatoa tamko lingine kulaani uwepo wa BBA. Kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Haya tunayoyaona leo kutoka kwenye serikali hii ni ya firauni kwa hakika. Yaleyale ya bei za mafuta kushushwa in not more than a week the relevant authority (EWURA) inapandisha bei, sasa hapa mtumiaji na mtanzania wa kawaida amesaidiwaje. Ndiyo haya Mwl Nyerere aliwahi kutahadharisha huko nyumba,serikali ikiwa imekamatwa na wafanyabiasha, basi haiwezi kuamua jambo zuri kwa interest za wananchi. Poor Tanzania,poor leaders