Nchi zinazolipa wananchi kuzaa watoto

Nchi zinazolipa wananchi kuzaa watoto

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Serikali ya China hivi karibuni ilizindua mpango mpya wa kutoa malipo ya kifedha kwa familia zinazojifungua watoto, ikiwa ni jitihada za kupambana na kupungua kwa kasi kwa viwango vya uzazi.

Kupitia mpango huo, familia zitapokea takribani dola 500 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitatu.

Mbali na China kuna baadhi ya nchi zenye sera ya kutoa fedha kwa wanachi ili kuongeza watoto
  1. Australia
  2. Finland
  3. Estonia
  4. Japan
1754032775423.png

1754032799162.png

1754032869290.png

1754032895087.png

1754032931248.png
 
Tatizo hawataki damu za waafrika ili kutoharibu DNA zao
 
Wachina walishagundua kampeni za "uzazi WA mpango" ni mpango WA mabeberu kwadhoofisha kiuchumi na kuwaletea ukoloni mamboleo.

Kiuhalisia, "Watu ni mtaji"
China inakua Kwa Kasi sana Kwa mtaji WA watu walionao (Nguvu Kazi) .
 
Sipàti picha wavietnam wangelikua wachache, Ile "Vietnam war" wamarekani walivokua superior, wangelikua koloni la USA Hadi leo
 
Angalia anachopitia Ukraine Kwa ukosefu WA watu vitani dhidi ya Russia mwenye mamia ya milioni ya watu.

Pia, Trump alipoingiza tu madarakani USA , kapiga marufuku kutoa Mimba, na kasema wazi, uchumi waviwanda unakufa kwasababu ya idadi ndogo ya wafanyakazi.

Kumbuka, Chama Cha democrats Chini ya Biden kiliruhusu wahamiaji ili angalau kufidia pengo la idadi ya watu (Nguvu Kazi) kuendesha uchumi WA marekani.

Angalia Canada inavokaribisha wageni Kwa Nguvu, Hadi inatoa uraia Kwa wakimbizi kwenye Kambi mbalimbali maana uchumi wao unakufa, nchi nzima imejaa mapori.
 
Angalia anachopitia Japan,
nchi imejaa wazee zaid ya 50%,

kiuchumi Japan enzi hizo ndo alikua mbabe na superpower WA bara zima la Asia,

Ila saivi kafulia na kageuka chawa WA USA tangu apigwe nuclear ya Hiroshima & Nagasaki,

Amebaki skeletoni TU la kuchonga, anaishi Kwa huruma ya UN Kwa kulipwa pensheni ya madhara vita aliyofanyiwa na USA tangu mwaka 47 huko.

Kiufupi saiv japani ni kama Lucas au babalevel WA Asia, Ni mpaka amsifie beberu wake USA ndio mkono wake uende kinywani.
 
Tatizo hawa jamaa hawataki "damu nyeusi", ingekuwa hivyo nadhani hii ni opportunity kwa mtu mweusi.
 
Wachina walishagundua kampeni za "uzazi WA mpango" ni mpango WA mabeberu kwadhoofisha kiuchumi na kuwaletea ukoloni mamboleo.

Kiuhalisia, "Watu ni mtaji"
China inakua Kwa Kasi sana Kwa mtaji WA watu walionao (Nguvu Kazi) .
Niliandika hapa kipindi cha nyuma kuwa ili taifa lolote liendelee linahitaji population ya watu wake kuwa wengi. Watu wakanishambulia na kusema sijui ninachosema.

Japani hao wanalipa watu kuzaliana.
 
Angalia anachopitia Ukraine Kwa ukosefu WA watu vitani dhidi ya Russia mwenye mamia ya milioni ya watu.

Pia, Trump alipoingiza tu madarakani USA , kapiga marufuku kutoa Mimba, na kasema wazi, uchumi waviwanda unakufa kwasababu ya idadi ndogo ya wafanyakazi.

Kumbuka, Chama Cha democrats Chini ya Biden kiliruhusu wahamiaji ili angalau kufidia pengo la idadi ya watu (Nguvu Kazi) kuendesha uchumi WA marekani.

Angalia Canada inavokaribisha wageni Kwa Nguvu, Hadi inatoa uraia Kwa wakimbizi kwenye Kambi mbalimbali maana uchumi wao unakufa, nchi nzima imejaa mapori.
Ata huku kwetu tunaelekea huko huko. Hii dunia ya kujiongezea mashepu halafu hawazai ni tatizo.
 
Ongeza na china

Population la china inadidimia Kila siku
 
Hao China si Kuna kipindi walipiga ban kuzaa watoto zaidi ya wawili kimewakita Nini Tena?
 
Warusi walikua mbali ya muda,
Huo ujinga WA uzazi WA mpango walishaukataa tangu enzi za Soviet union,

Tangu Utawala wa Stalin Hadi Leo hii, urusi ukiwa na watoto kuanzia Watano unalipwa mshahara wa serikali WA kima Cha chini Cha mshahara, Wewe pamoja na mkeo.

Wewe na mkeo mkifikisha watoto 10, wote mnakua mnalipwa mshahara ya watumishi 4 WA kima Cha chini.

Mfano:
Saivi Bongo kima Cha chini ni laki 5 cash, hivyo Wewe na mkeo mnakua mnaingiza milioni 1 Kila mwezi Kama mshahara Kwa uzao WA watoto 5+

Ila mkiwa na watoto 10+,
mtaingiza mil 2 kwenye familia Kila mwezi.

Haijalishi una ajira nyingine au ni jobless
 
Back
Top Bottom