Nchi zilizotawaliwa na Ufaransa zimejitambua, bado sisi

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,152
10,866
Nchi zjilizowahi kutawaliwa na Ufaransa miaka ya nyuma zile za magharibi na kaskazini ya Afrika kwa sasa zimetia akili na kukataa kufanywa kama watoto wa dola hilo korofi.

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita taifa hilo limesababisha hasara kubwa ya maisha na uharibifu wa mali wa mataifa hayo.Imetumia mbinu ya kuwafitinisha kwa visingizio kama ugaidi na kuwafanya watu wao wasiwe kitu kimoja huku wenyewe wakikomba mali za mataifa hayo.

Jambo la kufurahisha katika miaka hii michache isiyozidi mitatu mataifa hayo yamekuwa yakitunishiana misuli na wafaransa na kujibishana nao kwa mtindo wa kisa mkasa.

Mali mara kadhaa imekataa kutii amri za taifa hilo na kutaka waondoe majeshi yao. Burkina Faso nao wameitaka nchi hiyo iondoe askari wake nchini humo haraka na bila masharti.

Wananchi nao wameiunga mkono serikali yao kwa kuandamana na kutaka hata ubalozi wa nchi hiyo nao ufungwe mara moja.

64478941_1006.jpg
 
Back
Top Bottom