Tingatinga na dictator ni mbinguni na ardhi! Tumia akili!Wananchi wa mataifa yafuatayo wamewahi kuwa na bahati mbaya kujikuta wakitawaliwa na marais Matingatinga - yaani wapenda sifa,wasiopenda kukosolewa na wakiukaji wakubwa wa katiba za nchi zao.Hupenda kudhibiti bunge,mahakama na huminya uhuru wa raia kupata na kupashana habari
1. UGANDA - Idi Amini Dada( 1971-1979)
2. NIGERIA - Sani Abacha(1993-1998)
3. JAMHURI YA AFRIKA YA KATI - Jean-Bedel Bokassa(1966-1979)
4. GUINEA YA IKWETA - Francisco Macias Nguema(1968-1979)
Kusudi la kuanzisha uzi huu ni hofu tu kuwa isitokee siku moja Tanzania tukatawaliwa na Rais Tingatinga wa level ya kina Bokassa,Idi Amini Dada, Abacha na Macias Nguema maana itakuwa ni kilio kikuu na kusaga meno!
kumbuka hata diomond ni Raisi wa wasafiUnataka kutuambia nini?Hebu kuwa na heshima na adabu katika cheo cha Raisi unataka tukuamini iliganisho wako kwa thread hii kisa neno TINGATINGA
wilaya ya Namtumbo ipo wazi, ntakufikiria.Usiumizwe kichwa na Nyumbu ambao wanalilia mgao wa bilioni mbili za fisadi walizopokea marubani wa kubadili gia za anga!
Usiumizwe kichwa na Nyumbu ambao wanalilia mgao wa bilioni mbili za fisadi walizopokea marubani wa kubadili gia za anga!
Na tulimbiwa Waishio kama malaika watashushwa na kuishi kama shetani. Basi tunatawaliwa na shetani.Aliyepita aliambiwa dhaifu huyu wa sasa anaambiwa ni mkali na anaelekea kuwa dikteta. Huyo rais mwenye sifa ya katikati ya Kikwete na Magufuli, labda ni malaika, sidhani kama yupo binadamu wa aina hiyo.
Rais anayefuata sheria kanuni na taratibu za nchi kwa ukamilifu wake...huwa nawaza sana ila sipati jibu,watanzania mkoje? hivi mnataka rais wa type gani sasa?.kama vile hatujitambui.
Wananchi wa mataifa yafuatayo wamewahi kuwa na bahati mbaya kujikuta wakitawaliwa na marais Matingatinga - yaani wapenda sifa,wasiopenda kukosolewa na wakiukaji wakubwa wa katiba za nchi zao.Hupenda kudhibiti bunge,mahakama na huminya uhuru wa raia kupata na kupashana habari
1. UGANDA - Idi Amini Dada( 1971-1979)
2. NIGERIA - Sani Abacha(1993-1998)
3. JAMHURI YA AFRIKA YA KATI - Jean-Bedel Bokassa(1966-1979)
4. GUINEA YA IKWETA - Francisco Macias Nguema(1968-1979)
Kusudi la kuanzisha uzi huu ni hofu tu kuwa isitokee siku moja Tanzania tukatawaliwa na Rais Tingatinga wa level ya kina Bokassa,Idi Amini Dada, Abacha na Macias Nguema maana itakuwa ni kilio kikuu na kusaga meno!
ahahahaWatanzania juzi tu hapa walikuwa wanalalamika JK ni rais dhaifu daah!
Usichukulie maneno ya watanzania serious. Tafiti zinaonesha wengi wana magonjwa ya akili. Wakati wakimnadi mtuhumiwa wa ufisadi walisema ana maamuzi magumu, wakatoa mifano ya mkurugenzi wa Same na mhandisi wa temeke, walisema hapa nchi ilipofika inahitaji dikteta, leo wameanza ooh hatutaki maamuzi magumu, ooh majipu yana haki, ooh mafisadi wasitajwe hadharani......Watanzania juzi tu hapa walikuwa wanalalamika JK ni rais dhaifu daah!
Usiwe too general. Ainisha hucho unachoona kuwa anaoaswa kuachana nachoSijui lengo lako ni nini kwa andiko hili...Ila ushauri wangu kwako ni kuwa uachane na hoja za aina hii, zitakufikisha pabaya...ni ushauri tu.