Nchi zilizopata kutawaliwa na Marais "Matingatinga"

Nchi zilizopata kutawaliwa na Marais "Matingatinga"

Wananchi wa mataifa yafuatayo wamewahi kuwa na bahati mbaya kujikuta wakitawaliwa na marais Matingatinga - yaani wapenda sifa,wasiopenda kukosolewa na wakiukaji wakubwa wa katiba za nchi zao.Hupenda kudhibiti bunge,mahakama na huminya uhuru wa raia kupata na kupashana habari

1. UGANDA - Idi Amini Dada( 1971-1979)
2. NIGERIA - Sani Abacha(1993-1998)
3. JAMHURI YA AFRIKA YA KATI - Jean-Bedel Bokassa(1966-1979)

4. GUINEA YA IKWETA - Francisco Macias Nguema(1968-1979)

Kusudi la kuanzisha uzi huu ni hofu tu kuwa isitokee siku moja Tanzania tukatawaliwa na Rais Tingatinga wa level ya kina Bokassa,Idi Amini Dada, Abacha na Macias Nguema maana itakuwa ni kilio kikuu na kusaga meno!

endelea kuomba isitokee, nyumbu ww.
 
Umemsahau Mao na Stalin
 
Matingatinga mengine ni Adolf Hitler (Ujerumani), Benito Mussolin (Italia), Mobuto Seseseko (Congo DR/Zaire), Paul Kagame (Rwanda) na Pierre Nkuruzinza (Burundi)....Hawa hata mabunge yao hawataki yaoneshwe live.
 
Iddi Amini alikuwa na kasi sana alifanya makubwa katika kipindi kifupi
hata Stalin na Hitler waliendeleza nchi zao kwa speed ya ajabu
lakini end results wote tunaijua......
tusubiri ya kwetu sasa
 
Kushindwa kubaya
Kukosa sera ni dalili za kufa kisiasa
Mkuu acha uongo, nani kakuambia hawana sera? Uliambiwa sera zipo kwenye ilani ya uchaguzi na ulitakiwa ukazisome kwenye mtandao!! Sasa kama huna mtandao shauri yako!! Mimi binafsi sikuzisikia na sikutaka kwenda mtandaoni kwa kuwa sikuwa na MB!!
 
Iddi Amini alikuwa na kasi sana alifanya makubwa katika kipindi kifupi
hata Stalin na Hitler waliendeleza nchi zao kwa speed ya ajabu
lakini end results wote tunaijua......
tusubiri ya kwetu sasa
Mkuu The Boss tumetoka mbali hapa JF ila unakoelekea unaweza kutuachia simanzi. Tuwe na kiasi
 
Mkuu maendeleo gani hamna hata dalili ya viwanda kilimo chenyewe cha jembe la mkono. Sasa haya majipu si mtahamaki 2020 imefika. LUGUMI vipi anarudisha hela au ndo imetoka hiyo
 
Naamini Rais Magufuli ni mzuri hata kama siyo perfect. Mimi ninachomshauri ni kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kulinda misingi ya demokrasia ili wananchi wote wenye dhamira njema wawe nyuma yake. Huwezi kupata maendeleo hata kama ungekuwa na akili kiasi gani kama utawagawa watu wako. Nafahamu Rais analijua sana hilo, ndiyo maana kila mara amesema kuwa Watanzania wote tushirikiane.

Tatizo la Rais Magufuli, akiona rangi nyingi za kijani zimemzunguka, na yeye anavutika kwenye siasa za kivyama badala ya kusimama kitaifa, na kukemea siasa za kivyama kwenye mambo ya Kitaifa. Kuna wakati amepotoka kwa kuingia kwenye lugha za vijembe dhidi ya UKAWA. Siasa za maneno ya kimbea kama yale ya kwenye kanga, na mengine yale ya taarabu ambayo yanapendwa na baadhi ya watu hata humu JF, waachiwe wale wasiojitambua, Rais asimame kama alama ya Taifa.
 
Hebu tuambie unataka kutuaminisha nini asa
 
Kwa manazi wa CCM awamu zote sawa tu. Ya JK ilikuwa njema; ya Magufuli nayo njema. Hakuna anayejiuliza inakuwaje Magufuli kila wakati analalamika jinsi wananchi wanyonge walivyoteswa na mafisadi; walivyoibiwa hadharani na yeye amekuja kuwakomboa! Toka serikali ipi, ya chama kipi? Bila shaka CCM itatawala milele. Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya. People get the government they deserve.
 
Back
Top Bottom