The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Viongozi wa Ulaya wamezindua Alhamisi mjini Rome, mkutano wa kila mwaka wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ukraine baada ya vita, wakitarajia kukusanya dola bilioni 12.
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky waliufungua mkutano huo kwa kuwatolewa wito wamiliki wa makampuni na watu binafsi kuwekeza katika miradi itakayosaidia mpango huo.
Mkutano huo umefanyika wakati Urusi ikizidisha mashambulizi nchini Ukraine kwa usiku wa pili mfululizo huku Umoja wa Mataifa ukitahadharisha kuwa idadi ya wahanga wa mashambulizi hayo imefikia kiwango cha juu zaidi.
Hayo yakiarifiwa, rais wa Marekani Donald Trump amesema bila kutoa maelezo zaidi kwamba siku ya Jumatatu atatoa "taarifa muhimu" kuhusu Urusi.