Nchi za magharibi zimefurahi Dr Slaa kushindwa

Hayo ni mawazo yako; mali inayoibwa Tanzania na makampuni ya Kanada haimsaidii mlipa kodi wa Kanada ambaye ndiye anayetoa dola zake kuisadia Tanzania katika umaskini wetu. Waziri mkuu wa Kanada aliwahi kutamka kuwa Makampuni ya nchi yake yanavuna sana nchini kwetu kutokana na ujinga wetu na wala yeye binafsi na serikali yake hawafurahishwi na hali hiyo, kwa vile inabidi tena wamege fundu kujza bakuli letu kiasi ambacho tungejipatia wenyewe kutokana na raslimali zetu.

Kwa taarifa yako nchi za Magharibi zinataka Afrika iamke haraka sana iondokane na umaskini kusudi isiendelee kutumiwa na CHINA.

Nafikiri muanzisha thread anaposema nchi za magharibi anamaanisha serikali zao - jambo ambalo linayumkinika kabisa. Kama uliweza kumuona Tony Blair akiwa PM wa UK alivyotetea ununuzi wa rada ya Tanzania toka BAE systems akihakikisha kuwa ulikuwa mpango safi kabisa: "above board" kwa maneno yake, unaweza kuelewa jinsi maslahi ya kiuchumi yanavyopewa kipaumbele kwenye nchi hizo. Ni kweli kwamba wananchi wengi wa nchi hizo wanajali haki zetu kuliko hata viongozi wetu wenyewe. Aidha, kazi iliyofanywa na SFO kumthibitisha uongo Tony Blair i wazi kuonyesha baadhi ya watu makini walio tayari kupinga mitizamo ya viongozi wa serikali zao wasiosimamia maadili.
 
Kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

Nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini JK alialikwa white house baada tu ya Obama kuapishwa. Kwa nini G Bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini Iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia Mugabe na rais wa Venezuela?

Kwa nini Rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema Hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa Slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua Slaa ni tishio?

Nakubaliana nawe. Hivi mligundua kuwa nembo ya Chadema kwenye fomu ya kupiga kura ilikuwa imefubaa na kwa nini iwe hivyo?
 
Kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

Nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini JK alialikwa white house baada tu ya Obama kuapishwa. Kwa nini G Bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini Iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia Mugabe na rais wa Venezuela?

Kwa nini Rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema Hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa Slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua Slaa ni tishio?

Hey usituposhe hapa. Nchi za magharibi hazipendi hizi nchi zinazotawaliwa kimabavu. CHADEMA wanapinga tawala kama za kiimka kama za Mugabe, Rwanda na Venezuela. Kamwe katiba za vyama vinavotawala kwenye nchi hizo hazifani hata chembe na katiba ya CHADEMA.
Katiba ya CHADEMA ni katiba ya watu yaani madaraka kwa watu wakati katiba za nchi ni za kikandamizaji kama ya CCM.

Tatizo letu waafrika tukishindwa tunae wa kumlaunu huyo anaitwa mzungu wakati tumeboronga sisi. Katiba ya CHADEMA ni kama katiba ya sasa ya KENYA ambayo ni nzuri na imeshinikizwa na hizo nchi za magharibi.
Obama kumwalika JK ni kuwa huko nje Tanzania inaonekana ni kioungo muhimu kwa amani ya maziwa makuu na amani iliyonayo wakati ndani imejaa mifupa kama kaburi.
 
Una maana makampuni ya Canada hayalipi kodi, review your comments please!
Jifunze sheria za kodi ili ujue kwa nini makampuni yanafungua offshore offices: Barick Tanzania hailipi kodi huko Canada, kwa hiyo kama hawalipi kwetu basi wanaula kweli kweli.
 
Kwa taarifa yako nchi za Magharibi zinataka Afrika iamke haraka sana iondokane na umaskini kusudi isiendelee kutumiwa na CHINA.

Hii dhana kuwa nchi za magharibi zanapenda Africa iendelee unaitoa wapi? Unadhani vijimisada vinavyoletwa Tz vinalenga Tz kuendelea? Pipi hizo ndugu yangu. Serikali ya Canada siyo kwamba hainufaiki na makampuni yanayoiba rasilimali zetu, hii serikali ya Canada inapata wapi hizo hela za kutuletea sisi? Hizi kampuni zinalipa kodi mkuu. Maneno ya kiongozi wa Canada ni kama taarabu za viongozi wa Tz. Hakuna kiongozi wa nchi za magharibi anayependa sisi tuendelee. Kwa taarifa yako sasa wafadhili wanakuja na mkakati wa kuzitaka nchi za Africa kutoa tenda za manunuzi ya serikali kwa kampuni za kigeni tu. Kumbuka, makampuni makubwa ya biashara yanamilikiwa na haohao viongozi unaowataja kuwa wanataka Africa iendelee. Bush Iraq, kwa nini?
Tafakari.

Hayo ni mawazo yako; mali inayoibwa Tanzania na makampuni ya Kanada haimsaidii mlipa kodi wa Kanada ambaye ndiye anayetoa dola zake kuisadia Tanzania katika umaskini wetu. Waziri mkuu wa Kanada aliwahi kutamka kuwa Makampuni ya nchi yake yanavuna sana nchini kwetu kutokana na ujinga wetu na wala yeye binafsi na serikali yake hawafurahishwi na hali hiyo, kwa vile inabidi tena wamege fundu kujza bakuli letu kiasi ambacho tungejipatia wenyewe kutokana na raslimali zetu.

Kwa taarifa yako nchi za Magharibi zinataka Afrika iamke haraka sana iondokane na umaskini kusudi isiendelee kutumiwa na CHINA.

sikubaliani nawe...nadhani hata raia wa kawaida huko ulaya hawana nguvu kubwa linapokuja suala linalojumuisha corporate interests...fikiria vita ya congo nilisoma kipindi article fulani ya profesa baregu kuhusu corporate interests na zinavochochea instability katika ukanda huo ni mambo ya kushangaza...so linapokuja suala la corporate interests anything is possible
 
Umekosea.. Canada wananufaika.. Coorporate taxes zinalipwa Canada 40% kazi za management na consultant kwa Ajili ya migodi zilipewa kampuni ya Canada. Bariki shareholders wengi ni wacanada wanaspend hela nchini Canada hivyo hukuza uchumi wa nchi Yao.
Kisheria Canada hairuhusu kampuni kuchimaba maliasili zao Kama Hiyo kampuni halimikiwi 30% na wacanada, na top management lazima ease wawe wacanada! Jiulize ni kwanini watumishi wa ubalozi wa Canada walikuwepo Dodoma wakati wabunge wanajadili mikataba ya madini
 
Hayo ya kuwepo bungeni wawakilishi wa Canada na the amount of corparate taxes za Canada siyajui (na wala siyabishii), hila spot on kwenye Canada kuwa wakali kwenye maliasili zao na jinsi ya kumiliki hizo rasilimali ni moja ya nchi zinazojulikana kwa kuwa na tough protectionism laws when it comes to their natural resources.

Pili the point of share holders ndio kubwa sana kwa nini hizi western government zinatoa misaada kwanza ukitoa the americas, nchi nyingi produce very little in terms of food produce or having enough natural resources to maintain their economies hivyo the're always on the lookout for the means to support their economies and life styles. The easier the access the better, na last thing they would want once their intrest is succesful are any radical changes in terms of contracts (ask mugabe what happened when he tried to fight their policies), or politacal uncertainies where there is an interest.

Hivi vitu vina huge impact on their markets kama ulivyosema kuna shareholders katika haya makampuni ambao wameweka hela zao na baadhi wana-rely na hivi vipato, kuna corparate taxes from companies to the governments, kuna capital gain taxes ambazo investors wanalipa kwa serikali, kuna bidhaa ambazo watu wao wananunua ambazo zimewekea ushuru faida tena kwa serikali. Yaani nchi kama uingereza aina chochote cha maana ndio maana huwa wanakuwa wakali sana kwenye losses kama adhabu waliompa Mugabe au wanavyoikomalia Kenya kuwe na stability hili ku-protect their interest lakini si kusema eti wanajali amani au kutaka kuona democracy kwa faida ya muafrica.

Bado ujazungumzia hizi kampuni nyingi especially za uwekezaji its almost impossible for a western company to operate without debts, kwa hivyo tena kuna mikopo ya benki ambazo ni hela za watu wameweka na huko pia kuna shareholders mchezo ule ule unajirudia, tumeona athari ya kuanguka kwa uchumi kutokana na mikopo ya hovyo kutoka kwa mabenki si muda mrefu hivyo ni muhimu hizi kampuni kuwa na mafanikio nje ya nchi yaani zina contribution kubwa sana ndani ya nchi yzo (na kama benki ziki fail ndio unaona sasa wanakuja na necessary bailouts) kwa hivyo the best solution is to take measures to avoid failures hapo ndipo serikali zao zinapoingia indirectly to protect their economics.

Kitu kingine example kesho kukiwa na mfarakano wa muda mrefu nchi kama Ghana uchukuaji na ununuaji wa Cocoa ukaathirika. Yaani gharama ya chocolate and any other product that comes out of Cocoa is bound to increase and small businessness that rely on that particular product ni kwishnei na huko pia watapoteza ajira. Upuuzi wa muafrica kwa leo unawawezesha kuwa na maisha raisi na kukuza uchumi wao kwa kiasi kikubwa ndio maana watu kama kina Chavez wanaona 'hell no' to cheap contracts and to hell with Mzungu.

Hivyo tusione eti wao (serikali zao) wapo mbali na uwekezaji tukazani hawana interest vinginevyo wala wasingeangaika na kutoa misaada na wala wasingekuwa wana push for us to follow their policies na kutu punish kama atusikii watakavyo. Kama umeona msaada safari umepungua kutokana na kwamba wanadai kumekuwa na rushwa mno na utapeli ambao inabidi uthibitiwe kwanza. kwa lugha yetu mimi na wewe wanachomaanisha jamaa akina 'Jack Pemba' na watoto wengine wa mjini (mfano tu nimetoa hilo jina kati ya wengi waliopo) wamesha watia mjini sana wazungu wanaotaka kuwekeza Tanzania na hili kuweza kusaidia small business huko kwao kwa namna moja au nyingine.

Serikali ya mzungu itakachofanya hawataweka hayo mbele yetu, hila kama ni tatizo na mzungu kesha lalama kwa mbunge wake na limejadiliwa ndani ya bunge pengine na wabunge hatawasoizidi ishirini siku hiyo, serikali wala hawatalisema kwenye media wata act based on information kutoka kwa ground intelligence na concerns za wawekezaji kama zimezidi utashangaa wanasema tuna punguza msaada kwa kuwa hili alitekelezwi ndio ujue sio wazungu wote africa watalii au wote wanaokuja kufanya reseach ni kwa kutusaidia. Yaani mzungu sio mjinga kabisaa anyway atakuawaje mjinga mtu mwenye maendeo hatacho kifanya hata tupa bomba moja lenye psychogical conditioning through their policies au aid mwenyewe utakoma watu au watakugeuka Muulize Mugabe.Ni sisi waafrika ndio tunaamini mtu anaweza kuwa mjanja bila ya elimu huwa nacheka sana nikiwatazama watanzania hapa nilipo, we are poor for many reasons na decision making being at the fore front.
 
There we go again!, yea we can blame "the wazunguz"

1. Kwa hiyo ni wazungu wanaofanya mpaka leo Tanzania watu wenye access ya maji safi na salama kuwa chini ya 20%, 50 yrs down the line?

2. Ni wazungu waliotujengea shule hovyo hovyo (shule za kata) na kusababisha kukosa walimu, vitendea kazi, maktaba na maabara?

3. Ni wazungu hao hao waliotuletea Richmond?

4. Ina maana ni wazungu ndiyo walisuka michongo ya EPA?

5. Ni wazungu ndiyo wamefanya tufike mahali tunaimpoti kila kitu kuanzia sabuni, dawa za meno, midoli etc.?

6. Ni wazungu ndi waliochafua jiji la Dar es Salaam halafu wakagoma kulisafisha?

7. Wazungu hao hao wametufanya tusiwe hata na mji mmoja wa mfano katika suala zima la mipango miji?

8. Ni wazungu ndiyo waliosababisha yale madimbwi na vijinjia visivyoeleweka nje ya mahekalu ya kutisha kule Mbezi beach, Tegeta na Kunduchi?

9. Nna hamu nikutane na hao wazungu wanaotusababishia ajali mbaya za barabarani zisizokwisha.

10. Ni wazungu ndiyo walisababisha mpaka leo hatuna umeme wa uhakika?
 
Kichuguu, naheshimu mawazo yako ingawa naamini unahitaji kujielimisha zaidi kuhusu Aid configuration na neo colonialism. You need sound analytical powers. Je una taarifa kwamba balozi wa Canada Hapa nchini alikuwa anafanya active lobying kwa wabunge wetu wakati wa kujadili ripoti ya haji bomani na wakati wa mapitio ya Sheria ya madini? Unaelewa kwamba ni balozi wa Norway Hapa tz ndiye alikuwa achitect wa muafaka wa Zanzibar kwa sababu ya maslahi ya makampuni ya mafuta ya Norway Hapa tz?

Another old lie! old lie! same lies! NEO-COLONIALISM!

Kama alivyosema kichuguu, waafrika wenyewe ndio wenye matatizo, hata wewe ungekuwa mzungu ungefanya wanachofanya, never mentio that vocabulary, ambayo hata viongozi wanaitumia!!! neo-colonialism! Mkwawa na Mirambo waliwapiga hawa wakoloni na hawakusoma wala hawakujua kitu kinaitwa ukoloni, THEY SIMPLY PROTECTED THEIR RESOURCES! sasa wewe karamagi kwenda kusign mikataba ulaya unasema neo-cololialism! kama sio matusi ni nini, ukisema hilo NENO ni sawa na unasema we are not human, we can not think, we are just puppets!!!!!

ubinafsi , uroho ndio unatumaliza, NEO-COLOLIALISM is not existing for intelectuals !!!

Yaani mtu aingie kwangu achukue kabati langu na vyombo anipe kioo NISEME NEO-COLINIALISM

usiseme tena hili neno kama umesoma darasani lifute!!
 
Umaskini wetu ni uzembe wa muafrika, ambao mzungu anau utumia kwa advantage yake. Yeye nia yake na maslahi yake africa ni kuchota hayo ya maendeleo ni sisi wenyewe na kujilinda kutoka kwa mzungu kama kipato tunapoteza kwake uoni ni indirectly yupo involved.

Therefore umaskini ni sisi kwanza ndio maana mada ina sema wazungu kwa upande fulani watakuwa wamefurahia kushindwa kwa Chadema(though no direct evidence i must say). Kwa mtaji huo taka nyingi zitabakii na little will change to the current system ambayo ina wafaa wao zaidi kuliko sisi. Sasa hilo sio tatizo la mzungu wanachotaka kwenye huu upuuzi wetu leo ni kutuibia tu no more, mengine tuta ji JJ wenyewe. Ni mpaka hapo tutakapo hamka ndio vinginevyo.
 
There we go again!, yea we can blame "the wazunguz"

1. Kwa hiyo ni wazungu wanaofanya mpaka leo Tanzania watu wenye access ya maji safi na salama kuwa chini ya 20%, 50 yrs down the line?

2. Ni wazungu waliotujengea shule hovyo hovyo (shule za kata) na kusababisha kukosa walimu, vitendea kazi, maktaba na maabara?

3. Ni wazungu hao hao waliotuletea Richmond?

4. Ina maana ni wazungu ndiyo walisuka michongo ya EPA?

5. Ni wazungu ndiyo wamefanya tufike mahali tunaimpoti kila kitu kuanzia sabuni, dawa za meno, midoli etc.?

6. Ni wazungu ndi waliochafua jiji la Dar es Salaam halafu wakagoma kulisafisha?

7. Wazungu hao hao wametufanya tusiwe hata na mji mmoja wa mfano katika suala zima la mipango miji?

8. Ni wazungu ndiyo waliosababisha yale madimbwi na vijinjia visivyoeleweka nje ya mahekalu ya kutisha kule Mbezi beach, Tegeta na Kunduchi?

9. Nna hamu nikutane na hao wazungu wanaotusababishia ajali mbaya za barabarani zisizokwisha.

10. Ni wazungu ndiyo walisababisha mpaka leo hatuna umeme wa uhakika?

big-tick.jpg
 
Nakubaliana na wewe mkuu,most of this countries they still want to capitalies all resources coming from emerging nation,
Ndo maana Makapuni kama Tullow OIl(Ireland) imeweka base hapo Uganda baada ya kugundua mafuta yote hii ni kunyonya tu,Obama(us) na David Cameroon(uk) wote wako Asia.Obama yuko India,Indonesia na nchi nyingine hapo hapo pia Cameroon yuko China yote hiyo ni madili ya kuwaibia watu!
Juzi juzi walikua wana ishtumu China kwa haki za kibinadamu lakini linvyokuja swala la masilahi ya UK hamna haki za kibinadamu wanvyo ongealea cha kwanza Rolls Royces wamekula mkataba wa maana na China hayo mengine badae.
So mtu anayesema kwamba nchi za magharibi wanaitakia mema Africa ni mwongo hao hawana urafiki usiokua na faida!
 
Nafikiri muanzisha thread anaposema nchi za magharibi anamaanisha serikali zao - jambo ambalo linayumkinika kabisa. Kama uliweza kumuona Tony Blair akiwa PM wa UK alivyotetea ununuzi wa rada ya Tanzania toka BAE systems akihakikisha kuwa ulikuwa mpango safi kabisa: "above board" kwa maneno yake, unaweza kuelewa jinsi maslahi ya kiuchumi yanavyopewa kipaumbele kwenye nchi hizo. Ni kweli kwamba wananchi wengi wa nchi hizo wanajali haki zetu kuliko hata viongozi wetu wenyewe. Aidha, kazi iliyofanywa na SFO kumthibitisha uongo Tony Blair i wazi kuonyesha baadhi ya watu makini walio tayari kupinga mitizamo ya viongozi wa serikali zao wasiosimamia maadili.

Asenti.
 
There we go again!, yea we can blame "the wazunguz"

1. Kwa hiyo ni wazungu wanaofanya mpaka leo Tanzania watu wenye access ya maji safi na salama kuwa chini ya 20%, 50 yrs down the line?

2. Ni wazungu waliotujengea shule hovyo hovyo (shule za kata) na kusababisha kukosa walimu, vitendea kazi, maktaba na maabara?

3. Ni wazungu hao hao waliotuletea Richmond?

4. Ina maana ni wazungu ndiyo walisuka michongo ya EPA?

5. Ni wazungu ndiyo wamefanya tufike mahali tunaimpoti kila kitu kuanzia sabuni, dawa za meno, midoli etc.?

6. Ni wazungu ndi waliochafua jiji la Dar es Salaam halafu wakagoma kulisafisha?

7. Wazungu hao hao wametufanya tusiwe hata na mji mmoja wa mfano katika suala zima la mipango miji?

8. Ni wazungu ndiyo waliosababisha yale madimbwi na vijinjia visivyoeleweka nje ya mahekalu ya kutisha kule Mbezi beach, Tegeta na Kunduchi?

9. Nna hamu nikutane na hao wazungu wanaotusababishia ajali mbaya za barabarani zisizokwisha.

10. Ni wazungu ndiyo walisababisha mpaka leo hatuna umeme wa uhakika?

Ndugu Nyambala,

Huwezi ukamuondoa mzungu kwene madhila yanamkuta mwafrika..aghalalabu popote ambapo mwafrika anataabika kuna mkono wa mzungu. Huo ndio ukweli. Pamoja na kwamba tuna viongozi wabovu, weney uoni finyu na fikra zao kuzibwa na ulafi, bado control mechanism ya 'mzunguz' ina-play part kubwa sana.

Siasa is a multi-billion dollar business popote pale duniani, na mara nyingi wachezaji wakubwa ni hawa lobbysts, watu wenye mamiradi na mainvestment ya kufa mtu, hawa ndio wanaoshika kamba za kuwachezesha wanasiasa. Wanatumia mitandao yao ya kibiashara ku-control media na ku-influence polls.

Kwa mechanism za namna hii, halafu kwa huku kwetu Afrika unakutana na viongozi wa dizaini ya 'Dr.Mkwere' lazima ile kwetu.
 
Umaskini wetu ni uzembe wa muafrika, ambao mzungu anau utumia kwa advantage yake. Yeye nia yake na maslahi yake africa ni kuchota hayo ya maendeleo ni sisi wenyewe na kujilinda kutoka kwa mzungu kama kipato tunapoteza kwake uoni ni indirectly yupo involved.

Therefore umaskini ni sisi kwanza ndio maana mada ina sema wazungu kwa upande fulani watakuwa wamefurahia kushindwa kwa Chadema(though no direct evidence i must say). Kwa mtaji huo taka nyingi zitabakii na little will change to the current system ambayo ina wafaa wao zaidi kuliko sisi. Sasa hilo sio tatizo la mzungu wanachotaka kwenye huu upuuzi wetu leo ni kutuibia tu no more, mengine tuta ji JJ wenyewe. Ni mpaka hapo tutakapo hamka ndio vinginevyo.

Braza Juma usiwe unapotea sana mkuu.

Anyways, nakubaliana na wewe kwamba mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe na hawa wazungu wanatumilia huu udhaifu wetu ku-control mustakabali na hatima yetu. Dunia ya sasa inahitaji tuwe na viongozi wanaojua uelekeo wa sayari..we lack that kind of leadership, na ndio maana tunaona massive mismanagement na kudorora kwa uchumi.
 
Nakubaliana na wewe mkuu,most of this countries they still want to capitalies all resources coming from emerging nation,
Ndo maana Makapuni kama Tullow OIl(Ireland) imeweka base hapo Uganda baada ya kugundua mafuta yote hii ni kunyonya tu,Obama(us) na David Cameroon(uk) wote wako Asia.Obama yuko India,Indonesia na nchi nyingine hapo hapo pia Cameroon yuko China yote hiyo ni madili ya kuwaibia watu!
Juzi juzi walikua wana ishtumu China kwa haki za kibinadamu lakini linvyokuja swala la masilahi ya UK hamna haki za kibinadamu wanvyo ongealea cha kwanza Rolls Royces wamekula mkataba wa maana na China hayo mengine badae.
So mtu anayesema kwamba nchi za magharibi wanaitakia mema Africa ni mwongo hao hawana urafiki usiokua na faida!

- Well, saafi sana mkuu interest za West popote pale Duniani, huongozwa na USA ambao siku zote wanaamini kwamba interest zao hasa Africa zinaweza kulindwa na incumbent tu, ukiona wanashangilia Rais mpya ujue ametokea World Bank au IMF, kama sio UN. Kwa mfano hawakuwa na uhakika sana na Raila Odinga waliamini anaweza kuleta siasa za nationalization kama Hugo Chavez,

- kule Ivory Coast ni mtu wao kutoka World Bank, sasa hivi interest yao kubwa Africa ni kuchukua nchi zote za Francophone kwanza mengine sio muhimu sana kwa sasa.

William.
 
Ndugu Nyambala,

Huwezi ukamuondoa mzungu kwene madhila yanamkuta mwafrika..aghalalabu popote ambapo mwafrika anataabika kuna mkono wa mzungu. Huo ndio ukweli. Pamoja na kwamba tuna viongozi wabovu, weney uoni finyu na fikra zao kuzibwa na ulafi, bado control mechanism ya 'mzunguz' ina-play part kubwa sana.

Siasa is a multi-billion dollar business popote pale duniani, na mara nyingi wachezaji wakubwa ni hawa lobbysts, watu wenye mamiradi na mainvestment ya kufa mtu, hawa ndio wanaoshika kamba za kuwachezesha wanasiasa. Wanatumia mitandao yao ya kibiashara ku-control media na ku-influence polls.

Kwa mechanism za namna hii, halafu kwa huku kwetu Afrika unakutana na viongozi wa dizaini ya 'Dr.Mkwere' lazima ile kwetu.

Mkuu Abdulahim naweza nikakubali au nikakubali kutokukubaliana na maoni yako. Kimsingi I am not in favor pale ishu ya "wazungu" inapotumika kama slogan for our failures. "Wazungu," "Mabepari", "Mabeberu" imekuwa ni kisingizio kikubwa hasa kutoka kwa viongozi wa kiafrica as to why hatuendelei. Huwa nashindwa kuelewa inakuwaje wazungu hao hao they don't do the same in China, Malaysia, Singapore or else Botswana?

Wakati nchi ndogo na changa na zenye weusi kama sisi (Mfano PNG, Botswana, Namibia) zinaweza kumanage raslimali zao inakuwaje sisi tushindwe halafu tusingizie wazungu.

I agree with you on the fact that when push comes to shove, siasa siku zote itakuwa juu ya Economics. Na unapokuwa na haya makampuni ya kibepari amabayo mengi yao hayako straight namna yanavyoendeshwa plus the recipe ya viongozi kama Mkwere nio hatari juu ya hatari.

Kuhusu suala zima la lobbying hii imeanzia huko huko nchi zilizoendelea and still exists. Lakini I do not think the intensity and investment in that is as equal kwa nchi kama Tanzania. Na crrent lobbying iko tofauti kabisa ukilinganisha na wakati ule wa vita baridi. Msingi mkuwa wa Mijikampuni ya kibepari ni "Faida" na ili upate faida ni lazima uyassess vizuri mazingira unayoenda kuwekeza.

Lakini je ni kweli Sweden, US, Russia, UK, France na wazungu wengine ndiyo wamefanya sisi tuendelee kuwa maskini? Vikao hivi wanafanyia wapi na mara ngapi kwa mwaka?. Did they frog-jumped us kusaini mikataba ya kipuuzi juu ya madini yetu? Wana interest gani wanapotuona tunakufa kwa kipindupindu kwa kukosa maji safi na salama??

Bado natatizwa kuhusu uhusika wa wazungu katika kuvandalize communication system karibuyote upande wa Tanzania kwenye reli ya TAZARA. Vilevile kuhusika kwao as to why 61% ya budget ya serikali inatumika kuendeshea serikali hiyo.

All in all mkuu, kwa mtazamo wangu hii ngoma ni yetu na tunapaswa kuicheza regardles wazungu wanapenda au hawapendi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom