Nchi za magharibi zimefurahi Dr Slaa kushindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi za magharibi zimefurahi Dr Slaa kushindwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Nov 9, 2010.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

  Nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

  Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

  jiulize kwa nini JK alialikwa white house baada tu ya Obama kuapishwa. Kwa nini G Bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini Iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia Mugabe na rais wa Venezuela?

  Kwa nini Rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

  Niliwahi kusema Hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa Slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua Slaa ni tishio?
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bado inawezekana kwa hoja Bungeni.
   
 3. Shomoro

  Shomoro Senior Member

  #3
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yap! Wazungu ni wez! wametuletea shanga......(singing!)
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hayo ni mawazo yako; mali inayoibwa Tanzania na makampuni ya Kanada haimsaidii mlipa kodi wa Kanada ambaye ndiye anayetoa dola zake kuisadia Tanzania katika umaskini wetu. Waziri mkuu wa Kanada aliwahi kutamka kuwa Makampuni ya nchi yake yanavuna sana nchini kwetu kutokana na ujinga wetu na wala yeye binafsi na serikali yake hawafurahishwi na hali hiyo, kwa vile inabidi tena wamege fundu kujza bakuli letu kiasi ambacho tungejipatia wenyewe kutokana na raslimali zetu.

  Kwa taarifa yako nchi za Magharibi zinataka Afrika iamke haraka sana iondokane na umaskini kusudi isiendelee kutumiwa na CHINA.
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sikubaliani na wewe mataifa ya nje yanajua kila kitu na wanafanya makusudi kutunyonya! Hakuna anayetuonea huruma zaidi ya kutufilisi tuu na kutumia ujinga wetu kama daraja lao!
   
 6. K

  King kingo JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama sisi wenyewe hatujionei huruma hamna hata mmoja kutoka nje atakaetuonea huruma hilo msahahu kabisa
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Wazungu hawainyonyi Afrika ya leo; ni waafrika wenyewe ndio wanaoiharibu Afrika yao. Wazungu hawa hawakuchukua madini yetu kwa nguvu, bali tuliwapa. Makampuni yote ya madini yaliyoko Afrika siyo makampuni ya serikali za kwao, ni makampuni ya watu binafsi. Serikali zao hazifaidiki lolote na makapuni hayo kupata faida Afrika ukiachia mbali capital gain tax ya raia walio na hisa katika makampuni hayo; makapuni yenyewe hayawezi kulipa kodi kwa mapato yaliyopatikana Afrika kwa vile wanategemewa kuwa wamelipa kodi huko walikopatia faida. Ndiyo maana makampuni mengi ya magharibi yalipohamia China nchi za magharabi zitokwa jasho la damu kimapato, na china ikapanda sana kimapato.
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kichuguu, naheshimu mawazo yako ingawa naamini unahitaji kujielimisha zaidi kuhusu Aid configuration na neo colonialism. You need sound analytical powers. Je una taarifa kwamba balozi wa Canada Hapa nchini alikuwa anafanya active lobying kwa wabunge wetu wakati wa kujadili ripoti ya haji bomani na wakati wa mapitio ya Sheria ya madini? Unaelewa kwamba ni balozi wa Norway Hapa tz ndiye alikuwa achitect wa muafaka wa Zanzibar kwa sababu ya maslahi ya makampuni ya mafuta ya Norway Hapa tz?
   
 9. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Siyo kwa Spika Chenge au Anna Makinda
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  mi naamini itawezekana tu pale wananchi watakapokataa kauli za viongozi wanaowaabudu wafadhili. wananchi wafanye uamuzi wa kurudisha utawala wa rasilimali kwetu wenyewe badala ya kuchagua viongozi wanaopigia magoti wazungu. ili hii iwezekani, ni lazima wananchi wawakatae mafisadi kwani ndio makuwadi wa wazungu.
   
 11. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nafikiri hata majirani zetu pia wamefurai. Nchi nyingi zinapenda kushirikiana na sisi kwa sababu viongozi wetu hawajali rasirimali zetu. Dr. Slaa ,kampeni zake lazima ziliwatingisha wanyonyaji, alisema anagombea urais wa Tz sio Africa mashariki, Tanzania kwanza mengine baadaye na rasirimali zetu zinufaishe Tz kwanza. Msimamo kama huu lazima utaogopwa na wanyonyaji. Na nchi nyingi za magharibi ni wanyonyaji na 1.
   
 12. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una maana makampuni ya Canada hayalipi kodi, review your comments please!
   
 13. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kkwa mujibu wa mikataba ya kimataifa, haitakiwi nchi yeyote kuingilia maabo ya ndani ya nchi ingine. So kama wa TZ wenyewe hawachukui hatua zozote kurekebisha hali ya nchini kwao wanabaki kutegemea mataifa ya kigeni hata katika kudai marekebisho ya Katiba na Tume Huru ya Uchaguzi, siku ingine si tutawaambaia hayo mataifa ya nje kulala na wake zetu ili tupate watoto? Tuache kutazama watu wa nje watafanya nini, tujiulize sisi watanzania tutafanya nini kurekebisha hii hali?
   
 14. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ninachokijua mataifa hayo nje mnayoyasema ni kigeugeu kweli kweli, angeshinda Dr Slaa wangemkumbatia na sera zake za kuwanufaisha wanyonge. Kumbuka Mwalimu Nyerere was among the major reciepient of donor aid from all corners. It all depends on what we are doing ourselves, so wake up Tanzanians stop complaining take action, and it is now or never.
   
 15. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hili neno..!!:wave:
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ina maana ni watanzania ndio wanatakiwa kuamka badala ya kudakia na kuabudu kauli za viongozi waliopo madarakani bila kujua wana lengo gani. Frantz Fanon aliwahi kusema kwamba watawala wa kiafrika hawagombei madaraka kwa sababu wana uchungu wan umaskini na unyanywaji wa watu wao bali wanagombea kuingia madarakani ili waweze kuongea kama wazungu, kula vyakula vya kizungu, kuendesha magari ya kizungu, kuishi nyumba za kizungu na ikiwezekana kufanya mapenzi na wanawake wa kizungu.

  Hii dhana ndiyo aliyokuwa anahubiri dr. slaa, wachache walimuelewa lakini wengi walichanganywa na kauli pingamizi zilizotoka ccm. ni jukumu letu kuelimisha wananchi vya kutosha ili 2015 waelewe kupiga kura maana yake nini, na kulinda kura
   
 17. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa mawazo ya wachangia mada; ni kwamba dr slaa anatishia nchi za magharibi?

  Kichuguu amechangia vizuri sana, tena kwa kuweka arguments za maana.

  Kuhusu suala la kulipa kodi kwao, watalipa where they have done a taxable activity kwao. Kuna mambo ya offshore siku hizi.

  Ametanabahisha kuwa private sector ndio mara nyingi inayotafuna hela.

  Kuhusu mabalozi kuwa frontline, wanakuwa wanafanya hivyo kama agents wa walemabepari; wanakuwa ama wamewakamatisha au wana maslahi nao.

  Sisi wenyewe ndio wajinga; tuerevuke.


  Dr slaa ameshindwa kutishia majimbo ya clergy wambakishe, ataweza kutishia mataifa?
   
 18. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2010
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Gurudumu,
  Wenzetu balozi zao zinawasikiliza raia wao na kujaribu kuwasaidia iwezekanavyo siyo kwenye uwekezaji tu, hata raia wao wakikamatwa kwa kuvunja sheria ugenini balozi zao bado zinajitokeza kuwatetea na kuwaombea waachiwe lakini haina maana kuwa serikali zao ndo zimewatuma wakawekeze au wakafanye uhalifu...mifano iko mingi, ubalozi wa Japan Tanzania ulijitokeza kwa niaba ya kampuni moja ya kijapani, kuhoji ushuru wa magari yanayoagizwa toka Japan (habari yenyewe ilikuwemo humu JF kitambo kidogo), balozi za Marekani, Uingereza, Canada, Australia nk. zimejitokeza kutetea (ama kuombea) raia wao au makampuni ya raia wao mara kwa mara. Sijui kama ubalozi wetu umejaribu hata kumjulia hali yule Mtanzania aliyeko guantanamo, anyway that's another story for another time... Ndo maana si jambo la ajabu hizo balozi ulizotaja zilifanya ulivyosema...

  Wa kulaumiwa ni sisi wenyewe kama tunakubaliana na kila wanachotuambia, mfano mzuri Singapore, Malaysia wao wananyonga tu wahalifu hata ubalozi uombe vipi... lakini bado nchi za magharibi zinawaheshimu, sisi tunashindwa nini kusimamia maslahi yetu wenyewe? Wahenga walisema usipojiheshimu, hutaheshimiwa! Hebu fikiria waziri mzima anakimbiza mabosi wa makampuni ya madini mpaka ulaya hotelini ili wasaini mikataba, halafu tunategemea watuheshimu kweli? Wawekezaji hawaji kutuletea maendeleo wao wanachojali ni kutengeneza faida as much as they can, sisi badala ya kuwabana tufaidike kisawasawa na uwekezaji wao tunawachekeachekea tunaridhika na 3%, heshima itoke wapi? Sorry for venting, lakini kwa kweli inaudhi sana...
   
 19. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  check tena uelewa wako kuhusu tax jurisidiction,hao investors wanalipa kodi hapa kutokana na income wanayogenerate + repatriated income also wanalipa kodi nchini kwao kwa hiyo nchi yao inafaidika
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nadhani nakubaliana na wewe lakini jaribu kukumbuka kwamba kuna mfumo ambao hizi nchi zinatumia ndiyo maana zina tabia moja bila kujali ni nchi ya ulaya au Asia. Siyo kila mara wanachosema hadharani ndicho walichomaanisha.

  ili viongoze wetu waweze kujiheshimu na wazungu wawaheshimu, ni lazima wananchi washike hatamu. kama viongozi wanajua kwamba watakuwa madarakani tu hata iweje, wanajua wakila hawatafanywa lolote, wanajua wakiboronga hawatawajibishwa kwa namna ambayo ni definitive, basi wataendelea kufanya mambo wanavyofanya sasa hivi. wazungu kwa kuliona hilo ndiyo maana wana mifumo imara kabisa ya kuwasiliana na kujadiliana na viongozi wetu, wakiamini kwamba chochote watakachofanya kupitia hawa vibaraka wetu hakuna mtu atakaye tengua.

  hili hasa ndilo tatizo ambalo watanzania wachache wanaolielewa wanatakiwa kutumia nguvu zao zote kuelimisha wananchi ili ccm na pengo wanapohubiri amani wananchi waelewe amani maana yake ni nini. maana ya amani ni uzezeta na ujinga wa kujitolea kunyonywa na kudhulumiwa. hapa sina maana tunahitaji kupigana bali tuwe na ufahamu kwamba tunapopiga kura tunachagua nini. hatuchagui viongozi bali tunachagua maisha yetu na vizazi vijavyo.
   
Loading...