Nchi za magharibi zimefurahi Dr Slaa kushindwa

Nchi za magharibi zimefurahi Dr Slaa kushindwa

sikubaliani na wewe mataifa ya nje yanajua kila kitu na wanafanya makusudi kutunyonya! Hakuna anayetuonea huruma zaidi ya kutufilisi tuu na kutumia ujinga wetu kama daraja lao!

Wanatuonea huruma kwa ujinga wetu siyo kwa sababu wanatakaa tuwe na hali nzuri zaidi. Wanajua kuwa kutokana na ujinga wetu tunaweza kuwanufaisha mahasidi wao, na hilo ni gumu kwao kumeza. Kukosekana kwa utawala wa kisheria kunaruhusu hali ambayo siyo nzuri kwa manufaa ya Magharabi na hilo ndilo ninalotaka tu-exploit
 
Umekosea.. Canada wananufaika.. Coorporate taxes zinalipwa Canada 40% kazi za management na consultant kwa Ajili ya migodi zilipewa kampuni ya Canada. Bariki shareholders wengi ni wacanada wanaspend hela nchini Canada hivyo hukuza uchumi wa nchi Yao.
Kisheria Canada hairuhusu kampuni kuchimaba maliasili zao Kama Hiyo kampuni halimikiwi 30% na wacanada, na top management lazima ease wawe wacanada! Jiulize ni kwanini watumishi wa ubalozi wa Canada walikuwepo Dodoma wakati wabunge wanajadili mikataba ya madini
Angalia Corporate Tax return form ya kanada niliyoambatanisha hapa, chunguza maswali ya 151, 169, 207, 221,256 had 259 . Yes kuna wanachopata kutokana na mapato ya Barrick kutokana na sababu mbalimbali, lakini sehemu kubwa ya mapato yanayotokana na Barrick inayofanya kazi bongo hailipiwi kodi huko kulingana na vifungu hivyo nilivyotaja hapo juu

http://www.cra-arc.gc.ca/E/pbg/tf/t2/t2-lp-09e.pdf
 
Aliyetoa mada hii Gurudumu alitoa mpya pale aliposema eti nchi za Magharibi zinachukia serikali kama za Zimbabwe, Venezuela na Rwanda kwa vile zinafanya vizuri na wanawaonea wivu kwa kuwanyima rasilimali. Huo ni uongo tunaolishwa waafrika na tunafundishwa shuleni kuanzia primary hadi chuo kikuu.
Ukweli ni kuwa nchi za magharibi zinachukizwa na nchi hizo kwa sababu wanawanyanyasa watu wao hivo kuwapa mzigo usiokuwa wao. CHADEMA utaratibu wake uliokuwa unakusudiwa wa utawala ni tofauti sana na nchi hizo kandamizi kama Venezuela, Zimbabwe na Rwanda. Rwanda ilikuwa kipenzi cha nchi za magharibi kwa jinsi ilivoleta maendeleo na ndio walioisaidia kufika hapo. Kagame ameanza kukandamiza vyama nya upinzani na hapo ategemee upinzani kutoka nchi za magharibi.
Nchi za Magharibi zinataka Afrika iendelee ili iwe mdau wa biashara kuliko kuwa tegemezi kwao. Nchi za magharibi zingefurahishwa sana kama CHADEMA wangeingia madarakani kwani wanajua maendeleo yangekuwepo.
Viongozi wa Afrika wanaposhindwa kuongoza wanawasingizia nchi za magharibi kuwa zinawanyonya huku wao ndio wameshindwa kufanya kazi na kuongoza nchi zao kufikia mafanikio.
 
Back
Top Bottom