Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Pamoja na upungufu wa matamko hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesifu namna mkutano huo wa leo ulivyoonesha umoja dhidi ya Israel
Katikati ya mkutano huo katibu mkuu wa umoja wa nchi za kiislamu amelaumiwa na wachambuzi hao kwa kutumia sana maneno yenye kuonesha kuna maatumaini kwa Israel kufannya mambo aliyoyaorodhesha.
Hata hivyo mwishoni mwa kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa nchi zaidi ya 51 na wawakilishi wa nchi nyengine kadhaa tamko kuu limetoka kwa kuitaka Israel isitishe vita na iache kutaja kuwa inajilinda huku ikiuwa wananchi na watoto kwa maelfu.
Katika tamko hilo hakukuwa na sehemu ilipotajwa Hamas kwa kupewa lawama yoyote ile.Hilo limekuwa kama ni kukubaliana na tamko la katibu mkuu wa UN kuwa shambulio la Hamas halikuja bila sababu.
Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na raisi wa Iran,Mohammed Alraisi na raisi Bashar El Assad wa Syria.
Raisi wa Iran alisema wamekutana hapo kwa niaba ya umoja wa kiislamu ili kutoa tamko la kulaani Israel kutokana na mauwaji yake kwa wapalestina.
kwa upande wake raisi Al Assad alizishutumu nchi zilizorudisha uhusiano na Israel kwa kusema kila tunavyotoa mkono zaidi kwa mazayuni ndio tunavyokaribisha mauwaji kwetu.