Nchi yetu inaitwa Tanganyika

Khaa!! hii nayo ni sababu tosha kabisa ya kuvunja Muungano :wave:
 
Hakika Tanganyika ni lazima irudishiwe hadhi yake ya nchi baada ya kuanza serikali tatu.Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara.Hata uki "undo" unapata Tanganyika na Zanzibar,haihitaji ufundi mwingi kufamu umuhimu wa Tanganyika.Kuhusu kuvunjika kwa muungano ni dhahiri haiepukiki kutokana na kero za muungano kutotatuliwa kwa moyo wa dhati badala yake maslahi binafsi ya baadhi ya wakubwa ndiyo yamezingatiwa,matokeo yake yatadhihirika 2015.
Mpigakelele anamaslahi binafsi na jina hilo analolitetea kwa mujibu ya maelezo yake hayana mashiko kwa watanganyika ambao baada ya miaka 50 ya uhuru wameshudia nchi zingine zipiga hatua kubwa kimaendeleo huku sisi tukiweza kugharimia 60% ya matumizi yetu! Ajabu;
Tuna taka Tanganyika yetu.
 
jina lina udini hili......dogo aliweka initial ya ya jina lake na dini yake

Tanzania=Tanganyika +zanzanzibar +i ( initial ya dini yake)+ a (initial ya jina lake)
 
Utumwa huo pimbi wewe.. Unakataa mpaka jina lako u ajipendekeza na na sisi.. Au unapenda hiyo zannnnn huh.... Aibu mtu mzima hiyo wacga kukataa unyika wako huo.. Jina limekaa kimsitu msitu kinoma mpaka mwenyewako unaliogopa..
Ebu tiririka vizuri...sijakupata. Vinginevyo nitaamini umeshidwa kujenga hoja ama ya kukubali au kukataa kile nilichoeleze.
 
Huu nao ni upumbavu...mnapigania jina?

-------- ni wewe usiye na hela, kazi wala demu! hatupiganii jina, tunapigania nchi yetu yenye kila kitu lakini vinapotea katika kivuli cha muungano
 
Ugonjwa wa MTanganyika kujiita Mtanzania Bara Bila hata historia ya Tanzania kusema nini maana ya Tanzania ni kirusi sugu vichwani mwa wavivu wa kufikiri watu wanapoana mwanamke ndiye anayebadili jina Hivi katika muungano wetu Tanganyika alikuwa Demu?
 
Huyu kidudu mtu aliyetukalia katukamata kweli kweli...Nchi imelala,hatuna kiongozi na hata watawala tulionao hawana meno! Wapo kisultani tu...Uongozi wa kijanja janja...likitokea hili linaibuliwa lingine ili kuteka umakini wa watu! Huu Uzanzibar na uzanzibara hautupeleki popote na hata ingekuwepo serikali moja ama kumi za kuendeshwa kwa mfumo huu hatutegemei muugiza!
 
Hilo halina ubishi. Tanganyika na watanganyika wapo. Siku ya tarehe 09/12 iwe ni siku ya kuadhimisha uhuru na Jamhuri ya Tanganyika na sio Tanzania Bara!
 
Hebu tuwekeni sawa ,hivi Tanganyika ni nchi au si Nchi ? Isije kuwa Zanzibar wanapiga mekelele wakati wenyeji hawaelewi hata Tanganyika ni kitu gani !
 
Hebu tujiulize tarehe 9 deckila mwaka huwa tuna sherehekea nini? Jana nilisikia upotoshaji toka kwa Msekwa ati Tanganyika ilifutwa. Hii mi kweli au ni muendelezo wa siasa maji taka za Maccm??
 
Hebu tujiulize tarehe 9 deckila mwaka huwa tuna sherehekea nini? Jana nilisikia upotoshaji toka kwa Msekwa ati Tanganyika ilifutwa. Hii mi kweli au ni muendelezo wa siasa maji taka za Maccm??


Katika hotuba ya JK alituambia zaidi ya 65% ya watanzania hawakuwepo enzi za Tanganyika, hivyo kigezo cha kuidai Tanganyika siyo cha msingi tena. Halafu baadaye nikawasikia wajumbe wa Bunge la katiba pamoja na wananchi wengine wakiisifia ile hotuba ya mh. Rais. Nimeogopa sana aisee...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…