Nchi ya Niger yajitoa kwenye umoja wa Francophone

Nchi ya Niger yajitoa kwenye umoja wa Francophone

Strong ladg

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
856
Reaction score
2,069
Nchi ya Niger imejitoa rasmi kutoka umoja wa nchi zinazotumia lugha ya kifaransa pamoja na zile zilizokuwa makoloni ya Ufaransa ujulikanao kwa lugha ya kifaransa kama Organisation Internationale de la Francophonie ( OIF).

Taarifa ya kujitoa huko ilitolewa na wizara ya mambo ya nje ya Niger mnamo jumatatu ya tarehe 17 Machi 2025.

Hata hivyo, Niger ilikuwa imesimamishwa uanachama kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwaka 2023.

CHANZO: Shirika la habari la Niger ( RTN)
 
Nilisikia pia na Mali ipo.

Kimsingi hizi jumuiya hazina faida yoyote.

Binafsi napendekeza hata Umoja wa Afrika ufutwe au wanachama waachane nao.

Kwanini tunashindwa kuwa na jumuiya zilizo imara kama Umoja wa Ulaya.
 
Nilisikia pia na Mali ipo.

Kimsingi hizi jumuiya hazina faida yoyote.

Binafsi napendekeza hata Umoja wa Afrika ufutwe au wanachama waachane nao.

Kwanini tunashindwa kuwa na jumuiya zilizo imara kama Umoja wa Ulaya.
Umoja wa Afrika ni chombo kinachotumiwa na Umoja wa Ulaya kufanikisha mambo yao. Kuuvunja sio rahisi labda wapatikane viongozi wazalendo kwelikweli. Sio hawa vibaraka
 
Sasa ndio ninaweza kusema Afrika inaanza kuamka 💪 Rwanda nae kawafukuza Wabeleji.

Thank you God.
Rwanda anatuigizia tu😂😂. Mkataba wa kuwauzia mádini ya Kongo nchi za Umoja wa ulaya ambao Rwanda walisaini mwaka jana si haujavunjwa? Sasa nini kilichobadilika hapo?
 
Nadhani ndio time ya Tanzania kujitoa jumuhia ya madola!
 
Back
Top Bottom