Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 198
- 322
Nchi tatu za Afrika Magharibi, Mali, Niger na Burkina Faso hivi karibuni kwa nyakati tofauti zimetangaza uamuzi wao wa kujitoa katika Jumuiya ya Francophonie (OIF). Nchi hizo ziliwahi kujulikana kama nguzo ya “Afrika ya Ufaransa”, lakini sasa zimechukua hatua thabiti kuondoa alama za kikoloni, ili kuunda upya utambulisho wake wa kitaifa unaojitegemea.
Mali, Burkina Faso na Niger zote zilitawaliwa kikoloni na Ufaransa. Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo tatu na Ufaransa umezorota kwa kasi, na zimeitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake wote kutoka kwenye nchi hizo. Baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa vinaamini kwamba kujiondoa kwa Mali, Burkina Faso na Niger kutoka katika OIF kunaweza kuwa ni jaribio la “kukata uhusiano wa kikoloni” kabisa na Ufaransa.
Kabla ya hapo, nchi hizo tatu za Afrika Magharibi zilikuwa tayari zimeingia kwenye mchakato wa kuondoa matumizi ya lugha ya Kifaransa. Julai 26, mwaka 2023, serikali ya Mali ilitangaza kwamba Kifaransa haitakuwa tena lugha rasmi ya kitaifa. Kwa mujibu wa katiba mpya ya nchi hiyo, hadhi ya Kifaransa ilishushwa hadi lugha ya kikazi nchini Mali, wakati lugha 13 za kitaifa zikipewa hadhi ya lugha rasmi. Pia, serikali ya Mali ilisema kwamba inaandaa mpango wa kuondoa Kifaransa hatua kwa hatua katika maeneo yote ya maisha ya watu.
Serikali ya mpito ya Burkina Faso ilitangaza mwezi Desemba mwaka 2023 kupitishwa kwa mswada wa marekebisho ya katiba, na kutokana na katiba hiyo, Burkina Faso itaondoa hadhi ya Kifaransa kuwa lugha rasmi, na kuishusha hadi kuwa lugha ya kikazi.
Hadi sasa Kifaransa bado ni lugha rasmi ya Niger, lakini nchi hiyo pia imechukua hatua mbalimbali za kuondoa alama za kikoloni. Mwaka 2023, serikali ya Niger ilipitisha “Glory to the Fatherland” kama wimbo wake mpya wa taifa, badala ya “Wimbo wa Niger” uliotungwa na mtunzi wa Kifaransa. Baada ya serikali ya kijeshi kuingia madarakani, pia ilichukua hatua nyingi za kupunguza ushawishi wa Ufaransa. Mwezi Oktoba mwaka 2024, serikali ya mpito ya Niger ilitangaza kubadilisha jina la barabara ya Charles de Gaulle katika mji mkuu Niamey kuwa barabara ya Djibo Bakari ili kumkumbuka kiongozi huyo muhimu katika harakati za kupigania uhuru wa Niger.
Lugha ndicho chombo cha kisiri zaidi cha utawala wa kikoloni. Wakati wakoloni wa Kimagharibi walipokuwa wakitekeleza kile kilichoitwa “jukumu la ustaarabu” barani Afrika, walidai lugha zao ni “lugha za kistaarabu” na kuzipandikiza katika jamii za kikoloni kupitia mfumo wa elimu na utamaduni. Baada ya nchi za Afrika kupata uhuru, lugha za kikoloni zilibaki kuwa lugha kuu katika serikali, elimu na mifumo ya sheria. Hali hii ni kuendelea kwa mamlaka ya kikoloni ambayo inakandamiza lugha za kiasili za Afrika.
Sasa, nchi za kikoloni za Magharibi zilizokuwa na nguvu kubwa ya kuvamia dunia nzima, hazina tena utukufu wao wa zamani, uchumi wao umedorora, huku ushawishi wao wa kimataifa ukishuka kwa kasi. Wakati huohuo, nchi za Afrika zinaendelea kwa haraka, na kutaka kuondoa kabisa alama za kikoloni. Lugha, kama alama wakilishi zaidi ya ukoloni, imewekwa kwenye ajenda ya utakaso na nchi nyingi za Kiafrika. Kifaransa ambayo hadhi yake ya kimataifa ni ya chini kuliko ile ya Kiingereza, ndiyo ya kwanza kuondolewa. Licha ya Mali, Burkina Faso na Niger, lugha ya Kifaransa imetolewa kama lugha rasmi katika nchi za Maghreb zikiwemo Morocco, Tunisia na Algeria, ingawa bado inatumika.