Nchi ya kusadikika na kisa cha binti Mfalme aliyebakwa; Baba wa binti anapofurahia kishika uchumba badala ya mahari

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Hiki ni kisa cha kweli lakini kimetokea kwenye hypothetical nchi ya kusadikika, naomba kisifananishwe na nchi yoyote ya kweli, wala huyo baba mwenye nyumba, asifananishwe na mtu yeyote.

Kwenye nchi ya kusadikika, kumetokea wafalme wengi. ila Mfalme ninayemzungumza hapa, namtambulisha kama Baba Mwenye Nyumba, ana binti yake mrembo aliyemlea akaleleka, kutokana na uzuri wa huyo binti, baba akaweka very high expectations za mahari ya binti huyo, hadi kuwaahidi ukoo mzima, siku binti akiolewa, kila mtu kwenye ukoo wake, na wananchi wote wa nchi ya kusadikika watanunulia motokari aina ya Noah, hivyo wananchi wa nchi ya kusadikika, wana legitimate expectations za Noah zao.

Likatokea tapeli Mshenzi Fulani, likamuhadaa huyo binti kwa chips kuku, likambaka, likamuweka kinyumba, sasa limemzalisha watoto kibao, na linamtumia kama kitega uchumi chake cha kumzalishia mali na huu ni mwaka wa 18!. Haya yote yalifanyika wakati wa ufalme wa wafalme waliotangulia kabla ya Mfalme Baba Mwenye Nyumba.

Ilipofika zamu ya Baba Mwenye Nyumba kushika ufalme, akavalia njunga jambo hili la nchi yake kufanywa shamba la bibi na vibaka hawa!. Hivyo alipopata taarifa ya ushenzi huo, akakasirika sana, akawakusanya ndugu zake wakamtokea huyo mshenzi aliyembaka binti yake na kumuweka kinyumba. Hakumtwaa binti yake kutokana na ameishakuwa mtu mzima ana ameishazalishwa watoto kibao, alichofanya Baba Mwenye Nyumba ni kutia kufuli maghala ya kibaka huyu kuzuia mali za binti yake zisitoke nje bila ya kutimiza masharti na kulipa fidia ya ushenzi wote aliofanya. Baba wa yule mbakaji akaja kuonana na Baba Mwente Nyumba, akamhakikishia Baba Mwenye Nyumba, kuwa anampenda kwa dhati binti yake na yuko tayari kulipa fidia, mahari na masharti yoyote atakayopangiwa ili mradi tuu ndoa ya watoto ao iendelee na binti aruhusiwe kuendelea kuzalisha mali za kuuza nje, hivyo baba kwanza akapanga masherti mapya, mahari na fidia ya ubakaji.

Mbakaji akasema amekubali kila kitu, ila kwanza wakae chini na kuzungumza jinsi ya ulipaji, maana mahari yenyewe sii haba!. Baba akaafiki wazo hilo, na wakaanzisha mazungumzo baina ya ndugu wa baba, na washenga wa mbakaji kuhusu namna ya kulipa hizo mahari.

Wakati wote wa mazungumzo, baba na ndungu zake wanasubiri kwa hamu, matokeo ya mazungumzo hayo, siku ya siku ikafika, taarifa ya mazungumzo ikatolewa, kwanza mbakaji akakubali kutimiza masharti yote, ikiwemo kugawana faida, kutoa matunzo, na vitu vingine vyote, ila kuhusu mahari, huyu mbakaji, hakuzungumza lolote, bali badala ya kuzungumzia mahari, na fidia, mbakaji akatoa ahadi ya kishika uchumba kinene, kuonyesha ana nia ya dhati ya kumuoa huyo binti, lakini hakuzungumzia lolote kuhusu mahari na fidia ya kumbaka binti yetu, kumweka kinyumba na kumtumia kama kitega uchumi cha kumzalishia mali kwa kipindi cha miaka 18!.

Baba mwenye nyumba, akasimama kibarazani na kuonyesha furaha yake kwa ahadi ya kishika uchumba hicho, akamuomba baba wa mbakaji akilete haraka hicho kishika uchumba ili kusaidia sekta mbalimbali kutokana na hali ngumu ya nyumbani kwake.

Kikawaida, kishika uchumba, huwa hakiahidiwi, bali ukijijua tuu unakwenda ukweni kwa nia ya kujitambulisha kuposa ili kuja kuoa, una kwenda na mshenga weko, na kishika uchumba chako, mmekiviringisha kwenye anjivu, hengachifu, wala bila hata kutaja kiasi chake.

Jee ungekuwa ndio wewe, baba mwenye nyumba, binti yako, amebakwa kwa miaka 18, amewekwa kinyumba, anazalishwa na kugeuzwa kitega uchumi. Wewe kwa hasira, unamchukua binti yako kumfungia ndani, na kutoa kiwango cha fidia na mahari na masharti, kisha huyo mbakaji anakujia na ahadi tuu za kishika uchumba tuu na wewe unafurahi!. Ungekuwa wewe ungefanya nini?.

My Take.
Kwa vile binti ameishabakwa na kuzalishwa sana, priority no.1 ni kulipa mahari na fidia yetu kwanza kabla ya mengine, mtu amembaka binti yangu, Nampa fidia, hazungumzi lolote kuhusu fidia, bali anakuja na ahadi ya kishika uchumba?!, nilidhani kama ni kishika uchumba, atakuja nacho mkononi na sio ahadi, akija na a roadmap, analipaje mahari ya binti yetu!. Kwa jinsi tulivyoshangilia hiki kishika uchumba, sitashangaa, kama tutayaondoa yale makufuli tuliomfungia mbakaji huyu na kuruhusu kuendelea kumtumia binti yetu!. Kuna mambo mengine, ingekuwa nchi zetu ni nchi nyingine, yasingewezekana, lakini kwa vile nchi hii ni nchi ya kusadikika, then everything is possible.

Jumamosi Njema.
Paskali,
 
Mkuu Paschal, wakati unabandika hili bandiko ulijiuliza maswali kama vile... "kuna watu wasiojulikana? Kuna watu watalisoma huku wameuma meno? Kuna wakati unaweza lazimika kupimwa mkojo bila hiyari yako? Je chombo chako cha habari hakitahusika na habari za uongo? na... na... na...?"

Nanukuu sentensi ya mwisho:

Jee ungekuwa ndio wewe, baba mwenye nyumba, binti yako, amebakwa, amewekwa kinyumba, anazalishwa na kugeuzwa kitega uchumi. Wewe kwa hasira, unamchukua binti yako kumfungia ndani, na kutoa kiwango cha fidia na mahari na masharti, kisha huyo mbakaji anakujia na ahadi tuu za kishika uchumba tuu na wewe unafurahi!. Ungekuwa wewe ungefanya nini?.
 
... Hiki ni kisa hypothetical kwa nchi ya kusadikika, naomba kisifananishwe na nchi yoyote ya kweli, wala huyo baba, asifananishwe na yeyote.

Kisa hiki ni kisa cha kweli kilichotokea kwenye nchi ya Kusadikika. Mfalme wa nchi ya Kusadikika,...
Contradiction!
 
Wanabodi,

Hiki ni kisa hypothetical kwa nchi ya kusadikika, naomba kisifananishwe na nchi yoyote ya kweli, wala huyo baba, asifananishwe na yeyote.

Kisa hiki ni kisa cha kweli kilichotokea kwenye nchi ya Kusadikika. Mfalme wa nchi ya Kusadikika, ambaye kwa hapaq nitambulisha kama Baba Mwenye Nyumba, ana binti yake mrembo aliyemlea akaleleka, kutokana na uzuri wa huyo binti, baba akaweka very high expectations za mahari ya binti huyo, hadi kuwaahidi ukoo mzima, siku akiolewa, kila mtu atanunuliwa Noah.

Likatokea tapeli Mshenzi Fulani, likamuhadaa huyo binti kwa chips kuku, likambaka, likamuweka kinyumba, sasa limemzalisha watoto kibao, na linamtumia kama kitega uchumi chake.

Baba alipopata taarifa ya ushenzi huo, akakasirika sana, akawakusanya ndugu zake wakamtokea huyo mshenzi aliyembaka binti yake na kumuweka kinyumba. Kwanza akamtwaa binti yake na na kumrudisha nyumbani na kumfungia ndani, yule mbakaji akamhakikishia baba kuwa anampenda kwa dhati binti yake na yuko tayari kulipa mahari yoyote ili kurejeshewa binti, hivyo baba kwanza akapanga masherti mapya, mahari na fidia ya ubakaji.

Mbakaji akasema amekubali kila kitu, ila kwanza wakee chini na kuzungumza jinsi ya ulipaji, maana mahari yenyewe sii haba!. Baba akaafiki wazo hilo, na wakaanzisha mazungumzo baina ya ndugu wa baba, na washenga wa mbakaji kuhusu namna ya kulipa hizo mahari.

Wakati wote wa mazungumzo, baba na ndungu zake wanasubiri kwa hamu, matokeo ya mazungumzo hayo, siku ya siku ikafika, taarifa ya mazungumzo ikatolewa, kwanza mbakaji akakubali kutimiza masharti yote, ikiwemo kugawana faida, kutoa matunzo, na vitu vingine vyote, ila kuhusu mahari, huyu mbakaji, hakuzungumza lolote, bali badala ya kuzungumzia mahari, mbakaji akatoa ahadi ya kishika uchumba kinene, kuonyesha ana nia ya dhati ya kumuoa huyo binti, lakini hakuzungumzia lolote kuhusu mahari na fidia ya kumbaka binti yetu, kumweka kinyumba na kumtumia kama kitega uchumi cha kumzalishia mali!.

Baba mwenye nyumba, akasimama kibarazani na kuonyesha furaha yake kwa ahadi ya kishika uchumba hicho, akamuomba akilete haraka ili kuaidia hali ngumu ya nyumbani kwake.

Kikawaida, kishika uchumba, huwa hakiahidiwi, bali ukijijua tuu unakwenda ukweni kwa nia ya kujitambulisha kuposa ili kuja kuoa, una kwenda na mshenga weko, na kishika uchumba chako, mmekiviringisha kwenye hengachifu, wala bila hata kutaja kiasi chake.

Jee ungekuwa ndio wewe, baba mwenye nyumba, binti yako, amebakwa, amewekwa kinyumba, anazalishwa na kugeuzwa kitega uchumi. Wewe kwa hasira, unamchukua binti yako kumfungia ndani, na kutoa kiwango cha fidia na mahari na masharti, kisha huyo mbakaji anakujia na ahadi tuu za kishika uchumba tuu na wewe unafurahi!. Ungekuwa wewe ungefanya nini?.

Jumamosi Njema.
Paskali,


Kaka Paskali wewe mchochezi, sijui kama umesahau kuwa Mayala kikwetu ni njaa. Unaweza kujikuta upo mikononi mwa wale watu
 
Wakuonea huruma ni hao ndugu za baba mwenye nyumba ambaye kafurahia "ahadi" ya kishika uchumba. Badala ya kumwambia mzee mambo gani haya tena? Mbona hailipwi mahari, hakuna fidia ya kubakwa na binti mbona anaendelea kumshughulikia nasi twalipwa kishika uchumba?
Sasa wao ndugu badala ya kuhoji hayo wanashangilia na kukatika mauno kucheza mdumange pamoja na baba mwenye nyumba kiasi cha baba mwenye nyumba kuona kuwa alichofanya yaani kukubali kishika uchumba ni jambo la maana sana.
Ila hadithi hii inafanana na tukio fulani silikumbuki sawasawa ila nikikumbuka nitarudi tena
 
Binti kabakwa? Hata sisi kwetu huwa tunakubali kulipa mahari yote but kwa awamu na tukishatoa awamu moja ndio imetoka hiyo deni la kifo
 
Hahahaa Pasco you nailed it, kuna wanafamilia aina ya kina Mzee Mwanakijiji wanafurahia kishika uchumba hewa wanasema si haba, hawajali kwa sababu dada yao anaolewa na tajiri wamepata shemeji tajiri bila kujali dada yao amekuwa akibakwa kwa zaidi ya miaka 18.

Ila Pasco kwa bandiko hili sahau uDC labda kama umesha give up.
 
Mambo haya yanavyo kwenda yanaonyesha nchi hii hatuna wana sheria kwanini kila siku tunapatwa na aibu mliosoma sheria mko wapi? Tunaangamia tuokoeni
 
Kwa kuwa Mayalla kule nyumbani kwa baba mwenye nyumba maana yake ni njaa

Basi itakuwa msimulizi wa kisa hiki anasikia njaa
 
Back
Top Bottom