Nchi nyingi za Afrika kutopigia kura mgogoro wa Ukraine sawa na China ndio kutofungamana na Upande wowote?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,931
141,894
Nimeona nchi nyingi za Afrika zikiongozwa na kinara wa uchumi Afrika kusini hazijapiga kura kuhusiana na mgogoro wa Ukraine na Russia pale UN

Nchi hizo zimeungana na China ambaye pia hajapiga kura.

Ndio nauliza kuwa kundi moja na China ndio Kutofungamana na Upande wowote?

Ingekuwaje kama China angemuunga mkono Russia?

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna mambo mawili yanayokinzana:
Kwanza, hatuungi mkono na hatupendi vita na watu kuuana - hapo inamhusu Russia.
Pili, hatupendi siasa za kujitanua na kutaka kutawala dunia zinazofanywa na marekani. Hakuna anayefurahia ukoloni mpya unaoletwa na United States!
 
Nimeona nchi nyingi za Afrika zikiongozwa na kinara wa uchumi Afrika kusini hazijapiga kura kuhusiana na mgogoro wa Ukraine na Russia pale UN

Nchi hizo zimeungana na China ambaye pia hajapiga kura.

Ndio nauliza kuwa kundi moja na China ndio Kutofungamana na Upande wowote?

Ingekuwaje kama China angemuunga mkono Russia?

Maendeleo hayana vyama!
Tumefuata mkumbo wa China tu; hamna lolote. China wanatafuta sababu ya kuivamia Taiwan; siku hilo likitokea tutaunga mkono. Tumesahau kuwa mwaka 2002 tulipinga USA kuivamia Iraq.
 
Tulipaswa kuwa upande gani mkuu ili tuwe "salama" machoni pako mkuu ?
 
Tulitakiwa tuwe upande wa ukweli; msema kweli siku zote ni mpenzi wa Mungu. Kitendo cha urusi kuivamia Ukraine na kusasabaisha vifo na mateso kwa raia wa Ukraine wasiokuwa na hatia ni haramu !

Ila sisi kuivamia uganda haikua haram si ndio?
 
Nimeona nchi nyingi za Afrika zikiongozwa na kinara wa uchumi Afrika kusini hazijapiga kura kuhusiana na mgogoro wa Ukraine na Russia pale UN

Nchi hizo zimeungana na China ambaye pia hajapiga kura.

Ndio nauliza kuwa kundi moja na China ndio Kutofungamana na Upande wowote?

Ingekuwaje kama China angemuunga mkono Russia?

Maendeleo hayana vyama!
Kumbe wewe ni mchanga sana kwenye Siasa, ulikuwa chawa wa zama
 
Eti hatufungamani na upande wowote. Hii mimi huwa na shindwa kuelewa kabisa.

Chagua kwenda ama kubaki. Wewe hujui uende ama ubaki.

Ni uwezo mdogo wa kusimamia mambo tunayoyaamini.
 
Back
Top Bottom