PostGE2025 Nchi na kilio cha maji

PostGE2025 Nchi na kilio cha maji

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Una ziwa Victoria la 2 kwa ukubwa Duniani,ziwa Tanganyika lenye kina refu zaidi Duniani,ziwa nyasa,mto mara,maragarasi,ruaha,na mingine mingi bado una sehemu kubwa ya bahari kwamba huko maji yamekauka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi au sio???
Bado una ardhi isiyo kame zaidi ya 10% imejaaa maji chini.

Tuache masihara basi unaotokana na uzembe wetu.
 
Acheni uhuni, maji hayapaswi kukosekana tanzania. Wale waliopewa dhamani kuongoza kwa miaka 64 sasa wameshindwa kutatua shida hiyo. Ardhini maji kibao unatwambia tusubiri mvua. Ni ujinga tu ndo umetufikisha hapa.
 
Ila kuna vitu vya msingi sana havitakiwi kukosekana jamani. Basi maji kweli, maji!!!!!! Kuna watu wanabeba dhima kubwa sana hawajui tu
Halafu ukaniambie nichague chama kikae madarakani ili kinihilikishe...big no
Wao mbona hawakosi maji wala umeme!!!!!! Hawajui wananchi vipi tunaumia na joto hili 🥵
 
Mnatupigia kelele tu hapa.

Tatizo linaeleweka ni kwamba vyanzo vya maji vumeharibiwa kwa kuchepushwa kwa maji, watu wamekata na wanaendelea kukata miti kwenye misitu ya asili wanatengeneza mikaa bila kukemewa na kuchukuliwa hatua.
Asante kwa kufikiri kwa kina , swala la mazingira ni pana sana. Watu wengi wanaliona kama ni dogo ila mazingira ndio kila kitu. Mazingira yanayotuzunguka kuanzia miti, vyanzo vya maji , mabonde , milima , vyombo vya moto tunavyotumia , taka tunazotumia , wanyama tunaowala na kilimo vyote hivi vinaathiri maisha yetu . Joto limezidi duniani kote , barafu zinayeyuka sehemu mbali mbali za dunia . Visiwa na majiji vinamezwa kwa uongezekaji wa maji bahari. Mengi yapo , swala ni utunzaji wq mazingira , sote tunapaswa kuwajibika.
Mmekutana wote wasaka tonge(UTEUZI).

Vijana kama nyinyi mna mchango mdogo sana kwa taifa ,ningekuwa Abdul ningesitisha ajira yenu haraka.

Changamoto duniani hazijaanza December 2025 ,zipo tangu enzi na enzi toka karne na karne ila AKILI KUBWA zinaumiza vichwa kukabiliana na changamoto ili dunia iwe sehemu salama za kuishi.

Mvua zinanyesha hadi mafuriko ,mito hadi inatapika maji ,nimeanza kusikia miradi ya kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji muda mrefu sana zaidi ya miaka 10 lakini mpaka leo hakuna hata bwawa moja lililojengwa.

Tungekuwa na viongozi wazalendo kamwe tusingepata tatizo la maji ,tungekuwa na project kubwa za kujenga mabwawa kuhifadhi maji tungetatua tatizo la maji permanent.

Njia ya pili ya kutatua matatizo ya maji ni kuchimba visima na kuhifadhi kwenye matank ,hii nayo inatushinda? Hivi Samuya akiuza zile Buggatti mbili za Abdul na Royce Rolls si tunachimba visima kila kata huko Dar?

Hivi kuna nchi yenye mazingira mabovu ya kupata maji kama UAE? Ebu nenda Abu dhabi au Dubai uone kama wana shida ya maji ,sehemu kubwa ni jangwa ,joto kali ,hakuna miti ,ardhi mafuta tupu pamoja na changamoto zote hizo lakini hawana shida ya maji.

kama wao wana mafuta na sisi tuna rasilimali nyingi sana kuliko hata mafuta yao ila wao wameendelee kwasababu hawachek na nyani ,wamefocus kwenye maendeleo ya watu ,huku kwetu viongozi wamefocus kwenye maendeleo ya familio zao na wahuni wanaowazunguka tu.
 
Una ziwa Victoria la 2 kwa ukubwa Duniani,ziwa Tanganyika lenye kina refu zaidi Duniani,ziwa nyasa,mto mara,maragarasi,ruaha,na mingine mingi bado una sehemu kubwa ya bahari kwamba huko maji yamekauka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi au sio???
Bado una ardhi isiyo kame zaidi ya 10% imejaaa maji chini.

Tuache masihara basi unaotokana na uzembe wetu.
Tatizo ni la viongozi wenye mamlaka ambao hawana nia ya dhati ya kumaliza tatizo la maji ,wao wanachowaza wakishaingia madarakani ni kutumia pesa za kodi kubakia madarakani.

Tuna water bodies za kutosha ,maji ardhini ya kutosha lakini TUNA SHIDA YA MAJI HATARI.
 
Ila kuna vitu vya msingi sana havitakiwi kukosekana jamani. Basi maji kweli, maji!!!!!! Kuna watu wanabeba dhima kubwa sana hawajui tu
Halafu ukaniambie nichague chama kikae madarakani ili kinihilikishe...big no
Wao mbona hawakosi maji wala umeme!!!!!! Hawajui wananchi vipi tunaumia na joto hili 🥵
Yaani katika vitu rahisi kutatua kwa 100% kwa hapa TZ ni maji lakini nashangaa imekuwa ni JANGA kweli kwenye miti hakuna WAJENZI.........TZ nzima imezungukuwa na water bodies kama zote ,ardhini maji safi na salama kama YOTE lakini DAR nzima week ya pili hakuna MAJI halafu kutwa kumsifia Aweso Aweso Aweso NON SENSE.
 
A
Dar kukosa Maji ni sawa na baba mwenye NYUMBA ununue Kuku jogoo aliyekomaa na wakati wa kula wakupe miguu ya jogoo

Ikiwa DSM inashikilia uchumi wa nchi kwa 80% je hatuwezi kuona Aibu kuwakosesha Maji

We don't need to find excuse on this
Aisee we jamaa umeongea point sana, kila siku huwa nawaza kwanini DSM hairejeshewi kama inavyoingiza??, yan huwa inafikirisha sana sehemu inayo changia pato la taifa kwa zaidi ya 18% lakini ndo sehem ambayo wanachi wake wanazidi kuteseka, kuanzia miundombinu ya usafiri na barabara na maji. Ki ukweli mapato yanayotokana na dar kuyatumia hayo hayo kuboresha miundominu na mikoa mengine halaf wananchi wanaotafuta hayo mapato wanateseka ni kitu cha kifedhuli sana.

Sasa hivi DSM imeelemewa, utitiri wa private sectors na fursa nyingine za biashara unaendelea ndani ya jiji na kila kijana anayetamani kufanikiwa anataman aje dar, population na huduma za kijamii ni irrelevant. Watu wanateseka makazi na huduma za usafiri sababu wamekua centered kwenye eneo finyu sana.

Haya mapato yanayogawanywa kwanini yasitumike kuboresha miundominu ili wanaozidi kuja kutafuta wasipate unnecessary obstacles? Kwaninj ule mpango wa kumega sehem ya pwani kuwa DSM Usiendleee kwa kulazimisha baadhi ya makampuni makubwa yahamie huko (ila yapewe specific period) na serikali igawe ardhi kwa njia ya kuuza kwa bei nafuu ili watu waanzishe makazi?

Kujenga barabara za mwendokasi si kutatua changamoto ya foleni…kwanza njia panda zote ziwekewe interchange, hii miradi ya mwendokasi isijengwe kwa kusua sua kama ilivyo sasa, lakini pia kariakoo ifike mahala sasa itafutiwe mbadala kuwekwe mpango wa kugawanya hawa wafanyabiashara na kutafuta sehem nyingne sio lazima milele kariakoo iwe sehem kuu ya biashara sio msaafu au biblia ile maana imekua kirusi sasa…

yani uchangie pato 18% + halafu wewe uhangaike barabarani, mara maji, umeme, msongamano wa watu, makazi kupandishwa bei zisizo na uhalisia aisee, serikali iangalie sana hawa wananchi wa DSM ni watu wasio na furaha kabisa (wengi wao sio wote)

Najua serikali ilianza kwa wao kuhama na kuhamisha serikali rasmi dodoma, basi waangalie hili la kuiongeza Dar kwenye sehem ndogo ya pwani, na kulazimisha baadhi ya huduma na vitu vingine pia vihame kwa awamu.
 
Back
Top Bottom