QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
NCHI MOJA MARAIS WAWILI
Tangu kuapishwa kwa Kikwete hakujakuwa na shamra shamra kuonesha kusherehekea ushindi kama katika chaguzi nyingine zilizopita. Wananchi mbalimbali wanasikitika na kulia sababu ya wanachoona kikiendelea. Wengi walijua na kuamini kuwa Kikwete hataweza kuendelea na kipindi cha pili cha Urais hasa kati ya sasa na 2015 kwa jinsi walivyomnyima kura lakini cha ajabu akatangazwa mshindi. Waliotarajia kununua siment kwa shilingi 5000 bila kodi ili kutengeneza makazi bora, wako kimya. Wale waliodhani ada itafutwa na serikali itachukua jukumu la kuwasomesha vijana wao, wanatokwa machozi kwa sababu fedha ambazo zingeelekezwa huko zitaelekezwa katika safari za nje, kulipa wafanya biashara walioprint tshet, kofia, kanga na skafu za CCM. Wakimaliza wataanza kukusanya fedha za kufanyia kampeni za mwaka 2015. Hapo mafisadi watakuwa hawajaanza kuchota fedha zao kwa mikataba feki waliyopewa na watakayopewa na Serikali ili mradi kila fisadi anachukua chake mapema. Wakati huo huo rasilimali zinazoisha zitaendelea kuporwa na kuwanufaisha wageni na kuwaacha wenyeji mikono mitupu. Sana sana watakaofaidika ni wale viongozi watakaowakilisha serikali katika mikataba hiyo.
Kutangazwa kwa kikwete kwa ushindi wa kupangwa na Tume (serikali) kumeleta mpasuko mkubwa nchini na si kikwete wala CCM wanaoweza kuuziba mpasuko huo. Mgawanyiko umeleta pande mbili moja ikiwa ni inayosherehekea (kimya kimya) kikwete kuwa madarakani kwa sababu watachuma kidogo kabla ya 2015 ambapo inawezekana ikawa mwisho wa Kikwete kuongoza Tanzania kama hatabadili katiba ili aendelee kwa kipindi cha tatu.
Upande wa pili ni ule uliodhulumiwa haki yao ambao unamuunga mkono Dr. Slaa kipenzi cha wanyonge. Hawa ndio walalahoi walio wengi. Hawa ni wale ambao watoto wao wanasoma shule za kata, siyo tu kwamba hawawezi kulipia watoto wao kusoma shahada ya kwanza na ya pili katika vyuo vya nje (kama Kikwete alivyofanya) bali hata vyuo vya hapa nchini hawawezi. Hawa bado wana hasira ya kuona haki yao imenyongwa. Lakini bado wana imani na busara alizo nazo Dr. Slaa na lile atakalosema ndilo watakalofuata. Hii inasababishwa na kuwa wengi katika Kundi hili ndilo linaloifanya nchi yatu ya Tanzania ishindwe kutawalika vizuri kwa sababu wana hisia mchanganyiko. Utawaona wako kimya lakini huwezi kujua wanawaza nini na hisia na maamuzi yao kukandamizwa imewauma kiasi gani.
Kuwepo kwa makundi haya mawili ndiko kunakofanya kila kundi kumheshimu yule wanayeamini ndiye Rais wao. Kundi la kwanza (serikali) lina Rais wake The president of the Government, Kikwete na kundi la pili (watu) lina Rais wao The president of the people. Kitu cha ajabu aliyeapishwa ni rais wa Serikali ambaye watu hawamuungi mkono ila anaungwa mkono na serikali na majeshi na kwa upande wa pili, Rais wa watu hakuapishwa badala yake watu ndio wameapa kuendelea kumuunga mkono kwa lolote. Je mwisho wake nini?
Ili Rais wa Serikali awe na nguvu, lazima apate msaada support kutoka kwa Rais wa watu maana hakuna serikali isiyo na watu ila kunaweza kuwepo watu bila serikali!
Peoples Power .... People Have Power ..... 4ever
Wasiliana nami kupitia: quality.chality0@gmail.com