Nchi moja marais wawili

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
NCHI MOJA MARAIS WAWILI
Hivi karibuni Tanzania imetoka katika uchaguzi mkuu wa madiwani, ubunge na Urais. Katika uchaguzi huo Tume ya Taifa ya uchaguzi(serikali) ilimtangaza Ndugu Jakaya Kikwete kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata zaidi ya 60% ya kura zote akifuatiwa na Dr Slaa aliyepata 26% kwa mujibu wa Tume. Pia katika uchaguzi huo idadi ya wabunge kutoka vyama vya upinzani iliongezeka ukilinganisha na bunge lililopita. Tayari Kikwete ameapishwa kuwa Rais
Tangu kuapishwa kwa Kikwete hakujakuwa na shamra shamra kuonesha kusherehekea ushindi kama katika chaguzi nyingine zilizopita. Wananchi mbalimbali wanasikitika na kulia sababu ya wanachoona kikiendelea. Wengi walijua na kuamini kuwa Kikwete hataweza kuendelea na kipindi cha pili cha Urais hasa kati ya sasa na 2015 kwa jinsi walivyomnyima kura lakini cha ajabu akatangazwa mshindi. Waliotarajia kununua siment kwa shilingi 5000 bila kodi ili kutengeneza makazi bora, wako kimya. Wale waliodhani ada itafutwa na serikali itachukua jukumu la kuwasomesha vijana wao, wanatokwa machozi kwa sababu fedha ambazo zingeelekezwa huko zitaelekezwa katika safari za nje, kulipa wafanya biashara walioprint tshet, kofia, kanga na skafu za CCM. Wakimaliza wataanza kukusanya fedha za kufanyia kampeni za mwaka 2015. Hapo mafisadi watakuwa hawajaanza kuchota fedha zao kwa mikataba feki waliyopewa na watakayopewa na Serikali ili mradi kila fisadi anachukua chake mapema. Wakati huo huo rasilimali zinazoisha zitaendelea kuporwa na kuwanufaisha wageni na kuwaacha wenyeji mikono mitupu. Sana sana watakaofaidika ni wale viongozi watakaowakilisha serikali katika mikataba hiyo.
Kutangazwa kwa kikwete kwa ushindi wa kupangwa na Tume (serikali) kumeleta mpasuko mkubwa nchini na si kikwete wala CCM wanaoweza kuuziba mpasuko huo. Mgawanyiko umeleta pande mbili moja ikiwa ni inayosherehekea (kimya kimya) kikwete kuwa madarakani kwa sababu watachuma kidogo kabla ya 2015 ambapo inawezekana ikawa mwisho wa Kikwete kuongoza Tanzania kama hatabadili katiba ili aendelee kwa kipindi cha tatu.
Upande wa pili ni ule uliodhulumiwa haki yao ambao unamuunga mkono Dr. Slaa kipenzi cha wanyonge. Hawa ndio walalahoi walio wengi. Hawa ni wale ambao watoto wao wanasoma shule za kata, siyo tu kwamba hawawezi kulipia watoto wao kusoma shahada ya kwanza na ya pili katika vyuo vya nje (kama Kikwete alivyofanya) bali hata vyuo vya hapa nchini hawawezi. Hawa bado wana hasira ya kuona haki yao imenyongwa. Lakini bado wana imani na busara alizo nazo Dr. Slaa na lile atakalosema ndilo watakalofuata. Hii inasababishwa na kuwa wengi katika Kundi hili ndilo linaloifanya nchi yatu ya Tanzania ishindwe kutawalika vizuri kwa sababu wana hisia mchanganyiko. Utawaona wako kimya lakini huwezi kujua wanawaza nini na hisia na maamuzi yao kukandamizwa imewauma kiasi gani.
Kuwepo kwa makundi haya mawili ndiko kunakofanya kila kundi kumheshimu yule wanayeamini ndiye Rais wao. Kundi la kwanza (serikali) lina Rais wake The president of the Government, Kikwete na kundi la pili (watu) lina Rais wao The president of the people. Kitu cha ajabu aliyeapishwa ni rais wa Serikali ambaye watu hawamuungi mkono ila anaungwa mkono na serikali na majeshi na kwa upande wa pili, Rais wa watu hakuapishwa badala yake watu ndio wameapa kuendelea kumuunga mkono kwa lolote. Je mwisho wake nini?
Ili Rais wa Serikali awe na nguvu, lazima apate msaada “support” kutoka kwa Rais wa watu maana hakuna serikali isiyo na watu ila kunaweza kuwepo watu bila serikali!
People’s Power .... People Have Power ..... 4ever
Wasiliana nami kupitia: quality.chality0@gmail.com
 
niliwahi kusema katika moja ya post zangu kuwa, kikwete atashinda kwa hila lakini utawala wake utakuwa mgumu kuliko jinsi tunavyoweza kufikilia.
 
Sijajua ni kigezo kipi hasa tunatumia kusema kwamba Kikwete hakushinda. Kiujumla hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba, kama kura zisingechakachuliwa Slaa angeshinda. Sijaona ushahidi huo. Ni dhahiri kwamba hata kama uchaguzi ungekuwa huru na haki, bila kuchakachua bado Kikwete angeshinda hata kama ni kwa tofauti ya asilimia moja na Slaa. Na hiyo ndiyo democrasia, kinachohesabiwa ni kura hata kama zitazidi mbili kati ya milioni, bado utakuwa ni ushindi.

Sasa hapo mwenye kasoro ni nani? Mimi nayaona makundi mawili: La kwanza wapinzani wenyewe ambao hawajataka kukubali kuungana, kila mmoja akiamini kwamba ndiye mwenye uwezo wa kushinda, jambo linalonifanya niwaone wengi wao kuwa ni wanafiki na si wanamageuzi wa kweli.

Kundi la pili ni la wananchi. Kama wananchi wananunulika kwa tshirt, kofia na khanga sasa kwanini wasinunuliwe. Chadema pia wangekuwa na hizo tshirt, khanga na kofia za kutosha ni dhahiri wangeshinda. Mfumo uliopo nchini sasa hivi uongozi ni pesa yako tu. Kwa hiyo safari yetu ya mapambano ianzie kwenye kubadilisha mitizamo ya wananchi hasa akina mama ambao ndiyo wengi zaidi kuliko wanaume, na ndiyo wanaojitokeza zaidi kwenda kupiga kura kuliko wanaume.

Hii ya Kikwete, kilichomponza ni kutaka tu kuongeza asilimia lakini hata asingechakachua bado angeshinda, hata Slaa anajua hilo.
 
Ndugu tunaevidence, elewa kuwa kuna maafisa usalama 400 walisambazwa nchi nzima ili kufanikisha uchakachuaji .
 
Etii hii ni nini, mbona sielewi. Huyo ni january makamba au?

Jionee mwenywe?
attachment.php
 
Unahitaji pongezi umeweza kutoa uhalisia wa hali ilivyo kiukweli,tuliyokuwa hatuyatarajii katika nchi hii sasa tunayaona yanatokea chini ya mwamvuli wa amani.Naamini kama tutaendelea hivi tutayaona mengi zaidi na ndio tutajua wale walioonja shubiri ya vurugu sio kwa ujinga wao bali waliuchoka ujinga wakakapiga moyo konde kuutokomeza.
 
Sijajua ni kigezo kipi hasa tunatumia kusema kwamba Kikwete hakushinda. Kiujumla hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba, kama kura zisingechakachuliwa Slaa angeshinda. Sijaona ushahidi huo. Ni dhahiri kwamba hata kama uchaguzi ungekuwa huru na haki, bila kuchakachua bado Kikwete angeshinda hata kama ni kwa tofauti ya asilimia moja na Slaa. Na hiyo ndiyo democrasia, kinachohesabiwa ni kura hata kama zitazidi mbili kati ya milioni, bado utakuwa ni ushindi.

Sasa hapo mwenye kasoro ni nani? Mimi nayaona makundi mawili: La kwanza wapinzani wenyewe ambao hawajataka kukubali kuungana, kila mmoja akiamini kwamba ndiye mwenye uwezo wa kushinda, jambo linalonifanya niwaone wengi wao kuwa ni wanafiki na si wanamageuzi wa kweli.

Kundi la pili ni la wananchi. Kama wananchi wananunulika kwa tshirt, kofia na khanga sasa kwanini wasinunuliwe. Chadema pia wangekuwa na hizo tshirt, khanga na kofia za kutosha ni dhahiri wangeshinda. Mfumo uliopo nchini sasa hivi uongozi ni pesa yako tu. Kwa hiyo safari yetu ya mapambano ianzie kwenye kubadilisha mitizamo ya wananchi hasa akina mama ambao ndiyo wengi zaidi kuliko wanaume, na ndiyo wanaojitokeza zaidi kwenda kupiga kura kuliko wanaume.

Hii ya Kikwete, kilichomponza ni kutaka tu kuongeza asilimia lakini hata asingechakachua bado angeshinda, hata Slaa anajua hilo.

Ndugu usibishane na mawe na wala sidhani kama kuna mtu ana muda wa kukujibu,wewe ndio umenunulika.
 
mimi mpaka kesho nawalaumu wanaume wa chadema mwanza kwa kuwazuia wake zao kupiga kura na kupunguza kura za jk!!!!!!
 
Back
Top Bottom