Nchi inapoprwa - SHIVJI

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
Shivji: Nchi inaporwa na walanguzi wanaojiita wawekezaji wa kigeni Send to a friend Thursday, 24 February 2011 21:23 0diggsdigg

Elias Msuya
PROFESA wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Issa Shivji amesema kuna wimbi kubwa la waporaji wanaohamishia uchumi wa nchi, katika nchi nyingine za nje kwa kigezo kwamba ni wawekezaji.

Akizungumza katika kongamano la Ardhi na Ulinzi wa rasilimali katika Katiba, lililoandaliwa na Asasi ya Haki Ardhi, Profesa Shivji alisema kwa miaka 50, baada ya uhuru wananchi wengi, hawana haki ya kupata ardhi badala yake wawekezaji ndiyo wameipata na wamekuwa wakiitumia kupora utajiri wa nchi.

Profesa Shivji alitoa kauli hiyo, wakati kukiwa na vuguvugu la mabadiliko ya Katiba na nchi ikikabiliwa na matatizo makubwa ya umeme na kupanda kwa bei ya vyakula mbali mbali.

“Kumekuwa na uporaji wa ardhi ya kijiji na wawekezaji-wafisadi wa ndani na nje kwa visingizio mbalimbali pamoja na bio-fuels na ulimaji wa mazao ya chakula kwa ajili ya masoko ya kimataifa. Utakuta matajiri wanatoka Dubai wanakuja kupora ardhi na kuhamishia utajiri wote kwao,” alisema Profesa Shivji.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Shivji alisema maisha yamekuwa magumu, bei za vyakula, zimepanda kwa sababu wananchi hawana nafasi tena ya kuzalisha.

Akitoa mfano, Shivji alisema katika Jiji la Dar es Salaam licha ya kuwa na majengo mengi marefu, asilimia 70 ya wakazi wake wanaishi katika makazi yasiyo rasmi na kufafanua kwamba walanguzi wamepora maeneo ya wananchi na kujenga, maghorofa na wananchi kukosa maeneo ya kuishi.


Alishauri wananchi washirikishwe katika kujadili mfumo mpya wa Katiba utakaotoa fursa kwa wananchi, ili wawe na nguvu ya kumiliki ardhi na rasilimali zao.

Alisema Katiba ya sasa, haisemi lolote kuhusu ardhi badala yake imegusia haki ya wananchi kumiliki ardhi, na kusababisha utata kuhusu umilikaji wa ardhi.

Naye Odenda Lumumba wa Chama cha Watetezi wa ardhi wa Kenya alitoa uzoefu wa suala la ardhi na jinsi lilivyoingizwa kwenye mabadiliko ya Katiba mpya nchini humo, akisema kuwa walianza mijadala kwa muda mrefu na baadaye, walifanikiwa.

“Tuliandaa mapendekezo yetu na tukayapeleka kwenye mchakato wa Katiba, tunashukuru asilimia 90 ya mapendekezo yetu yamepitishwa,” alisema Lumumba.
 
ni hatari sana namna hii. nchi imeshauzwa hii. serikali ya ccm imejawa na ubinafsi wa hali ya juu. hawajali maslahi ya watu maskini ambao ni over 98% ya watanzania...the other 2% ndiyo watawala waliojilimbikizia mali na kuamua kula keki ya taifa na mafisadi na mabeberu wa nje.
 
Nchi yetu wenyewe, tunakubali kuwa watumwa katika nchi yetu kwa kutunga sheria na kuchukua maamuzi wenyewe kupitia wawakilishi wetu wajinga na walafi(kama chief mangungo), au waliolewa madaraka!
 
UBEPARI MALAYA NDIO UNAOTUKOST
daima tutateseka na ccm tubadilishe chama tuone
 
Tubadilishe chama tuone

ukiona mtu anakataa wazo la kubadilisha cha cha si sisi em ujue huyo fisadi au anakula na mafisadi

si sisi em ndo imetufikisha hapa

nguvu ya umma inakuja!
 
UBEPARI MALAYA NDIO UNAOTUKOST
daima tutateseka na ccm tubadilishe chama tuone

tena umalaya wa kijinga, kugawa rasilimali za nchi bure kwa VISA za bure kwa rais na kundi lake kwenda ulaya na marekani wakati wowote wanapotaka.

It is time watz we must take charge of our our destiny, CCM....is leading us to hell.
 
Maandamano yameanza Mwanza sasa yasiishie hapo yaendelee nchi nzima
 
Wananchi wa Dar-es-salaam wanafiki sana hawana uwezo wa kufanya ujasiri walioonyesha wasukuma wakurya na wahaya jana.Kule lake zone Neno CCM limeanza kusahaulika, makada wa CCM ndiyo wanatoa siri za chama chao na wao wanadai ni chama cha watu wa pwani.
 
Back
Top Bottom