Nchi inaongozwa na CCM, kwanini wanalaumiwa CHADEMA?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,042
33,527
Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya kwenye mambo mbali mbali, nimegundua kwamba CHADEMA imekuwa ikilaumiwa mara nyingi kwamba haitimizi wajibu wake hadi mambo yanaharibika. Kwamfano;

Wakati wa Bunge la katiba CHADEMA iliongoza vyama vingine kutoka kwenye vikao vilivyokuwa vinaendelea vya Bunge la Katiba kupinga jinsi Bunge hilo lilivyokuwa linaendeshwa.

Na mchakato wa kupata Katiba mpya ukaishia hapo. Lakini wabunge waliobakia walikuwa wengi na walipitisha Katiba Pendekezwa. Kwa nini mchakato wa kupiga kura ya maoni ili kuipitisha hiyo Katiba ulifutiliwa mbali?

Huo ni mfano mmoja tu, lakini ukiangalia hata ile marufuku ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ililengwa CHADEMA. Hoja iliyotolewa wakati ule na hata sasa ni kwamba mikutano hiyo inazuia watu wasifanye kazi.

Nchi hii inaongozwa na CCM, ni kwa nini basi kila lawama ya kukwama kwa mambo wanatupiwa CHADEMA? Au CCM wanaona wanaostahili kuongoza nchi yetu ni CHADEMA?
 
JamiiForums753274111.jpg
 
Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya kwenye mambo mbali mbali, nimegundua kwamba CHADEMA imekuwa ikiliaumiwa mara nyingi kwamba haitimizi wajibu wake hadi mambo yanaharibika. Kwamfano;

Wakati wa Bunge la katiba CHADEMA iliongoza vyama vingine kutoka kwenye vikao vilivyokuwa vinaendelea vya Bunge la Katiba kupinga jinsi Bunge hilo lilivyokuwa linaendeshwa.

Na mchakato wa kupata Katiba mpya ukaishia hapo. Lakini wabunge waliobakia walikuwa wengi na walipitisha Katiba Pendekezwa. Kwa nini mchakato wa kupiga kura ya maoni ili kuipitisha hiyo Katiba ulifutiliwa mbali?

Huo ni mfano mmoja tu, lakini ukiangalia hata ile marufuku ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ililengwa CHADEMA. Hoja iliyotolewa wakati ule na hata sasa ni kwamba mikutano hiyo inazuia watu wasifanye kazi.

Nchi hii inaongozwa na CCM, ni kwa nini basi kila lawama ya kukwama kwa mambo wanatupiwa CHADEMA? Au CCM wanaona wanaostahili kuongoza nchi yetu ni CHADEMA?
Hiyo ndo kaz kubwa ya Johhthebaptist humu!!
 
Hiyo ndo kaz kubwa ya Johhthebaptist humu!!
Yule na wenzake hana shida za Maisha. johnthebaptist anakula anachotaka na siyo kinachopatikana na akitaka kwenda Ulaya au kwingineko hata mara tatu kwa mwaka, anaweza. Ana mafao ya kuendelea mpaka afe.

Humu anakuja kuonesha tu hasira zake dhidi ya CHADEMA na shukrani zake kwa CCM kwa kumwezesha kuishi maisha ya anasa mpaka uzeeni. Siyo kijana mdogo kama wengi wanavyofikiri.

Jana alikuwa analalamikia mambo ya Kawe. Jiulize Jimbo la kawe maeneo yake ni yepi.
 
Nimesoma mara ya kwanza sijaelewa, nikarudia mara ya pili sijaelewa, nikarudia mara ya tatu Ila bado. Wenzetu hamna akili?
 
Nimesoma mara ya kwanza sijaelewa, nikarudia mara ya pili sijaelewa, nikarudia mara ya tatu Ila bado. Wenzetu hamna akili?
Tatizo ni wewe uliyesoma bila ya kuelewa... Ukiona unasoma kitu na huelewi basi tatizo ni akili za wewe msomaji na wala siyo mwandishi.
 
Kwa kuwa ni vibaraka wa mabeberu, mafisadi, majangiri na wauza madawa ya kulevya.
Nakumbuka Kipindi Mbowe anasema chanjo iletwe mlisema anatumika na mabeberu, kaingia Samia kuanzia bunge mpaka mawaziri na serikali kwa ujumla Waka support Hilo suala tena ilifika hatua waliopinga chanjo wakasimamishwa teuzi!!

Kwahiyo zile lawama za CHADEMA kwenye chanjo zilikua na faida Gani kama Wana CCM na nyie mmesupport?? Au tukubaliane CCM inatumika na mabeberu?
 
Back
Top Bottom