Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
Mkuu, kwa wataalam wa saikolojia, mtu anapokuwa katika maruwe ruwe kuna nyakati husema yanayoonekana kama maruwe ruwe, ukweli ni kuwa anachosema ndicho alicho nacho moyoni.
Ni maruwe ruwe'delirium' ndiyo humusukama kusema bila kukusudia
Baada ya kufanikiwa kumtengeneza mfalme,mzee alijisahau au alijivika kofi ya ubaba wa Taifa.
Akawekeza sana , mwisho wa siku tunajua yaliyomkuta. Hapa namnukuu JK akisema 'naomba yaliyomkuta mzee X yasije yakanikuta''
Mzee alikuwa ndani ya 'Kitengo' tulichokuwa hatukijui hadi alipoapatwa na mkasa.
Hivi leo analalamikaje, ikiwa sisi wananchi wenye nchi hatukujua kitengo isipokuwa yeye na wana kitengo? Thanks to CCM
Kuhusu hoja zako
Kwanza, mzee anatueleza hatuna demokrasia. Hata hivyo, hatuwezi kukaa tukilalamika bila kufanya jambo.
Oktoba 25 tubadili mwenendo ili tuwape watu wa nje nafasi ya kutueleza kitengo kinafanyaje kazi
Pili, ninashangaa usalama wa taifa wanaingia katika kitengo cha CCM. Hapa napo pana jambo
Tatu, tume ya uchaguzi ni sehemu ya 'kitengo' nikupe mfano. CCM waliosema kura ya maoni ipo, tume ikashikilia msimamo huo.
CCM wakasema kura ya maoni ni pamoja na uchaguzi, tume ikashikilia msimamo.
CCM wakasema wameagiza BVR na kazi itamalizika kwa wakati, tume wakasema hayo.
Rais akarudia kule Washington kuwa kura ya maoni ipo pale pale, mwenyekiti wa tume akarudia maneno hayo hayo.
CCM wakasema wameshauri serikali iharishe kura yao ya maoni, tume wakasema nao wanaahirisha.
Yaani tume iliyopaswa kuongozwa kitaalumu, imekuwa inapokea maagizo ya ''kitengo''
Ndiyo maana tunasema, kama tutalalamika bila kuleta mabadiliko, 2020 tutakuwa hapa tunazungumzia hicho hicho
Tatu,kitengo kinaendeshwa na nani? Hapa mzee atusaidie maana hatukujua uwepo wa kitengo
Nne,Watu wangapi wanafanya maamuzi? Mzee anajua kitengo kimeundwaje na kina watu wangapi
Tano,maamuzi ya kitengo ni ya kitengo, na huwa ya kitaifa kupitia vyombo husika.
Kimoja ni hicho tulichoambiwa, kingine ni Bunge. Hivi watu hawajui mswada wa gesi na mafuta ni kazi ya kitengo?
Uliletwa haraka na serikali, ukapigwa mhuri haraka haraka na bunge ili watu waende kwenye kampeni, tumeondoa mafuta na gesi tupeni kura wazanzibar. Hili nalo linajibu hoja ya maamuzi kwa manufaa ya taifa
Sita,kuna fiada gani kushiriki uchaguzi? Tukikaa pembeni kitengo kinaimarika.
Tumekaa miaka 50 na kitengo, hatuwezi kuendelea kukaa mingine 50 tukisubiri kitengo kitatuhurumia.
Lazima lifanyike jambo, kazi hiyo ipo kwetu na si kwa kitengo. Oktoba 25 tukiendelea na ugonjwa wa kusahau, hewalaa!
Mwisho mzee wetu kasoma Urusi. Anajua vema falasafa za vanguard party na Polituburo.
Sina uhakika nani ameanzisha kitengo, ninachojua kitengo ni mfumo uliopo unaondeana na anachokieleza mzee