Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,960
- 11,221
Miaka kama mitatu iliyopita nilikuwa kwenye Hotel moja hapa mjini na ndugu yangu mmoja.. Tulikuwa tuko counter tunapata kinywaji. Wakati tunaangalia Habari, tukaona Kingunge akiongelea mambo flani nyeti sana ya nchini. Tukawa tunamjadili Mzee Kingunge na ndugu yangu pale kwa muda mrefu, kwanini aendelee kukomaa na mambo ya siasa wakati umri ushamtupa mkono. Kwanini asipumzike kama wazee wenzake?? na kwanini JK amteua yule kizee wakati kuja vijana na watu wa makamo wengi sana wenye ujuzi mkubwa wa siasa za kisasa. Pembeni yetu kulikuwa na Mzee mmoja akifuatilia maongezi yetu kwa muda mrefu.. Yule mzee aliongea kitu kimoja tu, "Vijana Hivi mnafikiri hii nchi inaendashwa na JK au Mnafikiri viongozi wakuu wa hii nchi wanachaguliwa na wananchi??" tukabaki tunashangaa, Yule mzee akacheka kidogo then hakuongea tena akaendelea na mambo yake..
Last year nikaja kumwona yule Mzee kwenye sherehe flani zilizofanyika Ikulu akiwa nearly na JK.. Zilirushwa na TBC.. Hapo ndipo nayatafakari yale maneno ya yule Mzee mpaka leo hii
Nchi yeyote duniani usalama wa taifa ukikaa mbali na siasa basi na amani yake na mshikamano wake utakuwa wa bahati nasibu na upo kama time bomb tu.
Usalama wa taifa lazima uingie kwenye vyama vyote vya siasa duniani no one expected Ed Milliband to win kwa sababu waingereza na wa-Marekani are not ready for someone with Jewish background na kulikuwa na mizwengwe mikubwa sana kuhakikisha kaka yake mwenye support ya watu wenye nguvu ashindi uchaguzi wa ndano.
Tofauti ni kwamba wako very sophisticated in their arrangement and disguising their operation inatakiwa uwe makini sana kuona jinsi wanavyoweza badilisha upepo kupitia makachori wao waandishi wa habari na jinsi wanavyoweza badilisha mgombea ndani ya chama kama anakosa sifa sahihi za muda huo na ataa kuamua chama gani kinashinda kubalance social interest kisera.
Kwa mtazamo tu hakuna mtu anae kiujumu CDM isipokuwa hawana sifa za kukubalika kwa sasa hivi watu wanaoenda kufanya campaign kanisani kwa Gwajima au wanaotegemea support za kanisa kutaka kuvunja muungamo uwape nchi kweli huo utakuwa uwandawazimu na watakuwa awafanyi kazi yao ya usalama vizuri.
Usalama na siasa ni damu damu isipokuwa hawa jamaa wetu wanapwaya sana wakati mwingine kimbinu na kuinyoosha serikari ya CCM and are very poor at propaganda labda kuna watu nao washazoea kufaidika personal na mfumo wa uzembe uliopo sasa ndio maana kuna vitu vya kijinga sana na ufisadi wa kishamba unao fumbiwa macho.
Lazima kuna watu wanafaidika walio responsible na ndio wanao haribu siasa zetu (mfano Apson) na kutokuwa na safu zenye uelewa wakujenga utamaduni wa chama.Ufisadi wa kutia aibu kabisa
The Boss ila inabidi tuwashukuru sana hata hivyo. Nchi yetu bado haijakaa sawa kuwaachia wanasiasa wafanye watakavyo. Kwa hiyo ushiriki wao hasa kwa chama ambacho bado kina nguvu sana kwenye dola ni muhimu.Kitengo kikiacha hii kazi tutanyukana muda si mrefu. Wanajua wanachofanya na wanakifanya kwa manufaa ya nchi na si kwa CCM. Tuwapongeze na tuache kuwatifua tifua. Wanopana mengi ambayo hatuoni. Mfano Mzee Mkapa alivyowaambia Wa NEC kwamba Kikwete anafahamu mengi kulio WANEC. Pia Mzee Karume alisema kwamba kuna mambo yakiwekwa hadharani watu wataishia kudhalilika. Ndo maana Lowassa yupo Kimya. Ila wafuasi wake wenye ufahamu mdogo ndo wanapiga kelele.
Ndo wazee wa 'kitengo' hao
Moja ya majukumu ya usalama wa taifa ni kuilinda presidential institute. Kwa hiyo wanakuwa wanahusika kwenye hiyo nafasi nyeti. Hawana Mandate ya kupambana na mafisadi. Ila wana uwezo wa kuilinda taasisi kuhakikisha haiendeshwi na mtu ambaye uadilifu wake una walakini.Kwanini wasubiri hadi uteuzi wa Rais ndo washiriki?
why wasizuie mafisadi wote before?
au kushinikiza wafungwe jela?
Unless kuna mapinduzi, hiyo ni standard practice dunia nzima.The Boss Hata mimi nilishangazwa katika hiki kipindi cha demokrasia ya vyama vingi eti Usalama wa taifa wanaingia kwenye vikao vya ccm kumchambua mgombea atakayepeperusha bendera ya ccm.
Kama taifa bado kazi tunayo. Naamini mwaka huu 2015 wa uchaguzi, hautokuwa wa haki kama ulivyokuwa wa 2010
Naelewa sana ndo maana nakupa pole wewe uliye kwenye giza mkuu.Poleni kina nani
wewe sio mwananchi?
faida ya 'kitengo' we unaipata?
Wananchi ndo wanaoipigia CCM. Kwa hiyo wa kuwalaumu ni wananchi na si usalama wa Taifa. Kama wewe hapa unalalamika inaonyesha tayari unaamini Upinzani umeshindwa uchaguzi mkuu. CCM kama Chama lazima kifanye mbinu zote kiendelee kutawala. Wapinzani nao wanatakiwa wafanye mbinu zote waingie madarakani.As long wananchi hawana sauti katika nchi yao
tunashindwa hata na vinchi vidogo kama Malawi wanabadili vyama na marais
pole ni kwa Watanzania wote
Kuna vitu vinajitokeza kipindi hiki cha uchaguzi
ambavyo vinapaswa kuulizwa
je nikweli wananchi wa Tanzania ndio wasemaji wa mwisho wa masuala ya nchi hii?
au kuna watu kwa aakili zao na utashi wao wamejipa 'jukumu' hilo?
Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
Hebu fikiria kama CIA au M16 kama wangekuwa wanafanya siasa kwenye taasisi zao hizo nchi zao zingekuweje? Leo hii hapa kwetu Tanzania wageni wanakuja kuiba mchana kweupe wanachukuwa wanyama huko kwenye mbuga zetu na kuwapakiza kwenye ndege, madini yetu yanaibiwa kila siku na vijidege vidogodogo vinavyotuwa kwenye migodi.
Eti usalama wa taifa wapo busy kwenye ofisi za ccm kuhakikisha ccm haitoki madarakani. Usalama wa taifa unatumikia CCM badala ya taifa na rasilimali zake. This is shamefully and disgusting to us Tanzanian. Politics is everywhere, this is too dangerous to our nation playing politics in serious matter
Mkuu siasa hutaziweza kabisa..Kuna vitu vinajitokeza kipindi hiki cha uchaguzi
ambavyo vinapaswa kuulizwa
je nikweli wananchi wa Tanzania ndio wasemaji wa mwisho wa masuala ya nchi hii?
au kuna watu kwa aakili zao na utashi wao wamejipa 'jukumu' hilo?
Kingunge alisema 'KITENGO' ndio kiliamua nani awe mgombea wa CCM na sio
wanachama......na Ukisoma gazeti la Raia Mwema wanasema watu wa 'usalama'
walimwambia Ngeleja awaambie wazanzibar kumchagua 'mgombea wa kitengo'
ndio akashinda....maswali yanajitokeza
1.kitengo kinaendeshwa na nani hasa?
2.Ni watu wangapi wanaofanya hayo maamuzi?
3.Ni kweli maamuzi yao yote ni kwa faidaya Taifa?
4.Wananchi wakipishana maamuzi na 'kitengo' maamuzi ya wananchi yataheshimiwa?
5.Nguvu ya 'kitengo' kwa tume ya uchaguzi ni halali?
6.kuna faida ya kushiriki uchaguzi huku 'kitengo' kimeshafanya maamuzi?
7.Je tuna demokrasia kweli au tunaruka ruka ttu na maigizo?
Uelewa wako unatia shakaMkuu siasa hutaziweza kabisa..
Dunia nzima KITENGO ni sehemu muhimu sana ya uchaguzi wa marais wake, hizi habari za Demokrasia ni kupigwa changa la macho tu. Hakuna nchi yenye demiokrasia ya kweli hapa duniani pasipo kulinda maslahi ya nchi husika.
Maadam Lowassa ameonekana ni hatari kwa Usalama wa Taifa akitaka Urais kwa kuunda Cartel inatosha kwako wewe na mtu mwingine yeyote mwenye akili kamili kutomzungumzia kabisa mtu huyu. Bahati yake baba wa Taifa Nyerere hatunaye, huyu Jambazi sijui gaidi angefungiwa kwao Monduli akapewa kifungo cha ndani asitoke akae huko huko hadi kifo kimkute.
Faida ya kushiriki uchaguzi ipo kubwa sana ikiwa wagombea wote wapo kwa interest za nchi na sio kununuliwa. Urais haununuliwi wala kufadhiliwa, hotuba ya Mwalimu Nyerere alitosha kabisa kwenu kujifunza siasa za nchi..
Maadam umetumia maneno ya Kingunge na hoja yake sisi tulomuelewa tunajua una maana gani. Pengine ungetumia mfano mwingine kabisa lakini hii issue ni nzito kuliko unavyoifikiria wewe.Uelewa wako unatia shaka
we umeona namzungumza Lowasa hapo?
umeshindwa kabisa kuelewa nilichoandika?
so sad
Maadam umetumia maneno ya Kingunge na hoja yake sisi tulomuelewa tunajua una maana gani. Pengine ungetumia mfano mwingine kabisa lakini hii issue ni nzito kuliko unavyoifikiria wewe.
haha..hiyo ndio habari..Hujajiuliza ZZK kwanini kaingi aktk deadlock Sasa hivi habari ya mujini ni Lowasa, CCM kitu ya cdm hailipi km kumthibiti EL...wakati ACT wanabipu kuchukua wabunge na sijui nani CDM wanapiga CDM km wamepewa airtime bure.Hata wewe zile threads zako na kinyumenyume nadhani sasa hivi hazina tena maana..Sasa umebaki na kingunge..kingunge hana cha kupoteza na anaonekana ana akili kuliko ccm pamoja na uzee wake.CCM walichemka kumkata Lowasa,mbaya walimkata ktk level ambayo iliwadhalilisha hadi akina Pinda na wnegine ambao CCM inawahitaji.Hiyo ndio democrasia.Maadam umetumia maneno ya Kingunge na hoja yake sisi tulomuelewa tunajua una maana gani. Pengine ungetumia mfano mwingine kabisa lakini hii issue ni nzito kuliko unavyoifikiria wewe.