Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,029
- 63,169
- Thread starter
-
- #161
Inawezekana kabisa hukujua ni kwa kiasi gani ufisadi ulikuwa unaendesha uchumi; hivi mnafikiri tulikuwa tunapinga ufisadi ili ili kila mtu aishi tu kwa raha.. au mlidhani ukiushambulia ufisadi nini kitatokea. Tanzania haijafika mahali bado kabisa pa kuweza kuwa pepo ya wengi... ufisadi uliharibu siyo tu watu wa serikali; uliathiri hadi wakulima na watoto ambao hawajazaliwa bado. Madhara ya ufisadi yalikuwa ni mapana mno na hata sasa bado hazijachukuliwa hatua zote sahihi na stahiki kusahihisha mfumo wetu. Kwamba hali ni ngumu ili lilitarajiwa.
Tumeshuhudia ufisadi katika chaguzi za marudio na kununua wapinzani, serikali ya chama kinachonunuanunua wapinzani kwa vihela hivi kinatumiatumia hakiwezi kuwa serious kwenye kupambana na ufisadi.
Mwakajana nilipanga 2019 nitachukua Gari ya mjerumani niachane na mjapani, lkn nashangaa mwaka unaingia nabadilisha mjapani mwingine mdogo zaidi....
Kibaya zaidi nawaza hata huyu nimuuze ninunue pikipiki, mana pesa zinatoka wala haziingii....
Kuna kapesa hapa kila biashara ninayoifikiria naona itaenda potea tu bureeee....
Mpango wangu wa mwisho km hali itabakia hv, 2020 December nitasepa Majuu nikapige kitabu niachane na tz kabisaa.....
Sent using Jamii Forums mobile app
Akuu,...
Na hii ni Dar, Jiji kubwa vipi huko mikoani?
Kubana matumizi ni umasikini.....Unaona sasa umeanza kufikiria eh... zamani ulihitaji kufikiri hivyo? sasa watu wanapanga na kuchagua; na kubana matumizi si umaskini..
Hao wapinzani wanaonunulika kirahisi hivyo walikuwa kweli wapinzani? Na upinzani ulikufa lini Tanzania? Wewe juzi kafungwa malkia wa ujangili... unadhani dogo lile; unajua ni kwa kiasi gani alikuwa anafanya kazi with impunity? Kina Rugemalira na Singasinga wako wapi hadi leo? Na kesi bado zinaendelea... udhaifu mkubwa ni kuwa bado hatujawa na utaratibu mzuri wa kuleta mashtaka na kuwatia watu ndani... hili ni udhaifu mkubwa.. lakini believe me.. wanaoguswa sasa hawakuwahi kuguswa huko nyuma...
😌😌😌
Rugemalira na Seth, ile ripoti iliwataja wengi mno hadi mawaziri wa wakati huo, mwanasheria mkuu wa zamani etc
Ripoti ya makinikia pia iliwataja vigogo wa zamani wa serikali
Hao wako uraiani wanapeta kwa nini?
Unakamata majambazi wawili watatu ila Unawaacha wengine 50 halafu unajaribu kuonyesha kuwa uko serious?
Hakuna userious wowote wa kupiga vita ufisadi hapo!
Si kweli; kubana matumizi si umaskini ni akili za kibiashara; wakati mwingine unabana hapa ili ufanikiwe kule.. usidhani utajiri ni kutapanya; kwamba unatumia hela bila kufikiria hali ya kiuchumi au ya kibiashara. Huwezi kufanikiwa kibiashara kama kila hela inayoingia unaitumia na unatumia hela bila kujali inavyoingia! Hapo ndio kukaribisha umaskini; sasa hivi unaanza kuwa na akili za kufanikiwa.. ulikuwa na ulazima wa kubadilisha gari toka moja hadi jingine au ulitaka na wewe uonekane tu kuwa una gari la kisasa?Kubana matumizi ni umasikini.....
Kubana kwangu matumizi kumeathiri biashara nyingine...
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni kweli kabisa...Miaka mitano iliyo pita huku Mbeya ulikuwa ukinunua chips za buku mpaka muuzaji anakuuliza mpo wangapi? Maana alikuwa Ana uhakika huta maliza. Ukisema upo mwenyewe atakushauri uchukue za jero. Lakini sasa hivi chips za buku unaweza ukamkunja muuzaji ukadhani amekutapeli hela yako kwa kukupa vipunje kidogo vya viazi[emoji2]
Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ndo uzalendo mnaujua!! Uzumbukuku wa kutotumia fikra na akil Mungu alizotujaria. Badirikawanaoshindwa kufanya biashara ni wale wanaofanya waliokuwa wakifanya biashara kiujanja ujanja kwa kukwepa kodi, nikiwa kama mwananchi mwema sijutii kuwapoteza wafanyabiasha wasio na faida kwa taifa langu.
Sasa haya magoli! Kila mtu anakamatwa kutokana na ushahidi uliopo na ambao unaweza kuufungulia mashtaka. Na ndio maana unaambiwa wakati mwingine "upelelezi unaendelea". Upelelezi unapotosha watu wanatiwa pingu. Sasa unataka watu wakamatwe tu bila kuwa na ushahidi wowote wa kuweza kusimama mahakamani si ndio watu watalia "udikteta"! Huwezi tu kukamata watu kwa sababu wametajwa; unakamata watu kwa sababu ya uzito wa ushahidi dhidi yao.
Ina maana ripoti kama ile ya Makinikia, iliyosheheni taarifa za kitafiti, iliyoelezea kula mhusika kahusikaje katika conspiracy ya kuuza kuingia mikataba mibovu haitoshi kuwa reference katika mkono wa sheria?
Basi haikuwa sahihi kutaja majina ya watu kama hakuna ushahidi wa kutosha dhidi yao!.
Nchi hii ukiniambia kuwa Ufisadi ulikuwa ni Seth, Rugemalira na Malkia wa meno ya tembo peke yao nakuona kuwa umeamua kuwa Spin doctor tu.
Katika nchi hii kubwa namna hii na kwa kiwango cha Ufisadi mliotuaminisha haiwezekani mafisadi wakawa watu watatu tu, certainly hawewezi kuwa watu 20 peke yao!.
Na kama kwa miaka Mitatu kwenda minne ya kukaa madarakani uchunguzi wako umeishia Kuwajua Watu wawili watatu kuwa ndiyo Mafisadi basi inaonekana kuwa Huuchimbui Ufisadi vya kutosha na kwa hiyo hoja yako kuwa unapambana na ufisadi ni Muflisi
Kubana matumizi ni umaskini?! No wonder biashara zinakushinda (Kwa mujibu wako)Kubana matumizi ni umasikini.....
Kubana kwangu matumizi kumeathiri biashara nyingine...
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimepita katika mitaa kadhaa ya jiji la dar es salaam.
Nilichokiona kinasikitisha, Mitaa michafu, watu wamekondeana, fremu zimefungwa na zilizofunguliwa wateja ni wa kuhesabu.
Ukizunguuka ukaenda kwa wauza chipsi mafuta wameyachomea chipsi wameyarudia hata mara tano yamekuwa meusi tiii, wanakwambia brother hali ni ngumu hatuwezi kumwaga yale tuliyokwisha tumia.
Ukienda kwa mama ntilie, unawaona jinsi watu wanavyohustle, vijana wanawakopa, hela ya kula ngumu na wanakwambia wanakula mlo mmoja kwa siku.
Siku hizi kuangalia TV majumbani imeshakuwa anasa, hela ya king'amuzi kila mwezi mtihani!
Hali ni ngumu kitaa, hali ni mbaya sana. Nchi imekauka kaukau
Hivi viongozi wa serikali wanalijua hili?. Hivi wako aware na hali ya kiuchumi ya wananchi wao?
Serikali ilijue hili kuwa hali ni mbaya mtaani, data na Takwimu za makusanyo na kukua kwa uchumi hazitusaidii sisi wananchi, matangazo yenu hayajatranslate kwenye hali halisi huku kitaa!
Na hii ni Dar, Jiji kubwa vipi huko mikoani?