Nchi hii inapoteza uelekeo, wasomi mko wapi?

mtaala wa chuo kikuu ulishabadilika kitambo... Kama unabisha ni aina ya wanafunzi wanaotoka kutoka katika vyuo , vyuo vyote , kutokana na mfumo uliopo ni assemby line au mass production au voda fasta tu.

Usitegemee watatoa msimamo na ukisikia wametoa msimamo fulani, chunguza kuna rupia imepenyezwa mahali fulani:flame:

Cjawahi kumwamini msomi mzaliwa wa africa na anaeendesha shughuli zake africa. Namwamini sana kijana kidato cha 4 mwingereza wa birmingham kuliko profesa wa dar. Nina mifano mingi sana lkn tazama mfano huu.
Profesa wa sheria au wa uchumi kawekeza ktk daladala za mbagala kariakoo na muuza ubuyu kawekeza ktk rout hiyo hiyo na biashara km hiyo. Wote jioni wanasubiri hesabu ya sh 100,000. Hapa kwa tafsiri ya haraka msomi ni muuza ubuyu.
Jingine dogo na kawaida ni msomi mwajiriwa, kafunga tai, mkononi ana ipad au smartphone kubwa halafu anamkopa mangi dukani mwezi mzima. Halafu mangi mwenye duka ni class 7 na haishi kwa mkopo. Je hapo msomi nani...so wasomi wetu hadi karne ijayo ndo nitajaribu kuwasikiliza
 
Nimesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari mbalimbali kuwa kuna wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar-es- salaam wameelani vikali kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA, shida yangu haipo kwenye wao kulaani hiyo kauli maana mimi sio mshabiki wa vyama vya siasa ila shida yangu iko kwa wasomi hawa wasioweza kutafuta 'solution' ya matatizo yanayoikumba nchi yao na wakiwa wamenyamaza kimya kwenye mambo ya msingi yahusuyo nchi, utawasikia tu 'boom' likiwa limechelewa au kujibu/kulaani kauli za wanasiasa!

Kuna fedha za 'account' ya escrow inayohusiana na tanesco wao hiyo kwao sio muhimu, hizi fedha zinazotafunwa bungeni bila kupata katiba woa hawatafuti 'solution' ya kuepusha fedha hizo zisitafunwe bali wanakaa kudandia hoja za wanasiasa, hii nchi kama inatengeneza wahitimu wa vyuo vikuu wa staili hii basi tujiandae kutawaliwa na 'vichaa' wasioweza kubuni na kutatua vitu vya msingi bali kudandia hoja na na kwenda na matukio!

wanafunzi jipangeni, hamuutendei haki ubongo wenu, elimu yenu, nchi yenu bali mnataka umaarufu wa kipumbavu!

Kwan kaka hulijui hili? 78% ya watanzania IQ zao ni kiwango cha chini! Nchi ipo best top ten ktk orodha ya nchi duniani ambazo watu wake IQ Zao ni ndogo! Aseh majanga kwelikweli! Wanajiita wasomi!
 
Mabadiliko Mengi Duniani Yanaletwa Na Nguvu Ya Umma

Wanaharakati Lakini Mabadiliko Matakatifu Bila Rabsha Yanaletwa Na Wasomi Hivi Kwanini Hawa Wa Kwetu Wamepooza Hivi?
Hivi Nini Kimempata Shivji Hata Kubadili Msimamo Wa Kutetea Taifa Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Wakiandamana Ni Kwaajili Ya Mikopo Hawajawahi Kutoka Kutetea Taifa
Fedha Yetu Imekufa,wabunge Wanatumia Kodi Zetu Kujadili Bajeti Hewa. Hivi Nani Wakuwatetea Hawa Wananchi Wa Tandahimba Na Namtumbo Wasomi Wetu Semeni Serikali Hii IMECHOKAA
 
Wasomi wa tanzania nawadharau sana kwa sababu wao ndo mtaji mkubwa wa kutumiwa na ccm
 
Kutegemea wasomi waliojaa kwenye siasa walete mabadiliko ni sawa na sista du kuivulia nguo saa akitegemea muda utasimama.

Au una maanisha mabadiliko hasi?

Play your part.
 
Wasomi wa TANZANIA wana laana ya usaliti kwakuwa na wao wanashiriki katika harakati za kumkandamiza mwananchi...hawapo tena harakati za kuikomboa jamii au kuifunua fikra jamii...wamegeuka kuwa wachumia tumbo na vibaraka wa wanasiasa....njaa walizoziweka mbele zimewafanya wajidhalilishe mbele ya mabwana wakubwa.....kodi zetu zilizotumika kuwasomesha ndio zimekuwa kaburi letu....kwani zimekwenda kinyume na matarajio.....wanalazimika kuishi maisha ya kinafki ili mkono uende kinywani....na wengine wameshakimbilia kwenye siasa wanakokula posho lukuki za vikao visivyo na kichwa wala miguu......hawapo tena vyuoni kugawa maarifa kwa watoto wetu au vijana wetu...wamekimbilia kwenye ULAJI....
 
Mpaka wabongo mtakapoacha uboya wa kulalamika lalamika na kusingizia nani na nani ndio chanzo cha matatizo bila kuchukua hatua mtakatwa mpaka basi
 
Mabadiliko Mengi Duniani Yanaletwa Na Nguvu Ya Umma

Wanaharakati Lakini Mabadiliko Matakatifu Bila Rabsha Yanaletwa Na Wasomi Hivi Kwanini Hawa Wa Kwetu Wamepooza Hivi?
Hivi Nini Kimempata Shivji Hata Kubadili Msimamo Wa Kutetea Taifa Wanafunzi Wa Vyuo Vikuu Wakiandamana Ni Kwaajili Ya Mikopo Hawajawahi Kutoka Kutetea Taifa
Fedha Yetu Imekufa,wabunge Wanatumia Kodi Zetu Kujadili Bajeti Hewa. Hivi Nani Wakuwatetea Hawa Wananchi Wa Tandahimba Na Namtumbo Wasomi Wetu Semeni Serikali Hii IMECHOKAA

kwa kifupi jua tu kila mtu anawaza kupiga hela au kupiga dili sasa linapokuja swala la nguvu ya umma wale wenye shida sanaaa ndo watajitokeza na wenue mawazo hasi kuwa wao wanacho watabaki barabarani na vijigari vyao vya mkopo...kwa hiyo itakuwa ni -1+1=0
 
kwa maana nyingine ni kuwa wameridhika na elimu zao walisoma ili kupig hela siyo kulisaidia taifa kuondokana na umaskini
 
Tatizo ni mind set ya watawala, wasomi na common wananchi.....
Kama kuna kitu serikali ya "Kidumu Chama Kilichotoboka" imefanikiwa ni kudhalilisha taaluma (professionalism).
Watawala wamefanikiwa kuwachonganisha wasomi na common wananchi kiasi kwamba jamii ya common wananchi inawachukulia wasomi kama wapiga kelele (mavuvuzela) tu. Kuna maeneo mengi tu wasomi hawaaminiki tena...Kama unadhani degrii yako itakubeba kushinda uchaguzi mwaka huu jitose uone.....Kwenye kura za maoni tu utagalagazwa vibaya sana na mwenzako mwenye fedha ambaye elimu yake mwisho ni kuandika jina lake...

Tupo katika nchi ambayo msomi mwenye madigrii ya uhandisi pamoja na kusomeshwa kwa fedha nyingi ndani na nje ya nchi hajawahi kushirikishwa na serikali kwenye shughuli yoyote ya maana!!

Serikali inawafurahia zaidi walimu wa primary schools...hawa ndo wataalamu wanaoshiriki kwenye shughuli kadhaa za utendaji... Uchaguzi, Sensa, Chanjo, tafiti mbalimbali, n.k.
Vijana wengi wamesoma sheria wapo majumbani.... Wengi wamesoma mambo ya uchumi, utalii, n.k wapo wanasota mitaani bila kazi... Lakini wote hawa walikopeshwa fedha za masomo na serikali...
Wanaambiwa ili uajiriwe rudi chuoni usomee ualimu...

Serikali ya watawala hawa kwa makusudi kabisa wanawachanganya wasomi na kuwasababishia maradhi mbali mbali kimwili, kiakili na kelele za kisaikolojia bila sababu zote za msingi...!!

Kulipiza kisasi angalia wasomi wanavolazimisha waitwe kwa title zao hata kama ni kinyume na uhalisia... Wako bize kusubiria utangulizi wa sifa zao...Yaani bila kutanguliza Professor, Doctor, Engineer, n k hupati huduma yake..Eti wanafidia heshima...sawa...

Lakini pia kila wizi unaofanyika kwenye mashirika ya umma/serikalini ndani yake kuna ushiriki wa wasomi wazuri tu waliosomeshwa kwa fedha nyingi sana...Eti wanafidia gaps kwenye maisha...

Haihitajiki akili nyingi kujua kuwa haya yote ni kwa sababu wamechanganyikiwa kutokana na dharau iliyoasisiwa na serikali ya CCM....

Ebu jiulize ni taifa gani duniani (tofauti na Roma ya zamani) inayoongoza kwa kuwadhalilisha na kuwaua wasomi kama Tanzania...???

Tunaishi kwenye ombwe kubwa sana...na itatuchukua muda mrefu sana kuliziba.....

Ila nina uhakika kwa sababu "Kidumu chao kimeshatoboka" ni vizuri huu mwaka 2015 tuwaweke pembeni ili tuanza moja kujenga msingi wa taifa letu bila matabaka haya yaliyopo sasa...!!
 
Back
Top Bottom