Nimesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari mbalimbali kuwa kuna wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar-es- salaam wameelani vikali kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA, shida yangu haipo kwenye wao kulaani hiyo kauli maana mimi sio mshabiki wa vyama vya siasa ila shida yangu iko kwa wasomi hawa wasioweza kutafuta 'solution' ya matatizo yanayoikumba nchi yao na wakiwa wamenyamaza kimya kwenye mambo ya msingi yahusuyo nchi, utawasikia tu 'boom' likiwa limechelewa au kujibu/kulaani kauli za wanasiasa!
Kuna fedha za 'account' ya escrow inayohusiana na tanesco wao hiyo kwao sio muhimu, hizi fedha zinazotafunwa bungeni bila kupata katiba woa hawatafuti 'solution' ya kuepusha fedha hizo zisitafunwe bali wanakaa kudandia hoja za wanasiasa, hii nchi kama inatengeneza wahitimu wa vyuo vikuu wa staili hii basi tujiandae kutawaliwa na 'vichaa' wasioweza kubuni na kutatua vitu vya msingi bali kudandia hoja na na kwenda na matukio!
wanafunzi jipangeni, hamuutendei haki ubongo wenu, elimu yenu, nchi yenu bali mnataka umaarufu wa kipumbavu!