Nchi gani hii?

Tuanzishe soko la konokono tanzania tuwauze nje hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira huku si hatuwatumii
 
hiyi kitu west africa wanakula matajiri tu, maskini hawezi kumudu gharama yake. hata akikamata bora akauze apate mpunga wa kutosha kutimiza mahitaji ya lazima kwake. Wenyewe wanaita ni delicacy food
 
Hiyo ni fursa nzuri sana kwa sasa ambayo haihitaji mtaji mkubwa. Kenya wanaitumia vizuri sana.
 
Mkuu una uhakika hiyo ni sea food? Hembu angalia vyema jombaa
 
Tatizo sisi tumewazoea kuwaona konokono katika hali yao ya utelezi fulani. Lkn hakuna mboga nzuri kama iyo kitu. Hapo Kenya umekua mradi mzuri sana kwa watu walioiona fursa. Mshana ukibahatika kula hii mboga,mbuzi na ndugu zake utawasahau.....
 
Never on earth
 
Ha ha ha! Kwakua neema ya mboga saba kujisevia ipo una haki kuendelea kuchagua.
 
nahisi ujenzi wa barabara unaendelea hapo kwa hisani ya wale wale wa feki
 
Mkuu una uhakika hiyo ni sea food? Hembu angalia vyema jombaa
Mkuu, kwani hiyo kitu ikipikwa inawekwa kwenye kundi gani la chakula. Mimi huko nilikoikuta ilikuwa iko kwenye kundi la sea food na kilikuwa chakula gali sana, wanakula watu wenye pesa au unaandaliwa kwa heshima kama Mgeni, kiliandaliwa kwenye ajili yetu kama wageni, tulikuwa wanane kutoka nchi za Afrika tuliokuwa masomoni (internship) nchini nchina. Jamaa kutoka Morocco ndo alikifurahia, kesho yake tulimwambia Mratibu (Mwenyeji) kuwa hiyo kitu baadhi yetu sio utamaduni wetu. Walikuwa wanamwandalia Jamaa kutoka Morocco.
 
daah ila kila sehemu na utamaduni wake,kuna mzungu mmoja mmarekani yaani yeye dagaa alikuwa anaona kinyaa kwelikweli na alikuwa anatuona waajabu kula dagaa
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…