Nchemba amshika pabaya Mnyika (leo bungeni)

muda huu wa saa sita na dkk 50 mbunge wa iramba mh. Nchemba amemshika pabay mh. Mnyika bungeni. Nchemba baada ya kuchangia ktk wizara ya maji, amemkumbusha mwenyekiti wa bunge mama mhagama kuwa leo ndiyo siku ya saba na ya mwisho ambazo mnyika alipewa kuthibitisha kuwa nchemba anahusika na wizi wa EPA. Mwenyekiti amemuomba asizungumzie suala hilo kwa kuwa linashughulikiwa na ofisi ya spika. USHAURI WANGU KWA CHADEMA Katika kikao cha kamati kuu ya chadema kinachoendelea, wanachadema wakumbushane kulinda kauli zao bungeni. bunge ni pahala patakatifu! siyo kijiweni. vile nchemba amekumbushia leo, inaelekea anaamii kuwa hahusiki. alijiunga na B.O.T baada ya kashfa ya EPA. na alikua ofisa wa chini. inaelekea suala hili litamkalia pabaya mnyika! tuache kuropoka! Wakatabahu: wakuziba (mzee wa ukweli unaochoma)
Sidhani kama aliropoka mkuu, yote yanayo ongelewa huwa na ushahidi, na katibu wa bunge aliposema linashughulikiwa na ofisi ya spika hatujui alimaanisha nini.. may be ushahidi ulishapelekwa but kunao wengi wanaohusika na itaharibu picha nzima ya movie ya serikari bungeni that why wamesema linashughulikiwa na bunge.....
 
Mwalimu!
ni kwanini hii forum siku hizi inapotokea mtu ana mawazo tofauti na wachangiaji wa Pro Chadema basi anaandamwa na kejeli na matusi au kukatishwa tamaa ,Hoja kwa hoja zimekwenda wapi?
Swala la Pro-CHADEMA na Pro-CCM huenda linaingia inherently kwa vile CCM iko upande wa serikali inayoshindwa ku-deliver, na CHADEMA inajitokeza kuishambulia serikali hiyo kwa lengo la kuitaka i-deliver. Mimi siyo shabiki wa chama chochote ila nachukia serikali kutapanya raslimali za nchi na kuwaacha wanachi wengi kama watu wasiokuwa na nchi. Kwa hali hioyo ni rahisi kuchukulia kuwa mimi ni pro-CHADEMA lakini siyo kweli; juzi juzi nilim-support sana mbunge wa Musoma Vijijini kwa tiketi ya CCM- Mkono, kuhusiana na swala la Kiwira, ingawa nimeshampiga vita sana kuhusiana na mambo mengine ya hela za umma Benki kuu. Mara kadhaa nimemshabikia Filikunjombe (CCM) kutokana na msimamo wake dhidi ya serikali. Majuzi tu nilikuwa nimeshupalia mbunge wa CHADEMA aliyekuwa anashukiwa kuwa na kesi ya jinai Marekani ingawa baadaye ilikuwa onekana kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli. Kwa hiyo mimi siyo mfuata upepo wa siasa bali ninafuata maslahi ya nchi.

Sasa tukirudi kwenye ile post niliyoquote, je wewe uliisoma na kuona kuwa kulikuwa na mada ya kujadili? Mimi nimeona ni thread yenye title kubwa lakini ndani yake ni upuuzi mtupu uliojaa ushabiki wa kisiasa, na hicho ndicho nilichojibu. Kungekuwa na hoja, basi ama ningejibu hoja, au ningekaa pemebeni niachie wanaoijua mada hiyo sawasawa waijadili. Onyo langu kwa watu wa aina ya mwanzisha thread hii ni kuwa watumie akili zao sawasawa kuwa wanaleta mada zenye ama kueleimisha au kuchochea majadiliano ya maana kitaifa badala ya kuleta mada zenye nia ya kubishana kisasa.
 
muda huu wa saa sita na dkk 50 mbunge wa iramba mh. Nchemba amemshika pabay mh. Mnyika bungeni. Nchemba baada ya kuchangia ktk wizara ya maji, amemkumbusha mwenyekiti wa bunge mama mhagama kuwa leo ndiyo siku ya saba na ya mwisho ambazo mnyika alipewa kuthibitisha kuwa nchemba anahusika na wizi wa EPA. Mwenyekiti amemuomba asizungumzie suala hilo kwa kuwa linashughulikiwa na ofisi ya spika.

USHAURI WANGU KWA CHADEMA

Katika kikao cha kamati kuu ya chadema kinachoendelea, wanachadema wakumbushane kulinda kauli zao bungeni. bunge ni pahala patakatifu! siyo kijiweni. vile nchemba amekumbushia leo, inaelekea anaamii kuwa hahusiki. alijiunga na B.O.T baada ya kashfa ya EPA. na alikua ofisa wa chini. inaelekea suala hili litamkalia pabaya mnyika! tuache kuropoka!



Wakatabahu: wakuziba (mzee wa ukweli unaochoma)

Nadhani hufahamu kabisa tafsiri ya neno hilo!
 
Back
Top Bottom