Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,498
- 7,065
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walikuwa wanafahamu kuhusu uwezo wa viongozi waliochaguliwa ndani ya chama lakini wanachama wa CHADEMA wao wenyewe ndio walikuwa wakiaminisha watu kwamba Mwenyekiti wao Tundu Lissu hatoshi katika nafasi hiyo
Soma: Ester Bulaya: Lissu ana uwezo wa kutufikisha kwenye Demokrasia ya kweli. Apongeza CHADEMA kwa Uchaguzi Uhuru na Haki Bungeni Dodoma
Mwigulu ameyasema hayo tarehe 13 Februari, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Taarifa ya ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC
"Dada yangu Esther akisema kwamba Tundu Lissu anaweza, na Mnyika anaweza na Heche anaweza, Mwenyekiti sisi wenyewe tulikuwa tunajua anaweza, lakini wao ndo walisema hatoshi hata kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji kwahiyo sio sisi ni wao, sisi tulishafanya naye kazi kwenye Kamati humu", amesema Mwigulu.
Mwigulu aliinuka kuzungumza baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya kusema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu anao uwezo wa kukiongoza chama hicho na kukifikisha kwenye demokrasia ya kweli.