Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
Mwandishi wetu, Babati (Tanzania Daima)
CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimekishauri Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhakikisha kinaweka umoja na vyama vingine ili kujiimarisha katika uchaguzi mkuu ujao hatua itakayofanikisha kuibuka na ushindi katika ngazi ya urais.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Bermi, Kata ya Dareda, Wilaya ya Babati Vijijini, mkoani Manyara, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Danda Juju, suala la vyama vya upinzani kuungana halikwepeki kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina mtandao mkubwa.
CHADEMA kwa sasa wanajiona wako juu ya vyama vingine vya siasa, wao wanajiona ndiyo wapinzani wa kweli kuliko wengine wote japokuwa hilo siyo sahihi hata kama kitaungwa mkono na Watanzania wote, alisema na kuongeza kuwa kitendo cha kutoshirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuishinda CCM kitawagharimu kwa sababu hawawezi kushinda urais wakiwa wao peke yao, alisema.
Alisema kuwa kabla ya CHADEMA kuwa maarufu, kilianza NCCR-Mageuzi na kwamba kila Mtanzania alijua jinsi chama hicho kilivyotikisa wakiwa na uongozi wa Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.
Alisema kuwa hata hivyo umaarufu wa NCCR uliporomoka, na ikaja zamu ya Chama cha Wananchi (CUF) ambacho nacho kwa sasa kimepoteza umaarufu na sasa ni zamu ya CHADEMA ambao wanatikisa katika upinzani
My take: Ni wazo makini sana, kwani adui namba moja ni mmoja. Lakini viwe vyama vya upinzani vya ukweli, sio mamluki.