NCCR wapinga mgao wa Majimbo UKAWA

NCCR wapinga mgao wa Majimbo UKAWA

DEO MECK Mbag

Gazeti lenyewe na Mleta hoja wote ni 'chumia tumbo'...wanaombea 'dua la kuku limpate mwewe' wapi na wapi? Ungekuwa una uchungu na UKAWA au ungeijua UKAWA inavyoendesha mikakati yake ungekuja na hoja ambayo ni 'curious' au yenye kuaninsha kwa kutumia vigezo vingine ambayo UKAWA inaweza kumaliza hilo tatizo, kama lipo kweli kama sio linatengenezwa na CCM na ACT!

Unaposema 'viongozi wetu' wakati unajua akilini [UKAWA] sio viongozi wako, ...bali wewe unaelekezwa na 'wengine', hiyo ni failure no1 ya hoja yako! Na wanaoisupport wote wanaonekana wanashabihiana na mwelekeo wako kiitikadi, kwa style hiyo 'argument disqualified due to biasness'...hizi hoja za Ki-magamba magamba hazinaga 'wigo wa fikra'...wanajitekenya na kuanzia hapo wanaendelea kuchekeshana wenyewe kucha ..kutwa ...!
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa, lakini pia tuangalie hali ya chama hicho wilayani Tarime ikoje? Nashawishika kuamini kuwa tamko hili lina msukumo toka nje ya UKAWA. Ningewaelewa zaidi kama tamko lingetoka, kwa mfano, kwenye moja ya majimbo mkoani Kigoma siyo Mara. Huko walijifia Marando alipoondoka.
hilo ndio tatizo kudharau vyama vingine kuwa havina nguvu
 
Kila chama katika Ukawa kinategemea nguvu ya mwenzake ili kushinda Ubunge...lakini Nguvu kubwa ya ushindi inayotegemewa sana katika Ukawa ni CHADEMA ili vyama vingine vya ukawa viweze kushinda...Bila Ukawa...Nccr inaweza kushinda majimbo 3 tu ya kigoma tena nayo ni hati hati...na bila Ukawa hata Mbatia hatingi bungeni....Mimi natoka Tarime...Tarime hakuna nccr pale..labda Cuf iseme lakini siyo Nccr...

Tunazo taarifa kuwa Mbunge wa Tarime CCM Ndiye aliyewahonga hao jamaa ili watoe hilo tamko...na kuleta mvurugano ili yeye aje ashinde kirahisi...
 
Mim sio mnafiki huu muungano ni wa kinafiki mno upo tu pale juu huku chini kila chama kipo kivyake halafu watu hawataki kuwa wakweli

Mhh! Mbona muungano wa wengine wanaoumia na matatizo au changamoto ni wengine??? Inaelekea unatishia wengine?
 
Mkuu, wewe hili wazo la kwamba UKAWA ni muungano wa vyama umelipata wapi?

Kwa hiyo wewe unatakaje?


Mim sio mnafiki huu muungano ni wa kinafiki mno upo tu pale juu huku chini kila chama kipo kivyake halafu watu hawataki kuwa wakweli
 
Haya tulijua yatatokea na haya ni madogo sana na hayana uratibu rasmi bado wanajipanga kuhujumu UKAWA kwa mkakati rasmi.

UKAWA tutatasongo mbele na tutafanya maamuzi yetu kulingana na tukio,mazingira,mtu,nk.

(Varughe vushaa tekinasha icho.)
 
Kila chama katika Ukawa kinategemea nguvu ya mwenzake ili kushinda Ubunge...lakini Nguvu kubwa ya ushindi inayotegemewa sana katika Ukawa ni CHADEMA ili vyama vingine vya ukawa viweze kushinda...Bila Ukawa...Nccr inaweza kushinda majimbo 3 tu ya kigoma tena nayo ni hati hati...na bila Ukawa hata Mbatia hatingi bungeni....Mimi natoka Tarime...Tarime hakuna nccr pale..labda Cuf iseme lakini siyo Nccr...

Tunazo taarifa kuwa Mbunge wa Tarime CCM Ndiye aliyewahonga hao jamaa ili watoe hilo tamko...na kuleta mvurugano ili yeye aje ashinde kirahisi...
haishangazi kwamba hata wanaotokwa povu humu ni haohao ccm.
 
CHADEMA walishapotea pale walipoanza mgogoro na ZITTO na ndiyo maana wakaamua kuotesha Mbegu mpya ya CHADEMA HYBRID wakaiita UKAWA ...
Kwa maana hiyo unakiri kwamba wamerudi!
 
Nimeattach gazeti lenye tamko la chama cha nccr mageuzi wilaya ya Tarime kikipinga mgawanyo wa majimbo ndani ya Ukawa.Chanzo: Habari Leo

Let us be serious, hivi kweli NCCR Mageuzi nje ya UKAWA wanaweza ku imagine hata kushinda majimbo 10 ya uchaguzi let alone hayo 33 waliyopewa na UKAWA ambao wana uhakika wa kushinda > 60%

Kweli Waafrika tu waroho wa Madaraka! Yaani mtu anaona ni bora chama kipate majimbo 4, kuliko kupata majimbo 20 kwasababu tu yeye hakupata nafasi ya kugombea?!
 
Magamba at work na hayatafanikiwa............! Subiri octoba, wataamkia jikoni ndo wataamini wameshaliwa
 
Deo Meck Mbagi

Mkuu habari leo ndio umeliamini kuhusu habari zinazohusu issue ya upinzani nchini? Hao wanatafuta habari yenye mvuto kwa wananchi walio wengi ili angalau wapunguze magazeti yao kuwa visafisha na vilinda meza za mauzo ya magazeti hapa nchini.
 
Last edited by a moderator:
Kazi ya kuitoa CCM madarakani ni ngumu kama kumuondoa shetani duniani. Imejaa vikwazo, majaribu na kukata tamaa kwa baadhi ya washiriki.
Kila jambo lililo jema lazima likutane na vikwazo na hao CCM sio kuwa wameugua Polio kwamba watakaa tuu kuangalia wanavyo achia madaraka

Ni kweli mkuu kazi ni ngumu sana inayohitaji uvumilivu na umakini na ushirikiano wa hali ya juu sana,kukitoa chama kilicho kwenye dola ni mtihani sana.
 
NCCR mageuzi wanajua taratibu za kuzifuata kungekuwa na matatizo wengefuata taratibu za kichama.

Hayo mapingamizi ya kwenye magazeti ni ya magazeti,yataendelea kuwa ya magazeti na yataishia kuwa ya magazeti hivyo hivyo.

Kwa habari leo sishangai
 
Back
Top Bottom