NCCR MAGEUZI wako makini kuliko CHADEMA

NCCR MAGEUZI wako makini kuliko CHADEMA

Hizi ni propagannda tu ila siku moja CCM itakuwa chama kikuu cha upinzani nchini, na sijui watapinga nini!
 
mbona huna msimamo braza?kama baamedi yani kila mteja anaeagiza sana unataka umhudumie wewe.tuliza akili halafu ungana na upande unaouamini tena usifuate watu fuata misingi.mara Juzi ulikua CDM,Jana CCM,leo asubuh ACT jioni unaomba watu wakusaidie kuchagua.acha kua na akili za kushikiwa.utamegwa,utafata misimamo ya wanaume wenzio mpaka lini?utamegwa....
Misukule ya aina yako ndio inayochelewesha mabadiliko
 
Nadhani "Nyinyiem" mjiandae kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya Cdm kuchukua dola 2015.
kumbe siki hizi ukishinda jimbo la karatu linakuwa dola? nilikuwa sijui. kweli kupitia jf nitajifunza mengi!
 
Siasa za chadema ndio hivyo zipo ukingoni, kinapotea. Ni vyema tuanze kujiandaa kisaikolojia kukiunga chama kingine mkono ambacho kitashika hatamu ya kuongoza upinzani nchini na hatimaye kushika dola ya tanzania.
Nccr?
cuf?
chauma?
ADC?
A.C.T?
au the beautiful ones are not yet born...

...ccm kinafuata baada ya chadema...
 
Ndg yangu na mtanzania mwenzagu siasa ya nchi yetu inahitaji umakini mkubwa kuichambua na kujua khali halisi ya kila chama na nafasi yake. Unachotaka kukifanya kuwa ni kumbukumbu rejea kwa anguko la CHADEMA ni hizi chaguzi mbili zilizopita na mengineyo ikiwemo kufukuzana. Tambua watawala hutumia udhaifu wetu kiuchumi na kielimu kupenyeza kila aina ya propaganda wazitakazo au kuuwa nguvu ya vyama shindani pale inapohatarisha uwepo wao madarakani. Sidhani kama CUF imepotea katika ramani za siasa za Tanzania kwan bado ni chama dola kwa upande wa Tanzania Visiwani kinaunda serikali ya mapinduzi zanzaibar kikishiriki kwenye maamuzi mhm kwa mskabali wa Wazanzibar na hata Tanzania kwa ujumla wake. Kile kilichofanywa na chama kikuu cha upinzani kwa Tanzania bara ni kuondoa kila aina ya viongozi wasioenenda na kauli mbiu ya chama na dira yake. Usitegemee kipyatoka kwa mtu ambae kila uchao anataka kukurudisha nyuma na ukabaki kuogopa kufanya maamuzi sahihi kwa jambo ambalo huenda athari yake ingelikifanya chama kipotee kwenye ramani ya siasa za Tanzania,hatuna bdi kumshukuru Mungu kuweka safu sahihi ya uongozi na yenye kusimamia kile chenye tija kwa wengi vinginevyo leo chadema ingelikuwa historia. Chaguzi zinazofanyika kwa sasa na mazingira yake yalivyo ni vigumu kwa chadema kuweza kupenya,napenda uwepo wa upinzani imara kwa maendeleo la Taifa langu Tanganyika kama si Tanzania iliyo shirikisho.
 
Wewe ifweero inaonekana ni mchumba wa magamba,,lini ndoa yako itafungwa?walau nikuletee zawadi ya harusi yako.
 
CCM kinafaa kuwa chama kikuu cha upinzani baadaya CHADEMA
 
nafasi ya chadema imeshachukuliwa na chama makini cha ACT siku nyingi sana
 
Nadhani chama kikuu cha upinzani baada ya 2015 itakuwa CCM baada ya muungano Wa UKAWA kuchukua Dola Full Stop.
 
Endapo cdm kitafeli ktk nia zake za atleast kubaki ktk kiongozi wa kuongoza kambi ya upinzani bungeni,Sifikiri tena kama kuna chama kingine kitakachokuwa na ubavu kama cdm,ingawa nccr mageuzi iliwahi kuwa imara pamoja na cuf,Maana tumeshachoka na mavyama yakinafki,chama kingine kimaweza kuwa imara endapo tu,"Kiongozi pendwa atatoka ndani ya ccm na kuhamia chama cha upinzani"unless otherwise the die of cdm means the end of real multipatism in tanzania

sikubaliani nawe na hasa unaposema kufa kwa chadema ndio mwisho wa multipartism bcouse historia ya vyama vingi Tanzania wala haitufunfishi hivyo, ilikua NCCR na ilivyokufa CUF ikaibuka nayo iliposinyaa CHADEMA ikasimama hivyo kufa kwa CHADEMA lazima kiibue chama kingine kitakachokuwa na nguvu
 
Mbona mnajichanganya,mnasema cdm wachaga je Mbatia ni nani! Makenge nyie nendeni ccm mkawe majambazi.
 
Hizi ni propagannda tu ila siku moja CCM itakuwa chama kikuu cha upinzani nchini, na sijui watapinga nini!
CCM hakitakuwa chama upinzani, kitatoweka kabisa katika ramani ya siasa za nchi hii. Mungu sio wa kuchezea dhuluma ni lazima ilipwe
 
Nimefuatilia kwa ukaribu na kugundua kuwa NCCR mageuzi ndio chama pekee kinachoweza kukabiliana na chama dume CCM bila kuweweseka kama CHADEMA.

1. NCCR hawawatumii wananchi kufanya vurugu wapate umaarufu
2. Maandamano ya NCCR huwa ya amani
3. NCCR ni chama cha watu sio mtu mmoja.

Mpaka sasa kutoka upinzani ni Mbatia pekee(mwenyekiti wa NCCR ) aliefika kwenye tukio la ghorofa kuanguka Dar wakati CHADEMA walikuwa wanapiga kili baridi wakisubiri kutoa tamko.

Mengine naomba mniwekee wenyewe hapa.
Nccr mageuzi ya Mrema enzi hizo sikumbuki kama tuliwahi kuisifia namna hii zaidi ya kuipiga mabomu.NCCR ya sasa haina madhara kwetu lazima tuisifu.please take my word.Adui mkuu wa nchi hii ni CCM.Hao wengine kama akina chadema,CUf nk. tunawatoa kafara tu-Najua hata wewe ukiwa mwenyewe unakiri kuwa ccm in adui mkubwa wa Tanzania na watu wake.
 
Back
Top Bottom