Karamagi wa TICTS' ahaha kwa wahariri, wabunge
* Ni baada ya mkataba wao kufutwa bandari ya Dar es Salaam
* Kampuni ya PR ya Capital Plus yapewa kazi kuisafisha TICTS
* Wapanga uhujumu wa huduma za makontena bandarini baada ya kuenguliwa
WAZIRI mstaafu Nazir Karamagi na mfanyabiashara Yogesh Manek wameanza kampeni mahsusi kwa wahariri na wabunge kujaribu kuikwamua kampuni yao ya TICTS ambayo imefutiwa mkataba wa kuendesha eneo la makontena kwenye bandari ya Dar es Salaam.
TICTS wamefutiwa mkataba huo baada ya kushindwa kuonesha ufanisi kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
"Karamagi na Yogesh wanahaha kila kona kujaribu kushawishi wahariri, wabunge na maafisa waandamizi wa serikali wairejeshee mkataba huo," alisema mfanyakazi mmoja wa kampuni ya uchukuzi.
"Wanataka kuwaweka sawa wahariri ili waanze kampeni kwenye vyombo vya habari ya kuitetea TICTS irejeshewe mkataba"
Taarifa zinasema kuwa TICTS wameajiri kampuni ya PR ya Capital Plus kufanya kazi ya kuwasafisha kwenye vyombo vya habari."
Vyanzo vyetu vya habari vinasema kuwa baadhi ya watumishi wa TICTS wanapanga kufanya hujuma kwenye huduma za makontena bandari ya Dar es Salaam baada ya mkataba wao kwa hasira ya kusitishiwa mkataba.
"Huenda tukasikia huduma za makontena bandari ya Dar es Salaam zimesimama ghafla kwa hujuma baada ya TICTS kufutiwa mkataba kabla mwekezaji mpya hajaja," alisema.