Jicho la Tai
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 1,452
- 609
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ni Mgombea ambaye mambo yake yameenda Kimyakimya sana mpaka Dakika za Mwisho.
Hakuna aliyejua kuwa Pinda atagombea Urais mpaka Siku ile ya tarehe 21 Octoba 2014 alipotangaza Kimyakimya na hapo ndipo wapinzani wake kupitia Vijana wao walipoanza kumwagia Shutuma mbalimbali. Kunyume na hayo ni mtu safi ndani ya Chama.
Hajawahi kujitokeza kusema sera zake hadharani kama wengine, kwanza hakutangaza nia kwenye majukwaa zaidi ya kwenda kuchukua fomu na kuzungumza na waandishi wa habari hata hivyo hakuzungumza sera za Kuomba kura zaidi ya kusema nini serikali imekifanya mppaka sasa.
Waandishi wa habari walipotaka kujua yeye ana lipi alisema hawezi kwenda huko kwani Utaratibu wa Chama husimami na kuanza kuongea lolote, mara zote wanaongozwa na ilani ya chama cha Mapinduzi. Hivyo aisema atafanya nini atakuwa amekiuka miiko kwani hata ilani haijatoka.
Nimemuona mara chache sana kwenye vyombo vya Habari tofauti na wengine. Amekuwa akiendesha kila kitu kimyakimya mpaka dakika za mwisho. Watu wengi wamekuwa wakipata wasiwasi kuhusu ukimya wake na kwa habari ambazo ni za Uhakika kutoka chanzo change ni kwamba ana Mtandao wa Wajumbe wengi ambao wanamuunga mkono kuliko hata yeye anavyotegemea.
Hakuna mwenye sababu za kumpinga ndani ya Chama chake, kama sio Rushwa kwenye uchaguzi huo basi kuna uwezekano mkubwa Akapita.