Nawezaje kuondoa matangazo kwenye android?

Nawezaje kuondoa matangazo kwenye android?

Angalia application zako ndizo zenye kuleta hayo matangazo ambazo hutumii ondoa kisha angalia tena kama bado matangazo yataendelea kukufikia
 
Habari zenu wana Jamvi.Nina tatizo moja linalonisumbua,Tatizo hili yawezekana likawepo kwenye simu za wengine pia.Simu yangu nikifungua Data na nikifungua Internet inaleta matangazo ambayo si tu yananikera kwa kuniharibia program zangu bali mengine yananitia aibu kwani inaleta matangazo ya wadada walio uchi na wengine wanasex. Naomba msaada kama kuna njia ya kuzuia matangazo haya yasitokee
ipeleke kwa fundi simu anaeflash akuwekee firmware nyingine(aflash) otherwise utaendelea kusumbuka
 
Tafuta IT aliyoko karibu na ww na mwambie afanye rooting kwenye sim yako ili kuzuia start up apps
 
Kama simu yako iko rooted download app inaitwa ADAWAY(haipo playstore itafute kwenye Google search andika ADAWAY Apk) hii inaondoa ads zote kwenye simu yako haijalishi ziko kwenye apps au hata games hii ndiyo solution mkuu.
 
Imeshaa haribika hiyo...ITIE KWENYE MAJI....alafu weka sabuni ya UNGA kidogo...

...subiri kama dakika 5 ikitoka hapo BOMBA...! utafurahi na ROHO yako...
 
teh teh teh matangazo hadi ya porno.
pole nadhani michango ya wadau inatosha.
 
Factory reset haitoi adware..maana wanajieka kama system app ,solution ya uhakika ni kuweka rom mpya..
Akiweka antivirus je?........ Kwa sababu hata mimi laptop yangu iliingia hao virus nimeweka antivirus wameuawa wote sasa hivi niko poa!
 
Habari zenu wana Jamvi.

Nina tatizo moja linalonisumbua,Tatizo hili yawezekana likawepo kwenye simu za wengine pia.Simu yangu nikifungua Data na nikifungua Internet inaleta matangazo ambayo si tu yananikera kwa kuniharibia program zangu bali mengine yananitia aibu kwani inaleta matangazo ya wadada walio uchi na wengine wanasex.

Naomba msaada kama kuna njia ya kuzuia matangazo haya yasitokee
kuna app zifuatazo zinaweza kukusaidia
-Adsblock plus
-adaway
-Adclear
zipo nyingi tu jaribu google
 
Habari Wana Jf, Karibuni kwenye makala nyingine fupi kutoka Tanzania Tech leo tutaenda kuangalia jinsi ya kuondoa matangazo (Ads) kwenye app za android. Najua ni kweli kabisa kuwa matangazo ndio chanzo cha mapato kwa developer au muandishi wa app fulani lakini ukweli ni kwamba kuna wakati unakuta matangazo yamezidi kwenye app mpaka maana ya kuwa na app hiyo kwenye simu yako inapotea ndio maana leo tunakuletea njia hii rahisi na itakayo kusaidia kuondoa au kupunguza matangazo kwenye app za simu yako ya android.

Kumbuka njia hii inaweza kuondoa matangazo kabisa au kupunguza tu baadhi ya matangazo, vilevile njia hii inaweza kukataa kufanya kazi kwenye simu yako hivyo kama itakataa tuandikie kwenye maoni hapo chini nasi tutakujibu moja kwa moja. (Sorry kwa kukosea baadhi ya Spelling kwenye Video)



LINK MUHIMU
1. Download Programu ya Lucky Patcher Hapa http://bit.ly/2okfu5w
2. Maelezo Kamili yanapatikana Hapa (Muhimu Kuyapitia) Jinsi ya Kuondoa Matangazo Kwenye Programu za Android
KUJIFUNZA MAUJANJA ZAIDI LIKE NA SUBSCRIBE NA TEMBELEA TANZANIA TECH KUSOMA HABARI NA MAUJANJA MENGINE MENGI.
 
Back
Top Bottom