Habari ya wakati huu, wakuu?
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27, na ni ndoto zangu kwenda nchi ya Canada au ughaibuni popote tofauti na bara la Asia kusoma na kutafuta maisha. Nina shahada ya sheria, lakini hata hela ya kwenda pale Law School ni tatizo. Kama kijana nisiye na manung'uniko na kulaumu mzazi kutoniendeleza, nimefanya jitihada kadhaa mpaka sasa, kuomba scholarship na najinoa pia lugha kwa ajili ya mitihani ya IELTS.
Lakini katika mizunguko yangu, kuna mzungu mmoja ambaye hatufahamiani aliniuliza maswali kadhaa, na kwa kuwa anuani yake inaonesha yupo Canada, Jimbo la Quebec, nilimuomba kama kuna namna naweza kwenda nchi yao. Akasema ipo, akanitumia fomu ya VISA ambayo ilikuwa kwa lugha ya Kifaransa. Nikatafuta watu, nikawalipa wakanisaidia kuijaza.
Baadaye, akaniambia nitume hela kwenda huko kwao kwa ajili ya kuthibitisha taarifa zangu, hapo ni baada ya kupokea barua pepe kadhaa zinazoonesha kwamba taarifa zangu zimepokelewa. Nikaamua kwanza elimu yangu inisaidie, maana kusikia cha kike kuingia ni rahisi sana.
Nikadelay kulipia kiasi hicho cha shilingi laki mbili na hamsini, nikamuambia sina, labda next round. Lakini amekuwa mtu anayenisisitiza kuwa ameomba faili langu lihifadhiwe na wamekubali. Nifatilie passport, NIDA, na ripoti ya matibabu, halafu nilipie na pesa.
Kwa kuwa sio mtu tunayefahamiana zaidi ya mitandaoni, naingiwa mashaka, na hili linanileta jinamizi. Ninaomba kujua jinsi ya kuthibitisha taarifa zangu kama kweli zipo Canada. Kwa mwenye ujuzi, naomba anisaidie.