Naweza kumpata mpenzi wa kweli kwenye mitandao?

Naweza kumpata mpenzi wa kweli kwenye mitandao?

cha mcngi awe mcha mungu. la cvyo watakufanya vodashop,na tgoshop. kumbuka wapo humu kwa iyo ni bundle zinatumika. watashukuru kweli ili mishahara yao isiwe na bajet ya vocha. ha ha ha ha ha!
 
Utampata unae endana nae kama wewe ni wa kweli utapata wa hivo hivo kama wewe ni feki hivohivo.
 
cha mcngi awe mcha mungu. la cvyo watakufanya vodashop,na tgoshop. kumbuka wapo humu kwa iyo ni bundle zinatumika. watashukuru kweli ili mishahara yao isiwe na bajet ya vocha. ha ha ha ha ha!


Kwann usifikie kwamba watapendana na watatengeneza familia nzuri
 
Unaweza sana, ila uwe makini tu. Maana watu humu sio wa kweli
 
Ni kweli naweza kupata mpenzi au mke wa kweli kwenye hii mitandao?

wachangiaji wengi wamesema kwamba unaweza kupata au usipate kwa sabab walioko mtandaoni ni hao hao hao ulionao mtaani, ni sahihi kabisa....zaidi saana mtandao una uwezo wa kukuongezea uwanja wa kuchagua kwa kukukutanisha na watu ambao usingeweza kukutana nao, pengine kutoka maeneo ambayo usingeweza kufika.... My Take, usitafute mke mtandaoni,tafuta marafiki wa kike ambao, viwango vyenu vya urafiki vitakapokua, itafika mahali mtafahamiana zaidi hadi kwa kuonana, kwa historia na familia mnazotoka, na hata tabia zenu zitakuwa wazi kwa kila mmoja. Huenda Kwa kufikia hatua hii, na kwa 'quaresma', huenda ukampata mwenzi bora kabisa wa maisha yako, na ukafika hapa kutushuhudia...
 
Asilimia kubwa ya wanawake walioko mitandaoni ni machangudigital.! Pesa mbele! Ukimtigopesa tu umemaliza! Usiwe na mkono wa birika! Uwe unatoa!. Ukitaka wa maana rudi mtaani kianalogia.!
 
Naamini mume au mke anapatikana popote, wawezampata bar, barabaran, Nyumba za ibaada, kwenye daladala na hats humu na akawa wakufanana nawe haswaa, km ww wataka wa mtandaoni utampata tu, endelea kurusha kete zako

asirushe tu kete bila mgangilio. zikianguka mahali pasipostahili zaweza ota pia, ila mimea goigoi, na hapo ndipo taabu itakapoanza..
 
Ukielewa maana ya neno "upendo" basi popote unaweza kumpata. Ila kumbuka tu, mke bora hutoka kwa Mungu. Na kwa vile Mungu yuko kila mahali, basi na mtandaoni yupo maana wanaotandaa pia ni watu wake. Kuwa tu makini na fanya ibada, mke sio kitu cha mchezo.
 
Wapo unaweza pata mzuri tu mwenye kila sifa njema na aliyebarikiwa...

Ingawa mpaka umpate wa kweli huwa kuna kazi kidogo...

Mtandaoni yaweza kuwa, kupitia social medias, wrong number, redioni magazetini etc. njia zote hizo huwa zinatabia ya kufuatana na kuingiliana changamoto kubwa ni muda pamoja na identity mtu atakayo jivisha.. Na perception ya target husika nk

Kuna visa vingi vya tabia za hawa watafuta wenza humu, vingine vya huzuni vingine vya mzaha na vingine vya furaha, ila kwa wataalamu wa kweli wenye nia kwao wao hizo ni fursa za kuwasoma tabia na kuchagua.

Kwa mtazamo wangu kutafuta wenza digitally ni moja kati ya njia nzuri na rahisi za kumpata yule mnae endana... Na ni most secure kwani needs zenu zitabaki kuwa zenu nikimaanisha privacy. Lkin pia mtakuwa mpo radhi kuanzisha kitu familia mpya ndani ya jamii.

Madhara yapo mengi mno ila yanaepukika
 
Mdau hawa wanawake wa mitandaoni ndo hao hao wa mitaani, unaweza kumpata mtaani kumbe huyo huyo kuna mwenzio kampata mtandaoni. Mwanamke ni mwanamke tu no matter amepatikana wapi kikubwa ni tabia tu.
 
Ni kweli naweza kupata mpenzi au mke wa kweli kwenye hii mitandao?

Mtaani hakuna candidates?

Kama huwezi kumwangalia mtu machoni na kumweleza shida yako basi wewe ni fisi mla mizogoa. Hata huko kwenye mitandao utatakiwa umkabili mtu siku mtakayoonana!
 
Mtaani hakuna candidates?

Kama huwezi kumwangalia mtu machoni na kumweleza shida yako basi wewe ni fisi mla mizogoa. Hata huko kwenye mitandao utatakiwa umkabili mtu siku mtakayoonana!


Inawezekana akawa domo zege huyu 😂😂😂 jumaa kareem
 
Inawezekana akawa domo zege huyu  jumaa kareem

Hawa watoto wanakazi kweli kweli. Hawataki kusumbua akili yao ili wajijengee heshima. Wako tayari kuokotwa kama kambale wa masika.
 
Back
Top Bottom