Naweza kujua elimu ya mtu kupitia post zake?

najua tupo kwenye msiba lakini naomba kujua kama naweza kujua elimu au uwezo wa member kwa kusoma post au comment zake'
Nauliza kwa sababu mbili'moja kuna watu humu ndani nitawataja kama nikiruhusiwa'ningependa kuwajua elimu zao'pili mimi ni mgeni nataka nijipange kabla sijajulikana udhaifu wangu'asanteni!

Kumbe unataka kuwajua nidhani ukisoma tu post ya mtu unajua elim yake
 
figganiga, rev masanilo na Director1 hao wana elimu ya juu wamebobea haswa! Lakini Lizzy, sweetlady na kongosho wenyewe wamekalia mapenzi na mahusiano tu...

Hahaha...kweli wewe Mkuu wa Chuo.
Subiri majibu kwa hao uliowataja utakiona cha Mtema kuni.
 
cha ajabu kuna wenye PhD, lakini wanaamini 'Mungu alikamata na kisha akapigwa' tena kwa makosa ya wengine ! Elimu kama hii ina maana kweli !?
Naona unaanza dharau kuhusu imani za watu! Ukae ukijua kuwa katika suala la imani, Prof, Dk, std 7 wote ni sawa mbele za Mungu na wala mbinguni hakuna vyeo kama hivyo.
 
naona watu wameanza kujieleza kuh viwango vyao vya elimu, I thought hoja ilikuwa kama anaweza kutambua elimu ya mtu kupitia post zake, kwa upande wangu nasema unaweza kkutambua kiwango cha uelewa wa mtu kupitia post zake, ila kwa kujua kiwango cha elimu sina hakika kwa sababu elimu na uelewa/ufahamu ni vitu tofauti ingawa kuna ukweli mkubwa kwamba elimu humsaidia mtu/ kumuongezea / kupanua ufahamu wa mtu na mara nyingi waliopata elimu ya darasani huwa na uelewa mpana kulinganisha na wasiopata nafasi hiyo. vpi unataka kuwatumia katika shughuli zako au???

acha uongo
 
Naona unaanza dharau kuhusu imani za watu! Ukae ukijua kuwa katika suala la imani, Prof, Dk, std 7 wote ni sawa mbele za Mungu na wala mbinguni hakuna vyeo kama hivyo.

Vipi kuhusu wale wasomi waliokesha uwanja wa ndege wakitaka biblia iwasafirishe dunia nzima.
 
Mimi huwezi nitambua kwa posts zangu humu Jf, subiri mwisho wa nwezi ninapopeleka fungu la kumi kwa 'nabii' mkuu Mwingira ndio utajua mimi ni mjinga kiasi gani!
 
Mimi huwezi nitambua kwa posts zangu humu Jf, subiri mwisho wa mwezi ninapopeleka fungu la kumi kwa 'nabii' mkuu Mwingira ndio utajua mimi ni mjinga kiasi gani!
 
Naona unaanza dharau kuhusu imani za watu! Ukae ukijua kuwa katika suala la imani, Prof, Dk, std 7 wote ni sawa mbele za Mungu na wala mbinguni hakuna vyeo kama hivyo.
............ Yaaani nalinganisha madrasa na PhD ! ...sasa si unaona hapo ? :yawn:
 
Back
Top Bottom