Naweka sawa nini maana ya Dini na Sayansi

Sahir Punzy

Member
Jan 13, 2015
86
55
Kwanza nianze na hawa watoto wadogo wanaosema ''mimi siamini katika dini bali naamini katika science''

Dini ni nini?

Dini ni njia ya maisha (way of life). Tunaposema njia ya maisha hapa lazima turudi katika msingi wa uwepo wa mwanadamu hapa duniani na ndio walengwa wa dini (mwanadamu katokea wapi?). Kwanza mwanadamu ni kiumbe, na tunaposema ni kiumbe ni kwasababu uwepo wake ni physically
yaani anaonekana na anashikika (hapa sijamaanisha living thing) mfano ukikuta smartphone jangwani basi ujue hiyo itakuwa imeletwa na mtu au ilipeperushwa na upepo kutoka kwa mtu na kufika hapo ilipofika, kamwe haikujitengeneza yenyewe na kukaa hapo.

Kwa hiyo asli ya mwanadamu kuwa yeye ni kiumbe kilichoumbwa, (hapa hatutaji Mungu) kwakuwa yeye ni kiumbe basi lazima atakuwa ameumbwa na muumba, na lazima muumba atakuwa amemuwekea utaratibu wa kuumbiwa kwake, mfano jamii ya ma engineer wa utengenezaji vifaa vya umeme na umeme, Institute of Electrical and Electronics Engineers (IEEE) wamekubaliana kuwa vifaa vyote vya kiumeme vitakavyoundwa lazima viambatanishwe na vitabu vya maelezo ya kifaa husika (user manual).

Hivyo basi Muumba kamuwekea mwanadamu utaratibu wa kuishi wenye kugusa nyanja zote za maisha, na hapa sasa ndipo linapokuja suala la dini, na hapa sasa ndipo watu wanapovutana kuhusu ni ipi dini sahihi? na dini sahihi lazima iguse nyanja zote za maisha na tunaposema nyanja zote za maisha tuna maanisha elimu na siasa na mengineyo.

Elimu

Hapa kwenye elimu sasa ndio watu wanapomkataa Muumba, na kuikubali science, wamesahau kuwa sayansi ni maarifa tu ambayo Muumba amemtunuku nayo mwanadamu ili yamsaidie katika mazingira yanayomkabili, mfano kama tafiti mbali mbali za kisayansi zilizofanikiwa, na tukiona tafiti ambazo hazikufanikiwa basi ujue upeo wetu wa uwezo umefika mwisho na hapa inatakiwa tuache mara moja, mfano mpaka leo science imeshindwa ku retrieve memory ndani ya ubongo wa mwanadamu aliye hai au mfu.

Kwa hiyo hapa tukubali tu kuwa science sio dini wala haifai kuiona kama ndio mkombozi wa maisha ni bali maarifa tu! ya kielimu ambayo humsaidia mwanadamu kutatua matatizo yake ya kidunia, wanaosema wanaamini sayansi na kukanusha dini asli yake huwa hawana elimu kwanza ya science yenyewe na pia hawana elimu ya dini yenyewe.Na ndio maana science inapanda daraja moja hadi jengine kwa sababu ya hitajio la utatuzi wa kimazingira kwa wanadamu. Tujiulize kwanini miaka ya nyuma teknolojia ilikuwa nyuma ukitofautisha na zama zinazokuja, ukichunguza utakuta kuwa katika kila zama watu walitofautiana maumbile ya kijiografia na kibaiolojia.

Siasa

Ama siasa ni neno la kiarabu lenye maana ya kusimamia watu, na tunaposema siasa hapa ndio kwenye mzizi wenyewe wa maisha na Muumba hakutuacha bila ya kutuwekea njia ya maisha. Tunaposema siasa ndani yake tunakuta vitu kadhaa kama elimu,nidhamu ya utawala (serikali), afya, makazi na mengineyo. Kwa hiyo zipo baadhi ya dini zenye kubeba mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu (siasa) na zipo dini zenye mambo ya kiroho tu peke yake (spiritually) bila kujihusisha na siasa na zipo dini ambazo zimejihusisha na mambo ya kisiasa, na hapa sasa ndipo mahala panapofaa mtu kuangalia ni ipi dini iliyotoka kwa muumba iliyo sahihi.

Sipo hapa kuzungumzia dini ipi ni sahihi bali nazungumzia watu ambao wanaokana dini na kukubali science. Kwa hiyo kuna jamii mbalimbali zilikuja na fact mbali mbali kuhusu Muumba, wapo waliosema mwanadamu akishakufa amekufa hakuna chochote, na wapo wanaosema dini zililetwa na wazungu na waarabu, wapo wanaosema dini zisichanganywe na siasa, na pia wapo wenyekuamini uwepo wa Muumba na yeye anakusudi katika uumbaji wa mwanadamu.


Hivyo basi dini na science vyote hukaa pamoja na wala hakuna sababu ya kuvitenga sababu science ni maarifa ambayo huja kwa wakati maalum na pia inaweza kuondoka kulingana na mazingira lakini dini haiwezi kufutika kwa sababu imebeba nidhamu maalumu ya kimaisha ambayo haiwezi kamwe kufutika.

Kwa wenye akili timamu wataelewa.
 
Ukisema Muumba hakujileta ila aliumbwa ni malumbano yasiyoisha milele. Akina Socrates, Plato, Aristotle na wengi waliondoka bila jibu mpaka leo hakuna jibu. Kuna mwanafalsa alisema "unmoved mover " na uishie hapo upambane na hali yako. Kuna vitu vingi vinavyoonekana unapaswa uvijue na kazi yake. Metaphysical issues weka pemveni
 
Kila chanzo kina chanzo chake. Km ambavyo hiyo smartphone haikujileta pale jangwani ndio hivyo na ww umeshindwa kueleza chanzo cha huyo muumba.
 
huoni kama weweumejazwa usanii na wakoloni? maana biblia haijaandikwa na wakoloni ambao wewe wamekujaza conspirancy theories
una tatizo jingine la historia
kasome warumi walivyotawala ancient egypt
kasome the council of nacea chaired by emperor constantine of constantinople
kama hujui kuwa warumi ndio walitunga biblia basi jua kuanzia leo
 
una tatizo jingine la historia
kasome warumi walivyotawala ancient egypt
kasome the council of nacea chaired by emperor constantine of constantinople
kama hujui kuwa warumi ndio walitunga biblia basi jua kuanzia leo
mrumi gani aliyeandika biblia?halafu itakua wewe historia ndio ujui kwani unazijua tawala zilizokua na nguvu kabla ya dola ya kirumi kuwa na nguvu? je biblia wakati huo jiulize ilikua imeandikwa au bado nikiwa na maana agano la kale
 
Back
Top Bottom