Nawaza tu kuhusu TANESCO kwa huu utendaji wao

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Miaka ya nyuma kuwekewa tu simu ya mezani ilikuwa ni issue kubwa unaweza ukazungushwa sana. Mara paaap zikaja simu za mikononi TTCL yale maringo hayapo tena. Shirika la Posta sina ushahidi nalo kuhusu tuhuma za usumbufu mara paaap simu za mkononi kutumiana message sio lazima kuandika barua, siku hizi sekunde moja mtu wa Marekani msiba umetokea kwa Tanzania mtu wa Bukoba ndio anakupa taarifa wewe ukiwa hujui.

Sasa nawazia TANESCO ambao ndio shirika pekee lenye dhamana ya kusambaza umeme, je, kungeruhusiwa kampuni binafsi kusambaza umeme utendaji kazi wao ungekuwaje? Nasikia nchi za Kiarabu unaweza zalisha umeme ukasambaza mitaaani.

Ni mawazo tu TANESCO msichukie mtu hakatazwi kuwaza mnakera sana mtu mita imeharibika badala ya kuja haraka kumwekea nyingine inapita miezi mitatu hamuoni Serikali inakosa mapato?
 
Tanesco ndio shirika lenye kero kuliko yote nchi hii. Juzi nataka kuingiza umeme nyumbani kwangu wanataka 321,000/= na nguzo ipo upenuni mwa nyumba yangu.

Nawauliza hiyo gharama yote ya nini wakati hakuna kitu mnaongezea ,wanasema service line imefanyaje sijui.yani ni usumbufu tu ,kuja tu huyo surveyor mpaka umpe kitu kidogo
 
Hawa tanesco kwa kweli ni shida sana, yaani wanauzi mnoo. Serikali iliangalie hili, jana vitu kibao vimeharibika kwenye friji, umeme umekatika bila taarifa tangu asubuhi hadi jioni, Mimi nipo job, nimerudi Kila kitu kwisheni. Sina hamu nao.
 
Tanesco ndio shirika lenye kero kuliko yote nchi hii. Juzi nataka kuingiza umeme nyumbani kwangu wanataka 321,000/= na nguzo ipo upenuni mwa nyumba yangu.

Nawauliza hiyo gharama yote ya nini wakati hakuna kitu mnaongezea ,wanasema service line imefanyaje sijui.yani ni usumbufu tu ,kuja tu huyo surveyor mpaka umpe kitu kidogo
Acha tu kaka,mimi nimelipia iyo 321,000 plus laki mbili ya nguzo jumla laki 5 na bado nimeambiwa nisubiri ndani ya miezi mitatu!Inasikitisha sana kwakweli,umeme sio anasa ni hitaji la kila mtanzania😔😔.
 
Na fomu nimepeleka toka mwaka jana,yaan mwezi wa 5 tu huu nalala giza.
 
Mimi nimewekewa gharama za kodi 10000 kwa mwezi issue hipo ivi nilikuwa nikijaribu kununua umeme unakataa ikabidi nipige simu tanesco nauliza naambia issue sio wao ni TRA na vipi kuhusu marekebisho wanasema mpk j3 yani Ni mashirika ya ovyo
 
Miaka ya nyuma kuwekewa tu simu ya mezani ilikuwa ni issue kubwa unaweza ukazungushwa sana.Mara paaap zikaja simu za mikononi TTCL yale maringo hayapo tena.Shirika la posta sina ushahidi nalo kuhusu tuhuma za usumbufu mara paaap simu za mkononi kutumiana message sio lazima kuandika barua siku hizi sekunde moja mtu wa Marekani msiba umetokea kwa Tanzania Bukoba ndio anakupa taarifa wewe ukiwa hujui.
Sasa nawazia TANESCO ambao ndio shirika pekee lenye dhamana ya kusambaza umeme je kungeruhusiwa kampuni binafsi kusambaza umeme utendaji kazi wao ungekuwaje? Nasikia nchi za Kiarabu unaweza zalisha umeme ukasambaza mitaaani.
Ni mawazo tu TANESCO msichukie mtu hakatazwi kuwaza mnakera sana mtu mita imeharibika badala ya kuja haraka kumwekea nyingine inapita miezi mitatu hamuoni serikali inakosa mapato?
Niko chimbo namalizia project ya Tesla ya free energy soon mtadaka umeme kwa wireless.
Ni bure maana the universe is full of free energy.
Unasubscripe kila mwez na matumizi ni unlimited
 
Tanesco ndio shirika lenye kero kuliko yote nchi hii. Juzi nataka kuingiza umeme nyumbani kwangu wanataka 321,000/= na nguzo ipo upenuni mwa nyumba yangu.

Nawauliza hiyo gharama yote ya nini wakati hakuna kitu mnaongezea ,wanasema service line imefanyaje sijui.yani ni usumbufu tu ,kuja tu huyo surveyor mpaka umpe kitu kidogo
Magufuli mlisema ni dikteta
 
Aya acha kuwaza sasa.
ata wao pia wanajua wanafanya madudu na kama wakiruhusu ushidani bas shirika lao litakufa kama TTCL ilivyo hiv sasa.
 
Sasa kama Waziri aliyepewa hilo shirika anawaza eti atakuja kuwa Rais wa nchi unategemea nini? kajamaa kale hakuna kitu kabisa afadhali ya Kalemani alikua na kauweledi kidogo, ukishaona waziri anahangaika na vitengo vya mawasiliano kwamba havifanyi kazi ipasavyo ndio maana umeme unakatika katika na huduma zinadhorota kwa ujumla huyo ujue ni kiazi, tena mviringo kabisa . Mi sijui hizi teuzi zinaangaliaga nini, any way haya bana
 
Acha ndugu,sababu umeme umeshafika mtaani kwangu nikajua haitachukua mda nitaunganishiwa...TANESCO wanatudharau walalahoi na wala hawajali chochote.
Ungeongoza 100k hapo ukanunua solar lako watt 100 betri N 90 taa plus nyaya sasa hivi ungekuwa unaenjoy umeme wako usiokatiks 24/7
 
Sieijii amesemaje kuhusu hilo shirika kwani? Mama naye anasemaje?

Kwani haya mambo si nasikia yaliisha tangu March 17, 2021?

Sasa hivi watumishi wana nidhamu ya kutokea mioyoni wamesema!

Au wateja sasa ndio mmekuwa na nidhamu ya uoga?
 
Back
Top Bottom