Nawaza sana mimi, hivi ingekuwaje ?!

Nawaza sana mimi, hivi ingekuwaje ?!

Kwanza nimshukuru sana Mungu kwa kua kweli naamini mke mwema hutoka kwake hakika. Nilishakua na wanawake chungu nzima wakila sampuli wanene wembamba, warefu wafupi, weupe weusi lakini wewe mke wangu kweli ni wakipekee sana.

Nakupenda pasina mfano mke wangu kipenzi mama Adrian wewe ni chemchem ya furaha ndani ya roho na nafsi yangu ila nina maswali mengi sana na sina majibu sijui ingekuaje ??

Hivi ingekuaje kama ungekua kama hawa wadada wa mjini waliojaa tele ambao wao full kudanga, hivi ingekuaje ?!

Najiuliza vipi ungekua kama hawa wa makope bandia na mawigi, hivi ile style yangu nayokukamataga na kuzivuta nywele zako asili huku nimekubana barabara hivi ungekua mvaa mawigi yangekua yanachomoka hivi ingekuaje, tungekua tunaendelea au tunasubiri uvae kwanza tena ?!

Napenda navyorudi nyumbani toka job nakuta umeniandalia misosi nakula chakula chako hivi ingekuaje kama na wewe ungekua hawa wa "wanawake pia tunaweza" natoka kazini sikukuti home bado uko "kazini" unamalizia kazi ulizopewa na "bosi" hivi ningefurahia chakula alichopika house girl kwa mamna navyofurahia chakula chako ?! hivi ingekuaje ?!

Tunapolala najisikia vzuri unapojisogeza na kujilaza kifuani kwangu nikukumbatie, hivi ingekuaje kama ungekua kama hawa wanawake wa mashindano na magumbu na visasi hivi ingekuaje ?!

Tunapopishana unajishusha mpaka vumbi litulie ndo unanieleza kwa heshima na upendo na unyenyekevu upande wako, hivi ingekuaje ungekua aina ya wanawake wa kileo ngangari jino kwa jino full matarumbeta, hivi ingekuaje ?!

NAKUPENDA kwa mengi sana mke wangu, unajua napenda sana unaponikumbusha kusali kabla ya kulala, hivi ingekuaje ungekua type ya wanawake hawa waliojaa tele mjini wa movie za series mpaka usku wa mamane hivi ingekuaje ?!

Hebu subiri, kila neno baya unalosikia kuhusu mimi mengine hata hua ni kweli nimefanya ila daima unanitetea na kukataa kua mimi siwezi kufanya baya lolote, hivi ingekuaje kama ungekua aina ile ya wanawake wa kupokea maneno hivi ingekuaje ?! Sasa hivi najitahid kutunzia heshma yako mke wangu kwa maana kwa kweli unastahili kutunziwa hesma.

Wewe na mwanetu Adrian ndo mnanipa nguvu ya kuzisaka hizi pesa popote zilipo, hivi ingekuaje ningekukuta ulishazalishwa na "mwanaume mwingine" hivi ningempenda huyo mtoto pia kwa dhati au ningekua na neno juu yake ?!

Nakiri tabia yako yakutokua mpenda mitandao kweli inanipendeza, hivi vipi ungekua kila muda ni facebook upo, twiter haukosekani, instagram inakusubiri bado snapchat matakataka zote uto hivi ingekuaje kwanza hata jf huna time nayo, hivi ingekuaje ungekua kama Faiza Fox kutwa mitandaoni kujibazana na kubishana na wanaume hivi ingekuaje, ningeona sawa tu au nisingependezwa na je ingekuaje ?!

Hivi ingekuaje na wewe ungekua kama wanawake wa "haki sawa" mimi nikitoka na wewe unatoka mwanamke unarudi muda utakao hivi ingekuaje, unajua nakupenda kwa mambo mengi hata hili la kuomba ruhusa kila unapotaka kutoka.

Wewe inawezekana hujui tu mke wangu ila pia napendezwa na hulka yako ya kutaka kujua maoni yangu juu ya kila jambo upangalo hivi ingekuaje kama ungekua aina ya wanawake wanajiita "indpendent women" wao na maamuzi yao wana msemo wao "usinipangie" hivi ningeridhika na hali hyo je nisingeridhika ingekuaje ?!

Napata amani kwa jinsi ulivyo muwazi kwangu mpaka najistukia kua nakunyima privecy, hivi ingekuaje ungekua aina ile ya wanawake simu ina password ndefu kama mkojo wa mlevi na pattern juu na finger print lock hivi ningekua na amani au ningejifanya kua ninayo amani, je ningekua na vijimawazo kua unajambo baya huko ndani ya mapassword na mapatten au ingekuaje ?!

Mwisho naapa kufanya kazi kwa juhudi na unajua najituma sana wewe na mwanangu msipungukiwe jambo liwalo lolote, hata hali iwe ngumu vipi daima mtakua na ziada, tangu nikuoe sijapata kukuona ukitoa chozi na kamwe sitaruhusu utoke chozi kwa sababu yoyote na kama hyo haitoshi hautatoka jasho wewe ni malkia wangu.

Mmmh ila pia hivi ingekuaje kama nisingekuoa mimi ukaolewa na njemba nyingine, hivi ingekuaje ?!
ni jambo jema kumsifia mkeo ila kuwa makini sana maana hata Biblia inasema tuishi nao kwa akili
 
itapendeza sana mkuu ila ni vizuri tumuone na sisi wana jamvi ili tumpe sifa zake
 
imefikia hatua, mtu akileta habari nzuri kuhusu ndoa watu wanachukia, wanaponda na kutoa maneno ya kashfa. sio dalili njema!
Ni kweli mkuu,,,yaani wanataka mtu aje analia huku anaomba msaada kuhusu ndoa ndio waanze kutoa mawazo yao ambayo mengi yanakua Ni ya kinafiki,, ilah good news kuhusu ndoa,,hawaziami kabisa,,na wengine wanaishi kuzikejeli TU.

Haipendezi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app,using POP 2 power
 
Huyo ni malaika kabisa eti kila kitu yuko perfect aargh, mimi ni binadamu siwezi kuwa kama yeye[emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
Mabinti wa uswahilini lazima mumuone mama Adrian kama malaika maana huko uswahilini kiukweli hapawezi kutoa mke bora. Vigodoro kila kukukicha bikra zinatolewa darasa la pili, watoto wadogo full kudanga sasa mke bora kama mama Adrian apatikane vipi hapo
 
Mabinti wa uswahilini lazima mumuone mama Adrian kama malaika maana huko uswahilini kiukweli hapawezi kutoa mke bora. Vigodoro kila kukukicha bikra zinatolewa darasa la pili, watoto wadogo full kudanga sasa mke bora kama mama Adrian apatikane vipi hapo
Sawa kaka wa uzunguni, siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom