KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,182
Hata kama sio viongozi mliopo hivi sasa kwenye ngazi ya uongozi wa Jiji, swali hili linawahusu na ikiwapendeza jaribuni kulifikiria na kulifanyia kazi, kubadili au kupunguza heshima kubwa anayopewa kiongozi huyu kwa kutambuliwa kwa hadhi asiyoistahili kwa uongozi wake hapa nchini, Afrika Mashariki na Afrika.
Barabara muhimu sana katika Jiji hili yenye urefu na mandhari nzuri kupewa jina la kiongozi ambaye haijulikani alilifanyia nini Jiji, Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kunaibua maswali juu ya heshima hiyo anayopewa; na hasa ikizingatiwa kwamba Mwasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere yeye hakupewa heshima kama hiyo huko alikotawala kiongozi huyu. Ukitafuta barabara aliyopewa Julius Nyerere nchini Kenya utaikuta uchochoroni, si Nairobi pekee, bali hata katika miji mikubwa mingine kama Mombasa, Kisumu na kwingineko.
Swali ni hili: Ilikuwaje hadi barabara kubwa ya kuingilia Jijini akapewa Jomo Kenyatta, barabara inayochukua urefu mkubwa na kwa miaka ijayo eneo lote la kandokando ya ziwa inakopitia barabara hii litakuwa la kuvutia sana kwa Jiji hili?
Kuna jambo lipi muhimu alilolifanya kwa Jiji kiasi cha kupewa jina la barabara kuu ndani ya Jiji?
Nimetafuta barabara yenye jina la Sokoine, Kawawa, au Mkwawa hapa Jijini siyaoni. Milton Obote iko wapi? Samora Machel, Kenneth Kaunda, siwaoni!
Pendekezo: Badala ya kumpa barabara yote tokea huko nje ya mji hadi mjini kwenyewe; kama inalazimu aendelee kuwepo kwenye barabara hiyo, basi mwisho wake iwe toka mjini hadi Mkuyuni; kama siyo Igogo, na mtu mwingine apewe barabara inayokwenda hadi Nyegezi.
Kama hamtaafiki ushauri huu, italazimu pawepo 'petition' ya kuliondoa kabisa jina la huyu kiongozi ambaye hakuifanyia lolote Tanzania, Afrika Mashariki na hata Afrika. Inafahamika wazi kwamba huyu ndiye aliyekuwa kikwazo kikubwa katika ukombozi Kusini mwa Afrika, na alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuvunjika kwa ushirikiano wa Afrika Mashariki wa mwanzo.