Nawauliza Viongozi wa Jiji la Mwanza

Nawauliza Viongozi wa Jiji la Mwanza

Kwani hukusoma niliyoandika kuhusu Jomo Kenyatta kutostahili kupewa heshima hiyo?

Hebu tueleza ya huyo "ZONGII" kama naye alisukumizwa tu heshima aliyopewa bila ya kuwa na vigezo stahiki.

Mimi sijui "ZONGII" anasifa gani kwani simjui, lakini Jomo Kenyatta najua mengi yanayomhusu, na karibu yote hayampi sifa za kuwa kwenye barabara muhimu kama hiyo iliyopo Mwanza.
Kwani kuna vigezo ambavyo vimeainishwa na kuorodheshwa mtu anatakiwa awe navyo ili barabara iitwe jina lake?
Mwai Kibaki na hata Barack Obama walipewa barabara na Rais, vigezo gani hao watu wanavyo ambavyo Jomo Kenyatta hana?
 
Hoja nyingine bana
Basi Kama vipi na mimi nihoji hospital yetu pendwa sekouture ametufanyia la ajabu lipi hadi jina lake litumike kuitambulisha hospital yetu kubwa
 
Wewe ni mtoto unanukia maziwa mdomoni hujui kwa nini nyerere alilipa jina barabara hiyo jina la kenyatta
 
Hapa ndipo inapoonyesha kuwa hujui lolote kuhusu haya mambo.

Kwa hiyo, Rais aliamka tu na kuwapa hao watu barabara bila hao watu kuwa na vigezo?

Kama ungekuwa mtu makini huu mfano uliouweka hapa, wa Barack Obama na Mwai Kibaki ndio ungekufanya uone mantiki ya mada iliyoletwa hapa; lakini badala yake unautumia kuvyako tu bila ya kuweka tafakuri.

Inaelekea hukuelewa mada iliyowasilishwa hapa, kwa hiyo nakushauri ukaisome tena na uielewe inaeleza nini.
 
Tuonyeshe ushahidi wa hilo, la "Nyerere alilipa jina barabara hiyo jina la Kenyatta". Kwa hiyo baada ya kumpa Kenyatta barabara hiyo muhimu mjini Mwanza, Kenyatta akaenda kulipa fadhila kwa kumpa 'uchochoro' mjini Nairobi? Huoni dhihaka hiyo?

Na hata kama ingekuwa kweli, kwamba Mwalimu Nyerere ndiye aliyependekeza ipewe barabara hiyo jina la Kenyatta, barabara hiyo ilikuwa inaishia Igogo, kwa maana ya kuwa mjini na wala sio kwenda hadi mashambani Nyegezi kwa wakati huo. Kwa nini sasa iendelee, itaendelea hadi wapi Shinyanga?

Na kuhusu hili la "Wewe ni mtoto unanukia maziwa mdomoni"; inaonyesha kuwa uzee ulionao haukusaidii kitu kwa sababu hujui kwamba mambo haya yanawekewa kumbukumbu/historia, na hata kama ningekuwa "mtoto" kama unavyodai, hilo lisingekuwa jambo la kuzuia nisijue historia ya mji huo wa Mwanza.

Basi, ngoja nikupe fursa ya kuheshimu 'uzee' wako: tueleze hiyo barabara kabla ya kuitwa Kenyatta ilikuwa na jina gani?
 
Hoja nyingine bana
Basi Kama vipi na mimi nihoji hospital yetu pendwa sekouture ametufanyia la ajabu lipi hadi jina lake litumike kuitambulisha hospital yetu kubwa
Sekou Toure alikuwa rafiki yetu mkubwa. Jina hilo lilipewa hospitali hiyo wakati wa ziara aliyofanya hapa nchini, na hospitali ndio kwanza ilikuwa imejengwa. Ilikuwa haijapewa jina. Unajua aliyeizindua hospitali hiyo?

"Hoja nyingine bana"? Unauliza au unaona ajabu? Wewe huna ufahamu wa haya mambo ndio maana unashangaa kuwepo kwa mada kama hii.
Na kwa kukustua akili kidogo, hebu kumbuka hospitali kubwa kabisa nchini, ile inayoitwa sasa Muhimbili, unakumbuka ilikuwa inaitwa jina gani kabla ya kuwa Muhimbili?

Sasa kama ni "Hoja nyingine bana", umewaza kwa nini sasa inaitwa Muhimbili?
 
Hapa ndipo inapoonyesha kuwa hujui lolote kuhusu haya mambo.

Kwa hiyo, Rais aliamka tu na kuwapa hao watu barabara bila hao watu kuwa na vigezo?

Kama ungekuwa mtu makini huu mfano uliouweka hapa, wa Barack Obama na Mwai Kibaki ndio ungekufanya uone mantiki ya mada iliyoletwa hapa; lakini badala yake unautumia kuvyako tu bila ya kuweka tafakuri.

Inaelekea hukuelewa mada iliyowasilishwa hapa, kwa hiyo nakushauri ukaisome tena na uielewe inaeleza nini.
Hahahah! Unadought kwamba rais aliamka tu na kuwapa hao watu barabara, lakini umemeshindwa kuwaza je hao viongozi walimpa Kenyatta hiyo barabara waliamka tu na kumpa! [emoji3][emoji3][emoji3] Very interesting
 
Na hata kama ingekuwa kweli, kwamba Mwalimu Nyerere ndiye aliyependekeza ipewe barabara hiyo jina la Kenyatta, barabara hiyo ilikuwa inaishia Igogo, kwa maana ya kuwa mjini na wala sio kwenda hadi mashambani Nyegezi kwa wakati huo. Kwa nini sasa iendelee, itaendelea hadi wapi Shinyanga?

Eti barabara ilikuwa inaishia igogo!! Kwa hiyo hapo kabla watu wa Nyegezi, Missungwi na Shinyanga walikuwa wanapita barabara gani kuja Mwanza mjini?
 
Bora hiyo bara bara ipewe jina la moja wa wazazi wake mzalendo no1.
 
Eti barabara ilikuwa inaishia igogo!! Kwa hiyo hapo kabla watu wa Nyegezi, Missungwi na Shinyanga walikuwa wanapita barabara gani kuja Mwanza mjini?
Wewe naona siwezi kukusaidia, maana hata kusoma na kuelewa huwezi. Mji wa Mwanza ulikuwa umeenea hadi Nyegezi wakati barabara hiyo inapewa jina?

Ni wapi nilipoandika kwamba hapakuwa na barabara iendayo Nyegezi.
Kwa hiyo kwa kuwa barabara hiyo inakwenda hadi Misungwi, Shinyanga na hadi Dar, kote huko unataka ijulikane kwa jina la huyo babu yako Kenyatta?

Hivi ngoja nikuulize, inawezekana mtu kama wewe ndio hao waliomo kwenye uongozi wa Jiji? Kama hivyo ndivyo, basi ni hasara tupu! Maana huelewi kitu kabisa.
 
Wewe naona siwezi kukusaidia, maana hata kusoma na kuelewa huwezi. Mji wa Mwanza ulikuwa umeenea hadi Nyegezi wakati barabara hiyo inapewa jina?

Ni wapi nilipoandika kwamba hapakuwa na barabara iendayo Nyegezi
Hivi ngoja nikuulize, inawezekana mtu kama wewe ndio hao waliomo kwenye uongozi wa Jiji? Kama hivyo ndivyo, basi ni hasara tupu! Maana huelewi kitu kabisa.

Hahahah! Umesahau ulisema barabara ilikuwa inaishia igogo?! Ngoja tu nikutoe ujinga bwana mdogo, hiyo barabara haijawahi kuishia igogo
 
Hahahah! Unadought kwamba rais aliamka tu na kuwapa hao watu barabara, lakini umemeshindwa kuwaza je hao viongozi walimpa Kenyatta hiyo barabara waliamka tu na kumpa! [emoji3][emoji3][emoji3] Very interesting
"...unadought", ndiyo kitu gani hicho?

Mada imeeleza wazi kwa nini Jomo hastahili kupewa heshima kubwa inayoendana na hadhi ya barabara hiyo kuuu kabisa mjini Mwanza. Kama unaona hoja zilizowekwa hazimstahili, andika juu ya hilo, sio kuzungukazunguka tu bila mwelekeo wowote. 'In fact' sasa unani-bore'.
 
Hahahah! Umesahau ulisema barabara ilikuwa inaishia igogo?! Ngoja tu nikutoe ujinga bwana mdogo, hiyo barabara haijawahi kuishia igogo
Wewe ni mpuuzi, zaidi ya kuwa mjinga tu.
Barabara itaishiaje Igogo. Tunazungumzia mipaka ya mji ambako ndiko barabara zilikuwa zinapewa majina. Viongozi wa mji wa wakati huo wasingezipa barabara zilizoko nje ya mji majina. Hawakuwa na mamlaka hayo. Hili nalo ni jambo la kutaka ufafanuliwe?
 
"...unadought", ndiyo kitu gani hicho?

Mada imeeleza wazi kwa nini Jomo hastahili kupewa heshima kubwa inayoendana na hadhi ya barabara hiyo kuuu kabisa mjini Mwanza. Kama unaona hoja zilizowekwa hazimstahili, andika juu ya hilo, sio kuzungukazunguka tu bila mwelekeo wowote. 'In fact' sasa unani-bore'.
Mada imeeleza au wewe usiyejua kitu ndo umeeleza!! Ili ujue kwamba ulichoeleza hakina mashiko ebu soma comments za wachangiaji.
 
Wewe ni mpuuzi, zaidi ya kuwa mjinga tu.
Barabara itaishiaje Igogo. Tunazungumzia mipaka ya mji ambako ndiko barabara zilikuwa zinapewa majina. Viongozi wa mji wa wakati huo wasingezipa barabara zilizoko nje ya mji majina. Hawakuwa na mamlaka hayo. Hili nalo ni jambo la kutaka ufafanuliwe?
Kwa akili yako finyu unadhani uongozi wa mji wa Mwanza kwa wakati huo kimamlaka ulikuwa unaishia igogo tu!!
 
Mada imeeleza au wewe usiyejua kitu ndo umeeleza!! Ili ujue kwamba ulichoeleza hakina mashiko ebu soma comments za wachangiaji.
Sijaona mchangiaji aliyetoa maoni kukanusha niliyoandika ndani ya mada. Kwa hiyo huwezi kuhitimisha kuwa "...ulichoeleza hakina mashiko."
 
Kwa akili yako finyu unadhani uongozi wa mji wa Mwanza kwa wakati huo kimamlaka ulikuwa unaishia igogo tu!!
Huna lolote la maana katika mjadala huu. Ni bora niachane na wewe.
 
Back
Top Bottom