Nawatakieni Kwaresma Njema

Nawatakieni Kwaresma Njema

Amina sana, mwezi huu tujizuie kidogo hata kuangalia picha chafu na zisizo na maadili, maneno mabaya kwa wenzetu, kunywa pombe na mengineyo yasiyompendeza Mungu.

Huu ni mwezi mhimu sana kwa Wakiristo.

Tusali, tutubu na tuiamini injili!

Ni kweli mkuu lakini tujitahidi kuishi maisha matakatifu siku zote za maisha yetu. Yaani tuzifanye siku zote ziwe kama kwezi huu ili MUNGU aweze kutusaidia kuyashinda majaribu ya dunia hii
 
Nawe pia kbm
 
Last edited by a moderator:
Amina Sana wakuu Mungu atuongoze katika hili
 
Amina,..mkuu nami ndo nimetoka kwenye misa na nimeshapaka majivu...Tutubu na kuiamini injili..
 
Hii inawahusu makafiri tu.

Ndugu yangu ungekaa kimya ungepungukiwa nini labda . Mungu aliyekuumba wewe ndiye aliyeniumba mimi. Tofauti yetu ni ipi labda ..?? Halafu tukisema akili yako inaendeshwa na mashetani tutakuwa tunakosea. Je tangu hii thread imeanzishwa kuna sehemu umetukanwa au umekosolewa dini yako..?? Najifikiri wewe utakuwa under 21 sio bure mtu mwenye akili yake hawezi kupost takataka kama yako.
 
Ndugu yangu ungekaa kimya ungepungukiwa nini labda . Mungu aliyekuumba wewe ndiye aliyeniumba mimi. Tofauti yetu ni ipi labda ..?? Halafu tukisema akili yako inaendeshwa na mashetani tutakuwa tunakosea. Je tangu hii thread imeanzishwa kuna sehemu umetukanwa au umekosolewa dini yako..?? Najifikiri wewe utakuwa under 21 sio bure mtu mwenye akili yake hawezi kupost takataka kama yako.

uongo mbaya huwa nakereka sana na hili neno lao...nashangaa sana mtu kumuita mwenzake kafiri na huku hawezi kufanya chochote cha tofauti( unamuita mwenzio kafiri na huku huijui kesho)
 
Asante sana kwa salamu nzuri na tamu katika mwezi huu wa Rehema. Nami nasema Asante Yesu kunipa tena nafasi ya kutengeneza maisha yangu kwa upya
 
kila la kheri ndg zangu...nawatakia mfungo mwema tuombeane kheir In Shaa Allah
 
Amana, tuwe na toba ya kweli katika kipindi hiki.
 
Uzuri wa dini yetu, funga yetu haimkwazi mtu, we kula pembeni yangu, wala sitakwazika ndo kwanza nachukulia ka majaribu, na ninatakiwa kupambana ili kuishinda nafsi ya tamaa.
 
Tumeanza safari yetu ndefu na muhimu sana ya mfungo wa siku arobaini (mfungo wa Kwaresma), tunayoianza siku ya Jumatano ya majivu (leo).

Katika kipindi hiki cha siku 40, mama Kanisa anatualika sisi sote kushughulikia kwa jitihada kubwa zaidi uongofu wetu sisi wenyewe.

Masomo matakatifu pamoja na tafakari nyingi, zitatuelekeza kujitafiti katika roho ya ukweli wa ndani, tujifahamu tulivyo ili tujirekebishe pale ambapo hatukwenda sana na tujiimarishe zaidi pale ambapo kwa neema ya Mungu tuliweza kwenda sawa. Daima sote tunaalikwa kuongeza na kuimarisha maisha ya fadhila mbalimbali.

Kwaresma ni kipindi cha kujipatanisha kwanza na nafsi zetu. Kuna nyakati tumejitendea mambo makubwa maovu sana, hata tukaanza kujichukia sisi wenyewe, tumejikatia matumaini, tunajiona hatufai tena na tunahisi kuwa hatupendwi na wenzetu.

Hatua ya kwanza ya wongofu ni kujifahamu, pili ni kujikubali na tatu ni kuwa tayari kujisamehe na kujirekebisha. Acha ya kale, anza upya, songa mbele.

Kwaresma ni kipindi cha kumrudia Mungu kwa mioyo yetu yote. Kwa kinywa cha Nabii Yoeli mwenyewe asema “...nirudieni mimi kwa moyo wote, kwa kufunga, kulia na kuomboleza” Yoel 2:12.

Katika roho ya ukweli wa ndani, kila mmoja katika familia anajua ni namna gani amejiweka mbali na Mungu, na kwa kitendo cha kuwa mbali na Mungu, wewe katika familia umekuwa ndio uchochoro wa shetani, anayeingia katika familia ili kuivuruga. Bwana akuita kwa upole, asema nirudieni mimi kwa moyo wote.

Kwaresma ni kipindi cha kutoa sadaka sana, kusali sana kwa moyo wa toba ya ndani na kufunga (Rej. Mt. 6:1-6, 16-18). Hii ni sehemu ya habari njema inayosomwa siku ya Jumatano ya Majivu. Katika sehemu hii Bwana anatupatia nidhamu ya kutoa sadaka, kusali na kufunga ili kweli tupate mafaa ya kiroho. Na sisi kama familia tunapenda kwaresma hii tuwe na sadaka ya pamoja kama familia, tuwe na sala za pamoja zaidi na tuuchukue mfungo huu kwa pamoja.

Wataalamu wa mambo ya roho wanatuambia, kufunga ni namna bora zaidi ya kufanya kitubio na kujipatia nguvu mpya ya roho.

Kwa ujumla wake katika kipindi hiki cha Kwaresma, sisi wana kanisa la nyumbani yaani familia, tutatafakari sana juu ya tunu za toba na msamaha.

Tutakiri kwamba, katika familia zetu mara nyingi tumekoseana na kujeruhiana vibaya sana, kiasi kwamba tumeathiri vikali ule UZURI wa maisha ya ndoa na familia. Kwa matendo yetu tumeifukuza haki, tumefukuza upendo, tumefukuza amani na furaha ya familia. Dawa yetu ni mmoja tu – toba na msamaha, tufanye toba ya kweli, tusameheane na tuwe tayari kujirekebisha kabisa.

Familia nyingi zimekonda na kunyauka vibaya, hazijui tena kicheko wala tabasamu, wala utani kwa sababu wanashindwa kuombana msamaha wa kweli na kusameheana. Wengi wanapenda zaidi maisha ya ubabe na umame ambayo hayajengi familia kamwe.

Ugangwe, jeuri, kiburi na roho mbaya vinaelekea kutawala katika familia zetu!! Vilio vimezidi katika Kanisa la nyumbani. Nani anyamazishe? Ni MIMI NA WEWE.

Baba Mtakatifu Fransisko anatufundisha, maneno matatu yanayoifanya familia isonge mbele ni NAOMBA, SAMAHANI na ASANTE. Katika Kwaresma hii tutalitafakari sana hilo lihusulo KUOMBA MSAMAHA, KUTUBU KWA MANENO NA VITENDO, na KUFANYA JITIHADA YA KUJIREKEBISHA. Usijitese kwa kutokuwa tayari kutubu, na usijiangamize kwa kutokuwa tayari kusamehe.

Mume jipatanishe na mkeo, mke jipatanishe na mumeo, wazazi jipatanisheni na watoto wenu, watoto, jipatanisheni na wazazi wenu. Msamaha na mapatano mema VINAWEZEKANA. Bwana Mungu atuumbie mioyo safi na atengeneze tena roho thabiti iliyotulia ndani mwetu.

Tunawaweka mikononi mwa Mungu na tunawatakieni nyote Kwaresma njema.

Mwenyezi Mungu Awabariki Nyote...

Unafiki Mtupu! Tunamjua Mungu KINYAKATI Tu.
 
Back
Top Bottom