Nawatakieni Kwaresma Njema

Nawatakieni Kwaresma Njema

Nadhani wewe ni mwehu kabisa wewe una uhakika gani kama dini yako sio kafiri ila mkristo ndio kafiri kuwa makini unapochangia jf
 
Amen mkuu. Pia naamini itakuwa vyema saana kama tutatumia kipindi hiki kwa kumlilia Mungu wetu (Yahweh,Jehova) ili Roho Mtakatifu atuongoze watanzania wote kujiandaa vyema kwa kutuelewesha namna ya kufanya uchaguzi mwema na kupata viongozi ambao wana hofu ya kweli ya Mungu.
Nawatakia Wakristo wote na wasio Wakristo Kwaresma Njema,yenye baraka tele na matokeo hasi.
 
Wakristo Wote Na Tunaomjua Mungu ( Gentamycine Nikiwemo ) Kuanzia Leo Tunaanza Funga Yetu Ya Kukaa Njaa Huku Tukitaabika Na Ugumu Wa Maisha Na Hapo Hapo Matishio Ya Ugaidi Yakizidi Na Presha Za Kisiasa Nazo Zikipamba Moto. Hivyo Ombi Langu Naomba Kuanzia Leo Baada Ya Siku 40 Kuwe Na Ceasefire Ya Matusi, Kashfa, Shutuma Na Nyodo Humu JF Ili Tuweze Kumtumikia Vizuri Mwenyezi Mungu Na Tupate Thawabu.

Hivyo Nitakachokifanya Mimi Kama Mimi Kuanzia Leo Nitakuwa Napitia Post Zenu Wote Na Haswa Wale WATUKUTU Humu JF Na Nikigundua Kuwa Muda Wote Huu Wa Mfungo Hawajaenda Kinyume Na Hayo Mambo Hapo Juu Nitawapa Zawadi Zao Nzuri Tu Na KtK Hili Nipo Very Serious Na Nitaomba Mods Nanyi Pia Mnisaidie Kuniteulia Hao Watukutu Maarufu Humu JF Ambao Nina Uhakika Mnawajua Na Naomba Wawe Watano ( 5 ) Tu Na Ikithibitika Hao Members Watukutu Humu Muda Wote Huu Wa Kwaresma Wameishi Kwa Kumpendeza Mungu Nitawapa Zawadi Nzuri Ya Pasaka Na Itapitia Kwenu Mods Na Wamiliki Wa JF :smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:.
 
Mwenyeezi Mungu anapenda tendo la "Mfungo huu adhimu"

Tunawatakieni kwaresma njema ikubaliwe na ibarikiwe na Moula-karimu.

Kwa Amani na pongezi tumshukuru Mwenyeezi mungu kuunganisha Mema miaka Yote. AMIN
Good Luck and Blessings.
 
Mungu atubariki na atupe nguvu ya kufunga kiroho kwa siku zote arobaini kama kiongozi wetu YESU alivyotuagiza,atujalie tujue maana halisi ya kwaresma katika kuelekea sikukuu ya pasaka
 
Amina, tumwombe roho mtakatifu atuongoze katika kutenda mema kipindi hiki cha kwaresma na Siku zote za maisha yetu.
 
Kwaresima inaanza Leo kwahiyo tunakila sababu ya kumshukukuru mungu

Amina na tukumbuke huu ni mwaka wa uchaguzi katika funga tuombe Mwenyezi Mungu awatie nguvu makanda wote wapenda haki, wachukia dhulma awape wepesi katika kazi zao na awafunge ufahamu wadhumu wote, mafisadi washindwe na walegee.
 
kwa kweli ni safari ya matumaini, tumwombe ROHO MTAKATIFU atuongoze
 
Mungu atuongoze na hasa kipindi hiki taifa letu linapojiandaa kupita katika vipindi mbalimbali ikiwemo uchaguzi ufanyike kwa amani na Mwenyezi Mungu atujalie amani yetu ambayo tumekua nayo miaka yote isitetereke bali iwe ya kudumu. Pia Mungu wetu atujalie viongoz waadilifu akiwemo Raisi ambae atatuongoza vema
Amina!!!!!
 
Ni Jumatano ya majivu tena mwaka huu wa 2019.Nawatakia wote Kwaresma njema na mfungo wa Siku 40 katika kushiriki mateso ya Bwana wetu yesu kristo,kutubu dhambi zetu na kumrudia Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom