Nawahusia wanangu, mshindeni shetani - Rais Magufuli

Nawahusia wanangu, mshindeni shetani - Rais Magufuli

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1087470


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Teknolojia Mbeya (MUST), Mzumbe na Saint Augustine (SAUT) kutekeleza majukumu yao kwa haki na kutumia muda ipasavyo.

Rais Magufuli ameeleza hayo katika Chuo cha MUST baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa maabara ya chuo hicho, jijini Mbeya, leo.

Amewaonya madhara ya kuendekeza ngono vyuoni kwani mbali na kufeli masomo, wanakuwa hatarini kupata magonjwa ya zinaa na Ukimwi"Nawahusia wanangu, mshinde shetani.

"Najua majaribu ni makubwa inabidi niwaambie najua hamjazoea hilo,"alisisitiza Rais Magufuli. Hata hivyo, amewataka wahadhiri kutenda haki kwa kutowakosesha wanafunzi maksi wanazostahili ili wafeli.

"Walimu mtende haki kwa wanafunzi msije kuwanyima maksi ili mbembelezwe, mtabembelezwa na wangapi,"Rais alihoji huku wanafunzi wakionekana kufurahia.

Rais amehitimisha ziara yake ya siku tisa mkoani Mbeya baada ya kuzungumza na wananchi na kuzindua miradi ya maendeleo huku akiwawataka viongozi kutenga siku maalum ya kutatua kero zinazowagusa wananchi moja kwa moja.
 
Yeye mwenyewe Mke wake alimpatia chuo ,,aache vijana wale ujana na wao.
 
....Wanafunzi wa vyuo ndo mabingwa wa kudanga. Hivyo kuacha ngono ni sawa na kwenda msibani alafu huna nauli ya kurudia mkoani.
 
Mkuki kwa nyani.....? Lskini kwa binadamu.....?
 
Back
Top Bottom