Navunja ndoa ya mtu!!!!

Kweli kaka lakini pia amesahau kwamba simu ya mkewe si ya kwake, hatakiwi kuipokea mkewe akiwepo. ninaamini asingepokea yote haya yasingetokea
Wanaume tunadhani kuwa ukioa tu ndio unakuwa na mamlaka ya kufanya lolote kwa mwenza wako,mbaya zaidi alidhani mkewe kazini anafanya kazi na wanawake wenzake peke yake bila wanaume kitu ambacho anashindwa kuelewa kuwa huwa inafikia kipindi masuala ya kazini hulazimika kuja mpaka nyumbani kwa dharula.

Mimi simu ya mke wangu sina haja nayo na nikitaka kumfuatilia si mpaka nisubiri apigiwe simu kuna mbinu nyingi tu za kufanya,huyu jamaa kachemka sana.
 

unachoweza kufanya ndugu yangu Mvaa Tai nikumuomba uyo dada awatafute rafiki wa karibu wa mme wake awaeleze jambo lenyewe ili waweze kumsaidia kwa mumewe,ikiwezekana jambo hili unaweza ata kuwashirikisha ndugu na jamaa zako wa karibu ili kuhakikisha jambo hili linamalizika kwa amani na sio kwa visasi na kukomoana,wewe mwenyewe una familia yako una watu wengi tu wanakutegemea,embu fikiria jambo baya likikutokea utakua umewaweka ktk kundi gani hao ndugu zako hapo juu?
 
Last edited by a moderator:
Ndoa hizi!!! Haya zangu mie mboni tu, pole kaka!
 
Hapo cha muhimu tafuta watu wazima wamuone mumewe wamueleze kila kitu...halafu baada ya hapo acha kabisa kuwasiliana na wake za watu ............
 
Ngalikihinja ushauri wako mzuri sana,jamaa akiufuata utamsaidia

 
Andika sms hii umtumie HAJAKWAMBIA YA KUWA SIKO NAE KIHIIIVYO, KWA HIYO SIKUBALI KUACHIWA. KAA NA MKEO. Kisha subiria majibu.
 
Lara 1, kwenye maisha yako hadi leo, hujawahi singiziwa kuwa unatembea na fulani wakati si kweli? How did you handle it? Maana kuna wengine wakisingiziwa tu basi wanaamua kfanya kweli.

Mtu kama unajielewa huwezi kuhisiwa hisiwa!!! Haiwezekani mtu uendekeze mazingira tata afu ukihisiwa ujifanye kustuka!

Mimi waume za watu wote ikifika saa 2 baaas!!!!!!!!!!! Siwatafuti tena unlesss nijue mateja wa bar!
 

naunga mkono sana alichosema snow lakini niongezee kidogo
nahisi unaweza ukawa hujaoa, watu/vijana wengi hushindwa kujua mipaka ya kuhusiana na waume/wake za watu. kiukweli huyu mume kafanya maamuzi ya haraka na magumu ila, huwezi jua kama huyu jamaa alikuchunguza kwa urefu gani?? maana kuna technology nyingi siku hizi zinazowezakufatilia nyendo za wawili.

mimi nashauri kama ni suala la kusaidiana kazi si vizuri muendele kufanya hivyo. kuhusu sasa ufanyaje mimi nashauri mwache kwanza yeye atapata majibu on the way, unajua hadi mtu kufanya conclusion ngumu kama hiyo lazima kuna uchunguzi wa kina ambao wewe kama mtenda jambo huwezi jua kama ulifanya hivyo kiutani kumbe yeye akainasa kama sms, au kadi etc.then akaconclude.

upende usipende watu siku hizi si waminifu ktk ndoa zao. na mmomonyoko wa ndoa huanza kidogokidogo kama vile mchwa unapokula mti, then badae mti unaonekana mzima kwa nje lakini ukigusa tu unaanguka hata kwa kuni haufai. kuna combination ya mambo hapo! angekwepo JF na yeye mume amwage mashitaka yake ungeshangaa sana kiasi anachokutuhum. usichukulie rahisirahisi. kama umeoa uwe bize na mkeo bana.
 

There is a thin line btn TRUTH AND LIES!!!!!!!!!!
 
Mvaa Tai

Kumbe ni wewe unayeniharibia ndoa? Hili ni "onyo" la mwisho...!
 
Last edited by a moderator:
Kipi bora huyu dada angebaki ofisini kumalizia majukumu yake yenye deadline kesho yake asubuhi au aende akampokee mpenzi wake ila aendelee kuwasiliana na watu aliowaacha ofisini kupata msaada wa kumaliza kazi yake?
Tatizo inaonesha huwa unampigia sana kuhusiana na kazi hata kipindi ambacho sio cha kazi. We unafikiri utajisikiaje uko na mkeo unakula denda kwa raha zako. Mara kisimu
cha mfanyakazi mwenzio eti kazi za kiofisi. Inakeraa saana na hasa upokuja kufuatilia na kugundua mtu anayepiga na kupigiwa ni dume, tena mfanyakazi mwenzake. Au umesahau kuwa ofisi zetu siku hizi ni gest ndogo za kubinjuana. kubali umekosea na hukupaswa kuwa na mazoea na kivile kama dadako. Hivi wewe
Imagine akupigie saa mbili usiku unabinjuka na mkeo, unafikiri mkeo atakuchukuliaje. Umeharib toka mwanzo kaka angu. Hiyo ya mtoto imeongezea Imani zaidi kuwa wajisevia. Kwa ushauri wangu tafuta njia ya mme ajue hujala ili mkewe arudi Kwake, je kama huko alikotoka kuuguza mgonjwa yuko kwenye koma halafu anakutana na huu utumbo, eti badala ya wife kumfariji yuko busy na Ofisi
 
Silence speaks a lot than words. Sijui nini kinakuuma hapo!!! Kwani we ndiye uliyemtuma huyo dada kuolewa na dunya? We tulia zako, wala dhamira isikusute... wakisolve sawa, wasiposolve poa. By the way kwa jinsi alivyo huyo jamaa, bora tu hiyo ndoa ivunjike mdada akae kwa amani...
 

Huyu jamaa hajui tu kwamba mke anaye megwa hakamatwi kwa vimitego rahisi namna hiyo, mke anayemegwa unaweza usijue mpaka unakufa maana hujizuia sana kufanya mawasiliano na mzambi wake
 

ila mkuu mchunguze jamaa si ajabu anatabia y kudinya ovyo so anahisi na yeye wanamdinyia..

pole sana..
 
Well said mkuu
 
Hapo cha muhimu tafuta watu wazima wamuone mumewe wamueleze kila kitu...halafu baada ya hapo acha kabisa kuwasiliana na wake za watu ............

Kuacha kabisa kuwasiliana na wake za watu ni ngumu kidogo kaka, sema niache kuwasiliana na huyu dada kwasababu nishajua mmewe ana matatizo, tunawasiliana na wake za watu wengi tu katika maswala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kuweka huo mpaka itakuwa ngumu
 
Mkuu ndicho nilichosema tangu mwanzo kuwa huyu jamaa yetu Mvaa Tai alishalikoroga tangu mwanzo...Amekuwa karibu mno na mke wa mtu bila sababu za msingi..Na kama unakumbuka lara 1 alishawahi kuleta mada jinsi watu wa maofisini wanavyotafunana muda wa mchana...I second the guy mwenye wivu kwa kuliona hili na hii italeta heshima kati ya muda wa nyumbani na ofisini...Wakati mwingine kabla ya kulaumu tujaribu na sisi wenyewe kujiweka kwenye nafasi ya wengine...nimesafir..narudi unampigia simu mkewangu..usiku..huongei...na kwa nini namba ya mkewangu iwe bookmarked kwenye simu yako kwa kiwango hicho??


....angekwepo JF na yeye mume amwage mashitaka yake ungeshangaa sana kiasi anachokutuhum. usichukulie rahisirahisi. kama umeoa uwe bize na mkeo bana.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…