Naura spring hotel (Arusha) kubomolewa?

Kubingwa

JF-Expert Member
Apr 23, 2010
505
69
Habari za leo,wakuu!
Katika kupitia pitia magazeti leo,kuna gazeti moja limemnukuu N/W Ardhi na Maendeleo ya makazi kuwa majengo yote yaliyojengwa kando kando ya mito mjini Arusha yabomolewe akilitolea mfano naura spring hotel iliyopo kandokando ya mto themi.Hili jambo lishapigiwa kelele sana na wadau wa mazingira bila kupatiwa suluhisho.

Je,matamshi au maagizo haya ya mh.N/W kuitaka NEMC kufika Arusha ni nguvu ya soda au kuna nini nyuma ya pazia na je,walikuwa wapi (serikali kuu na mamlaka zake kuanzia mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi taifa) hadi lile jengo kusimama vile pale Sanawari-Arusha ?

Angalizo: Positive discussion na sio siasa wala majungu,ipotezeee,kama hauna la kuchangia.

Nawasilisha
 
Kama wataamuru libomolewe na vibali walitoa wenyewe itabidi walipe thamani ya jengo, gharama zote za kabla na baada pamoja na faida wataoikosa wamiliki kwa miaka itakayowachukua kujenga jengo lingine. Kuna uwezekano kabisa ni mbinu ya kujirudishia mtaji na faida ya haraka.

Nakumbuka majengo marefu ya Oyster-bay, yalibomolewa kwa mbwembwe, jamaa kashinda kesi na amelipwa kitita kuliko yasingebomolewa!

Kila action ina reaction.
 
Itabidi wabomoe na Police, Traffic na Fire.
Tatizo la maji Arusha siyo hayo majengo bali ni ukataji wa miti na kilimo kinachofanywa kando kando ya mlima Meru.
Pia kuna kilimo cha salad kinachofanywa katikati ya mto nacho ni noma.
 
Labda wanaGeologia wanaweza kunisaidia.
Mimi nafikiri Naura sprng Htl imejengwa pembeni ya mto Naura, na wala sio chanzo cha mto Naura. Hii paia inaonekana kwa majengo mengine mengi katika ukanda huo kuanzia ya NHC, makazi ya polisini n.k
Nadhani kinachowezekana hapa ni uchafuzi wa maji ya mto huo kwa majengo yao kuwepo karibu nao.
 
Habari za leo,wakuu!
Katika kupitia pitia magazeti leo,kuna gazeti moja limemnukuu N/W Ardhi na Maendeleo ya makazi kuwa majengo yote yaliyojengwa karibu na vyanzo vya maji Arusha vibomolewe.Hili jambo lishapigiwa kelele sana na wadau wa mazingira bila kupatiwa suluhisho.
Je,matamshi au maagizo haya ya mh.N/W kuitaka NEMC kufika Arusha ni nguvu ya soda au kuna nini nyuma ya pazia na je,walikuwa wapi (serikali kuu na mamlaka zake kuanzia mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi taifa) hadi lile jengo kusimama vile pale Sanawari-Arusha ?

Angalizo: Positive discussion na sio siasa wala majungu,ipotezeee,kama hauna la kuchangia.

Nawasilisha

Salaam Kubingwa;

Kwanza huyo aliyeyatamka huo ujasiri wa kutamka ukimwangalia usoni hana. Hana kabisa ujasiri huo lakini la pili hilo tamko si nguvu ya soda tu manake afadhali hata nguvu ya soda wakati mwingine yeye ameona Naura Spring tu???

Muulizeni kuna Hoteli inajengwa Sakina na ni ya mtu wake wa karibu sana na watu wa NEMC walianza kuhoji uhalali wa Hoteli hiyo kujengwa eneo hilo ambalo kuna mkondo mkubwa wa maji wakaambiwa nyamazeni ni wakubwa hao. Mbona asizungumzie hiyo Hoteli ambayo kwanza ni inaendelea kujengwa lakini pili haina tofauti na Naura Spring yeye anazungumzia ile ambayo imeshajengwa.

Embu awaache Watanzania bana asiwazingue na mamtamko ambayo kamwe hayatakaa na wala yeye hatoweza kuyasimamia kiutekelezaji manake kwanza locus standai hana na hata kama ana locus uwezo huo hatakuwa nao kwa sababu za kimaslahi na kama si sababu za kimaslahi embu Medeye leo atoe tamko kama hilo pale Sakina.........
 
Tatizo la jiji la Arusha wenyeji wanatamaa ya pesa wanauza mpaka mifereji na mito!
 
Itabidi wabomoe na Police, Traffic na Fire.
Tatizo la maji Arusha siyo hayo majengo bali ni ukataji wa miti na kilimo kinachofanywa kando kando ya mlima Meru.
Pia kuna kilimo cha salad kinachofanywa katikati ya mto nacho ni noma.

New Arusha Hotel pia
 
Nchi hii ni ya ajabu sana. Ina maana mradi kama ule ungetekelezwa bila ya kuwa na EIA report iliyopitishwa na NEMC? Na je Manispaa walitoa vipi Building Permit kama NEMC hawakutoa go ahead?
Msitegemee chochote kimpya kwani NEMC hiyo hiyo iliyotoa idhini kwenye EIA report awali haiwezi kubatilisha, la si hivyo itabidi hao watu wawekezaji wa Naura, walipwe fidia kubwa sana.

Ule ukuta wenyewe uliovunjwa kipindi kile baada ya Mh. Rais kwenda kuifungua ulileta mushkel kwa baadhi ya watendaji sembuse hotel nzima
 
Habari za leo,wakuu!
Katika kupitia pitia magazeti leo,kuna gazeti moja limemnukuu N/W Ardhi na Maendeleo ya makazi kuwa majengo yote yaliyojengwa karibu na vyanzo vya maji Arusha vibomolewe.Hili jambo lishapigiwa kelele sana na wadau wa mazingira bila kupatiwa suluhisho.
Je,matamshi au maagizo haya ya mh.N/W kuitaka NEMC kufika Arusha ni nguvu ya soda au kuna nini nyuma ya pazia na je,walikuwa wapi (serikali kuu na mamlaka zake kuanzia mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi taifa) hadi lile jengo kusimama vile pale Sanawari-Arusha ?

Angalizo: Positive discussion na sio siasa wala majungu,ipotezeee,kama hauna la kuchangia.

Nawasilisha

New Arusha iko kando ya mto, Equator iko kando ya mto, Mount Maru iko kando ya mto, Diwani Mathias anajenga kando ya mto, Jengo la Benki kuu liko kando ya mto, ofisi za TRA ziko kando ya mto, Ofisi za polisi na trafic mkoa ziko kando ya mto, ......fafanua unachotaka tikijadili
 
wakati inajengwa kuna kipindi ilisimama sana. Mgogoro ulikuwa wa aina mbili kwanza ni mazingira maana walikata miti mingi sana. Pili eneo lenyewe inasemekana linatitia sana kwa hiyo hakuna usalama kwa jengo refu kama lile maana ardhi haiwezi kulihimili. mara ghafla limeisha (maana walikuwa wanawahi mkutano wa sulivan). sasa leo mhu yetu macho tu!
 
Mtoa mada anashindwa kutofautisha kati ya ujenzi kando ya mto na ujenzi kwenye chanzo cha maji/mto.
 
dah! Wakibomoa watatunyima raha sana,c wengine ndo beach yetu ile,wana swiming pool safi sana
 
New Arusha iko kando ya mto, Equator iko kando ya mto, Mount Maru iko kando ya mto, Diwani Mathias anajenga kando ya mto, Jengo la Benki kuu liko kando ya mto, ofisi za TRA ziko kando ya mto, Ofisi za polisi na trafic mkoa ziko kando ya mto, ......fafanua unachotaka tikijadili
Mkuu yaani N/W amenukuliwa hivyo kuwa hiyo hotel iko kando kando ya mto na akahoji jeuchafu unaotokana na hoteli hiyo hasa maji machafu yanakwenda wapi na akafika mbali kuwa wakzi wa chini yaani huo mto unakotiririka wanakunywa ama kutumia maji yenye uchafuzi.nadhani nimeeleka,hoja ni je ni hii hotel tu au kuna majengo mengine na kwa nini ame base kwenye hoteli tu.au u mgeni kule arusha?
 
Mtoa mada anashindwa kutofautisha kati ya ujenzi kando ya mto na ujenzi kwenye chanzo cha maji/mto.
Mkuu ni typing error lakini imeeleweka hata kama ni kando kando ya mto,lile eneo lina chemchem na walipokuwa wanajenga palikuwa panatitia.so in that sense,eneo lile linachangia uwepo wa maji kwenye mto themi,usitoke nje ya mada tafadhali.tuendelee kupata mawazo mbadala,hasa kutoka kwa wana hydrolojia na wapenda mazingira
 
Hii hotel wakati inajengwa ujenzi ulisimama kutokana na kelele za wanamazingira! Lakini ghafla ikaja kuota kama uyoga kwa nguvu ya mafisadi,je tutarajie lolote kweli!!sidhani:nono:
 
Hii hotel wakati inajengwa ujenzi ulisimama kutokana na kelele za wanamazingira! Lakini ghafla ikaja kuota kama uyoga kwa nguvu ya mafisadi,je tutarajie lolote kweli!!sidhani:nono:
Ukumbuke pale pembeni kuna ofisi ya chama ambayo imejengwa kwa msaada wa huyu jamaa wa Naura, na ujenzi ulienda sambamba.
 
Kama wataamuru libomolewe na vibali walitoa wenyewe itabidi walipe thamani ya jengo, gharama zote za kabla na baada pamoja na faida wataoikosa wamiliki kwa miaka itakayowachukua kujenga jengo lingine. Kuna uwezekano kabisa ni mbinu ya kujirudishia mtaji na faida ya haraka.

Nakumbuka majengo marefu ya Oyster-bay, yalibomolewa kwa mbwembwe, jamaa kashinda kesi na amelipwa kitita kuliko yasingebomolewa!

Kila action ina reaction.

Sio rahisi ikabomolewa kwani mwenye hoteli alijenga Ofisi ya CCM pale Sanawari.
 
Back
Top Bottom