Halmashauri ya Arusha Matatani, Mahakama yaiamuru kulipa fidia ya Tsh Bilioni 1.7

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
726
1,575
Kaya zaidi ya 280 zimeathirika Kisaikolojia baada ya nyumba zao za kuishi na biashara walizojenga katika barabara Mianzini- Timbolo kuvunjwa na Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kufanya kuishi kwa kubangaiza .

Waathirika hao wamemwomba Rais Samia Suluhu Hassan aweze kuwasaidia kulipwa fidia ya shilingi bilioni 1.7 baada ya kushinda kesi mahakamani na halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia .

Nyumba 43 zilibomolewa na wananchi hao wamekuwa wakihangaika kule ya huko kutafuta haki lakini viongozi wa Halmashauri ya Arusha imekuwa ikiziba masikio na kuwaacha kama yatima na wasijue la kufanya.

Ombi hilo,wamelitoa kwa Rais Samia baada ya wananchi hao kushinda kesi katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa lakini halmashauri hiyo, imeshindwa kutekeleza agizo la mahakama .

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la tukio la uvunjwaji nyumba Mwenyekiti wa wananchi hao,Fanuel Titus Lamai ambaye ni Mwenyekiti wa Wahanga alisema walivunjiwa nyumba kutokana na kupanuliwa kwa barabara lakini Mahakama ilisema katika hukumu zake kuwa barabara ilifuata watu hivyo wananchi hao wanapaswa kulipwa fidia na sio vinginevyo.

Lamai alisema Jaji wa Mahakama Kuu Jaji Fatuma Masengi na Majaji watatu katika Mahakama ya Rufaa walieleza wazi katika maamuzi ya hukumu zao kuwa wananchi hao wanapaswa kulipwa fidia kwa kuwa nyumba zilikuwa nje ya sheria ya barabara hivyo barabara iliwafuta watu na wanapaswa kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria.

“Tunaiomba serikali yetu sikivu chini ya Rais Samia itusaidie tupate haki yetu kwa kuwa tangu mwanzo tulishinda mahakamani ila kumekuwa na shida kwenye utekelezaji wa amri ya mahakama.

“Tunaomba atusaidie tulipwe pesa zetu kwa ni haki yetu kwani baadhi yetu wamekufa kwa mshituko na wengine wamepooza mwili na hawajui la kufanya na wengine walikopa benki kujenga nyumba za kuishi na biashara sasa wako taababi kimaisha hawajui la kufanya’’alisema Lamai

Akizungumzia sakata hilo, alisema ilikuwa mwaka 2011 walipewa taarifa na halmashauri ya Arusha, kuvunja nyumba zao kando kando ya barabara kwa kuwa barabara ilitakiwa kupanuliwa.

Alisema walipopewa taarifa hizo, waliona hawajetendewa haki kwa kuwa wako nje ya barabara na wako nje ya barabara kwa mujibu wa sheria na walikwenda Mahakamani kufungua kesi na Mei 26 mwaka 2014 mbele ya Jaji Msengi walishinda na ilitakiwa walipwe fidia.

Alisema baada ya Jaji kutoa hukumu hiyo na wananchi hao kupeleka madai ya shilingi bilioni 6.8 ya wananchi 38 lakini Mthamini Mkuu wa Serikali alifanya Tathimini ya wananchi 32 waliokithi vigezo na kuitaka Serikali kuwalipa wananchi shilingi bilioni 1.7 tu na sio vinginevyo kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti huyo alisema baada ya hukumu halmashauri ya Arusha walikwenda Mahakamani na kudai kuwa hawakuwa na fedha za kufidia na Julai 7 mwaka 2015 mahakama ilitoa uamuzi kuwa kama hawana fedha basi barabara ibaki kama ilivyokuwa mwanzo kwa upana wa mita nane hadi hapo watakapolipa fedha za fidia.

Alisema mwaka 2016 Halmashauri ya Arusha ilikaidi amri ya Mahakama na kuamua kuwavamia na kuvunja nyumba zote zilizokuwa katika barabara Mianzini –Timbolo bila ya kuwafidia na wananchi hao walirudi tena Mahakamani na kesi ilisikilizwa Mahakama ya Rufaa Arusha chini ya majaji wa tatu na Agosti 25 mwaka 2020 walitoa uamuzi kuwa wananchi hao wanastahili kulipwa fidia

Naye Susan Joseph, mhanga wa sakata hilo mkazi wa Ilboru Wilayani Arumeru,alisema wamepata matatizo makubwa kutokana na uamuzi wa Halmashauri ya Arusha kuvunja nyumba zao bila kulipwa fidia kwani wengine walijenga nyumba za biashara na wengine walijenga nyumba za kuishi.

“Nikweli tumeathiri kutokana na adha hii, kwa kuwa mimi na familia yangu wakiwamo wajukuu ambao nawalea tulikuwa tunategemea kujikimu kimaisha,pia nilikuwa na mikopo mingi benki na baada ya kuvujwa nilishindwa kurejesha mkopo ya fedha niliyochukua na maisha yamekuwa magumu hivyo tunaomba Rais asikilize kilio chetu,”alisema.

Naye Agness Mollel,alisema hali ya utengenezaji wa barabara hiyo,imemuathiri sana kwa kuwa alikuwa mtumishi serikalini katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na alipopewa fedha za kustaafu alizitumia kujengea vyumba vya biashara vinne kando ya barabara hiyo.

Alisema kubomolewa kwa nyuumba yenye vyumba hivyo kumefanya kubaki katika hali ya ukiwa,shida na njaa kwa kuwa hana kitu cha kula alikuwa anategemea vyumba hivyo.

Akizungumzia sakata hilo Mwanasheria wa Halmashauri ya Arusha,Monica Mwailolo alisema kuwa kesi hiyo walikuwa wakishirikiana na ofisi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa maamuzi mapya ya Jaji J.Kamala yaliyosistiza wanachini hao lazima walipwe fidia lazima awasiliane na ofisi hiyo kwa maamuzi zaidi.

Mwailolo alisema kwa sasa sina la kujibu zaidi ya kusema kuwa atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia hilo pale watakapo kaa na kutoka na maamuzi ya pamoja.

Ends...

IMG-20220607-WA0143.jpg
 
  • Thanks
Reactions: ffn

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
16,579
17,767
Alisema mwaka 2016 Halmashauri ya Arusha ilikaidi amri ya Mahakama na kuamua kuwavamia na kuvunja nyumba zote zilizokuwa katika barabara Mianzini –Timbolo bila ya kuwafidia na wananchi hao walirudi tena Mahakamani na kesi ilisikilizwa Mahakama ya Rufaa Arusha chini ya majaji wa tatu na Agosti 25 mwaka 2020 walitoa uamuzi kuwa wananchi hao wanastahili kulipwa fidia

Wahanga wa maamuzi ya kimabavu ya serikali ya CCM ya JPM hivyo kwa wastani kila raia ktk nyumba hizo anadai shilingi 40,000,000 kama fidia.

Hiyo barabara ingekuwa Kenya lazima kwanza unapewa fidia kabla ya nyumba kubomolewa ili kupisha mradi wa barabara lakini Tanzania mwananchi anahangaishwa.

The project on the Kenyan side is estimated to cost US$85 million while the Tanzanian section (dual carriageway and bypass) will cost approximately US$353 million.
1654713534406.png


His Excellency Dr. John Pombe Magufuli, President of The United Republic of Tanzania and his counterpart from the Republic of Kenya, His Excellency Uhuru Kenyatta will on Thursday 3rd March, 2016 do the ground-breaking of the construction of the Arusha - Tengeru Dual Carriageway and Arusha Bypass Road at Tengeru, in Arusha Region, Tanzania. The historic event will be witnessed by the other Members of the Summit of Heads of State from the Republics of Burundi, Rwanda and Uganda.

The road is part of the Multinational Arusha - Holili/Taveta - Voi Road, which is a successor to the Arusha - Namanga - Athi River road that was completed in 2012. It forms part of the larger East African Road Network consisting of 15,000 km of international highways, and part of the Trans African Highways (TAH) No. 8 from Cape Town to Cairo via Gaborone.

Work on the Kenyan section of the project, from Taveta to Mwatate, commenced in May, 2014 and was launched in September, 2015 by H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, the then President of The United Republic of Tanzania and H.E. Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya, at Taveta in Taita Taveta County.

The scope of the construction consists of upgrading from gravel to bitumen surface of 90km of the road, part of which traverses the Tsavo West National Park. The finished road will have a 7-m wide carriageway and 2-m wide shoulders on both sides. There will also be a 9-km long bypass around Taveta Town to reduce congestion and enhance road safety in the town. It is expected that travel time will be reduced from 4 hours to 1.5 hours along this stretch.

The scope on the Tanzanian section, which commenced in June, 2015, includes the upgrading of the current two-way, 13-m wide road to a four-lane, 26-m wide highway from Sakina to Tengeru, a distance of 14 km. Service roads will be provided on both sides to facilitate the movement of local traffic. New bridges will be constructed alongside the existing ones on the new road. It is scheduled for completion in March, 2018
 

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,083
3,269
Naomba kueleweshwa, hiyo Halmashauri ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha ndio ipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom