Mandesy
Senior Member
- Mar 22, 2018
- 115
- 125
Tukiwa bado tunatafakari mabadiliko ya mara kwa mara ya baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya tano, hali inaonekana sio shwali ndani ya chama hicho.
Nasema hali sio shwari, kwani kila mtu amekuwa na hofu kubwa, hasa wale wadadisi ndani ya chama. Inavyoonekana kwamba sasa hivi JPM ameamua kuwafunga midomo CCM na yeyote atakayeibuka kusema kitu ambacho ni tofauti na fikra za mwenyekiti wa chama na Musiba et al, basi akumbuke kwamba, nafasi yake ndani ya chama itakuwa ni finyu sana.
Ndio maana, leo utaowaona akina George Kahama, Malechela, Mkuchika, Lukuvi ambao miaka ya 80 walikuwa vijana wakiendelea kuhudumu serikalini toka serikali moja kwenda nyingine na wamekuwa wakiheshimiwa hadi hivi leo.
Leo hii kuwavuruga Nape, Mwigulu, Makamba nk, ambao ni miongoni mwa vijana wenye ushawishi CCM, sio kitu kizuri na kinaweza kuharibu afya ya chama.
Hivi majuzi, tumeona bwana anayejiita Musiba akiendelea kuwadharirisha wazee wa chama kwa kuwakashifu hali iliyosababisha wazee hao kutoka hadharani na tamko ambalo limesababisha mjadala mkubwa miongoni mwa watanzania.
Ikumbukwe kwamba, mwaka 2015 kwenye sakata la kura za maoni CCM, hakuna aliyejua kwamba JPM atapenya kwani mchuano ulikuwa mkali sana. Bila wazee wa CCM, basi JPM asingepenya hata nafasi tano..leo hii huenda Membe, Makamba, ama wale akina mama wa Zanzibar ana Lowasa, mmoja wao angekuwa rais.
Maisha ya watanzania yamebadilika sana tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani. Njia kuu za uchumi zimeharibiwa na fedha zote zimeenda kwenye mikondo ya serikali, ambayo kwa mbwembwe zinaishia kununua ndege, madaraja nk, vitu ambavyo havijengi kabisa social capital. Tujifunze kwa Nigeria.. imeendelea sana lakini gap la maskini na tajiri ni kubwa sana hali inayosababisha wanigeria wengi kukosa imani na nchi yao na wengine kukimbia nchi.
Kwa sababu hizi nne, ninaona muelekeo wa CCM sasa huenda ukawa mbaya kwani CCM wanajulikana jinsi wanavyozika vichwa vyao ardhini na pale wanapokugeuka hutaamini kwamba ndio wao
Marijani Kyomo
Maruku, Kagera

- Kuwavuruga vijana

- Kuwavuruga wazee

- Kuwavuruga watanzania
Maisha ya watanzania yamebadilika sana tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani. Njia kuu za uchumi zimeharibiwa na fedha zote zimeenda kwenye mikondo ya serikali, ambayo kwa mbwembwe zinaishia kununua ndege, madaraja nk, vitu ambavyo havijengi kabisa social capital. Tujifunze kwa Nigeria.. imeendelea sana lakini gap la maskini na tajiri ni kubwa sana hali inayosababisha wanigeria wengi kukosa imani na nchi yao na wengine kukimbia nchi.
- Kuleta ukabila