Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,312
- 105,667
Tanzania kuna ubaguzi sana tu.Aiseee!
Nikishasikia haya hadi kwa nchi ambayo huwa naiona kama ya mfano kwenye civilization.Huwa naona bora nifie huku huku bara la giza, nipambane na wakina jiwe.
Sipendi kabisa kubaguliwa hata kama kwa kiasi kidogo, hasahasa kubaguliwa na ngozi nyeusi kama yangu.
Mfano. Watu wenye sifa nzuri lakini wanakosa ajira kwa sababu hawana ndugu wenye majina makubwa na nafasi, wanabaguliwa.
Nilivyoanza kufanya kazi Dar, nilikuwa nachukizwa sana na mawazo ya watu wengi niliokuwa nawaambia nimeanza kazi sehemu fulani. Kitu cha mwanzo kuniambia kilikuwa "Mzee amekuunganishia eeh?". Wakati kazi nilitafuta mwenyewe, hiyo "Mzee" alikuja kuambiwa baadaye.
Nikaona labda nikienda nchi ambayo watu hawamjui "Mzee" wangu, nitaweza kutambulika mafanikio yangu kama yangu mwenyewe, si ya kutumia mgongonwa "Mzee".
Akili za wengi zimekaa kutoangalia ubaguzi anaofanyiwa Mtanzania na Mtanzania mwenzake, hata ukiwa mkubwa.
Wakati mzungu akikupisha kiti kwenye basi tu, kwa sababu tuna tamaduni tofauti za "personal space", sisi tunaona kubanana ni sawa, wenzetu wanaona si sawa, kwa mtu yeyote tu, sisi nibwepesi sana kuona hapo umepishwa kwa kubaguliwa.
Kuna tangazo la kazi nililiona, linataka mtu anayewania nafasi ya kawaida tu aongee lugha ya Kigujarati. Hiki kigezo kimsingi kinamaanisha Wahindi walikuwa hawataki Mtanzania mweusi afanye kazi hiyo. Nchi kama Marekani sheria kama za Equal Opportunity zinakataza mambo kama hayo.
Tanzania hatuna sheria kama ya Equal Opportunity ya Marekani.
Ni rahisi kufanya institutional discrimination Tanzania kuliko nchi kama Marekani.